Kwa mujibu wa Taarifa ya habari ya Radio one ya saa mbili usiku wa leo
Kenya imeajiri waalimu laki moja ndani ya miaka mitatu na inatarajia kuajiri wengine 20,000 kabla ya mwisho wa mwaka huu; kufanya iwe imeajiri waalimu takribani 40,000 kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo. Nafikiri hii inatufanya tuone kabisa kuwa hakuna Nchi ya ukanda huu ya kuweza kushindana na Kenya kwenye uwekezaji katika Elimu.
Kwa wasiofaham ni kuwa kwa Kenya shule za Msingi na Shule za sekondari za Serikali ndio kimbilio la wengi kutokana na ubora wa hali ya juu wa Elimu inayotolewa huko na sio kawaida kusikia shule ya msingi au Sekondari ya umma haina waalimu sijui wa wa Hesabu au Sayansi.
Uwekezaji katika Elimu kwa kipindi hiki una manufaa sana kwani unafanya vijana kwa maefu waweze kuchangamkia fursa za kimataifa na hivyo kupunguza ukosefu wa ajira lakini kuongeza pato litokanalo na diaspora