VIDEO: Hizi hapa faida za ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Misri

Hebu weka ushahidi hapa,laa sivyo ni Udaku tu.
damedamn.png
 
Ushauri wa bure: Kutamka sahihi majina ya watu, hasa wakuu wa nchi ni kielelezo kikubwa cha jinsi ya elimu yako ya yanayojiri duniani, jinsi unavyowaheshimu au kuwajali na jinsi ulivyo serious. Hapa Waziri wetu wa Mambo ya nchi za Nje anamtamka rais wa Misri "Ali Alsis' jina ambalo ni tofauti kabisaa na linavyoandikwa na kutamkwa. Kweli, kama kiongozi wa dilomasia huwezi kuchukua dakika kumi ukasikiliza linavyotamkwa? Tena siku hizi hata kwenye Google wanakupa matamshi. Ni kwa sababu hiyo hiyo walimpotosha rais naye akalitamka ' Al-sis' badala ya 'As siisi', nikaona midomo ya baadhi ya Mawaziri wa Misri ina 'pout' kwa kumsikia mgeni anashindwa kutamka jina la mwenyeji wake! Kama Waziri wa Mambo ya nchi za Nje lazima utamke sahihi majina ya viongozi unaokutana nao au anaokutanan nao rais, no excuses!
Halafu Misri siyo kama Comoro kuwa rais wake hajulikani. Ni nchi ambayo kila siku iko katika vyombo vya habari duniani.
Watanzania tuna tabia iliyojikita ya kuchukulia kila kitu kuwa kawaida tu, noma, bila kujiandaa au kujiandaa dakika ya mwisho. Ndiyo maana hatuendi popote!
Sio rahisi kuweza kutamka kila jina namna linavyotamkwa huyo Mama yupo njema sana kwenye lugha ya malkia ambayo ndio kiswahili cha dunia.
 
Ningeomba sana mchango wangu kuhusu kinachoandaliwa kati ya serikali yetu na Egypt uwekwe hai kwa muda usioungua miaka mitano lakini ifike hata kumi.
Egypt ni nchi yenye siasa hatarishi sana kwa nchi zote zilizoko chini ya jangwa la sahara. Kila ujanja unatumika kusimamisha maendeleo ya nchi nyingi za Africa. Wao hujiona ni waarabu na siyo waafrika. Nchi yoyote ambayo mto Nile umepitia ikigusa yale maji kwa mradi wa maendeleo ya nchi husika hujikuta kwenye matatizo, ujasusi wa kila aina utafanyika hata kusababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe. Sitataja mfano kwani upo ulio hai. Mkataba wa kujenga mtambo wa kufua umeme tumewapa inasemekana wameujenga kwa mitabo chakavu ya miaka 1980. Tungoje tuone utatufaa kiasi gani. Ninaamini kabisa pale tumepigwa tena vibaya. Sasa tumejipeleka wenyewe kwenye mdomo wa chatu.
 
Mkuu ukweli ni upi?
 
Back
Top Bottom