Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Nimejikuta natetema kwa hasira baada ya kuona mtu kaanguka na kapoteza fahamu huku huyo huyo mtu alisababisha apoteze faham anasema DAR ES SALAAM OOYEEEE! Atupishe siye tunaendele kuchapa kazi.... Daaah watu ni wanyama zaidi ya mnyama[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]

Nasubiri tamko la vyama vya wafanyakazi, asasi na azise zinazotetea haki na utu
 
Duu...nafas ya utu inapokwa na "politics"...ila,kuna mbegu inapandwa na kukuwa kwa kasi,time will tell.
 
Kama hujakutana na hao jamaa unaweza kumlaumu sana RC but hao jamaa wanaumiza na kuliza watu wengi sana yaani ndio maana hata yeye kazimia maana anajua kinachofuata. Hana sifa za ukuu wa idara sasa kukaimu tu imekua tabu kwetu wanakera sana aisee bora awatoe tu wote hii Tanzania sio yao kitu kidogo unazungushwa kama unaomba roho ya mtu vile
Tahadhari usihukumu kwa kuwa unanafasi ya kufanya hivyo. Hata muuaji hupewa haki ya kusikilizwa na hata amapohukumiwa kifo bado hupewa faraja ktk nyakati zake za mwisho. Sipingi mtu kuchukuliwa hatua lkn hatua itakayochukuliwa izingatie taratibu zilizowekwa na kama tunaona ni mbaya basi tubadili kwanza taratibu ili kutupa uhalali wa haya tuyafanyayo. Vinginevyo watu wengi wataumia kwa maamuzi yasiofuata taratibu
 
Kwa iyo ee chama chako kikitawala kitale uzembe wa hati tatu tatu kwenye kiwanja kimoja!?
Ndo maana kuna onyo kwa mdomo, kwa barua. Hatimaye kufukuzwa kazi.. wew unadhani Makonda yupo perfect?? Hana kosa hata moja kwenye utendaji wake wa kazi?? Sisemi wazembe waendelee kuwepo kazini ila utaratibu uliowekwa kisheria ufuate.. kesho anaweza kushika mwingine na akatumia vibaya madaraka yake na matukio kama haya ndo yatakuwa reference yake
 
Mie nimejikuta nacheka coz sijamuelewa huyo jamaa kilichomfanya aanguke na kuzimia,kwani kushushwa cheo ndo nn,cheo ni dhamana na hata kazi unatakiwa kujiandaa wakati wowote
 
Makonda sijui kwann ccm wamechelewa kumleta? Alitakiwa afanye kazi na sokoine
 
Kwahiyo kushushwa cheo ndo kumfanya aigize kufa? Alitaka kuvuruga mkutano tu, tena ashitakie kwa kuleta fujo
 
Ingewezekana watu wa ardhi Tanzania wakazimia wote ingekuwa pomba sana, ni wazulumati , waomba rushwa ,wababaishaji mno.
 
Siku kubwa ya kuwa kiongozi ni hekima na maarifa...sijaona chochote kwa huyu mungu mtu...
Anashindwa kuelewa utu na ubinadamu hatimae anafanya mambo kwa sifa akitegemea ataonekana bora zaidi na kusifiwa kumbe ana jiharibia..hamna kitu hapa kama anaufukuzia ubunge au uwaziri basi imekula kwake
 
Ili kuepuka madhira kama haya, kama wewe ni hard worker na risk taker, kuna mambo mawili yatakayokufaa. Kufanya Kazi private ama ujiajiri mwenyewe! Mambo ya kusimamishwa hadharani kama haya na kutishiwa ugali wako yatakuwepo kidogo sana!
Mie ni mtumishi but sijui kunyenyekea mtu coz Niko tayari anytime kisaikolojia na kimkakati kwa whatever happen,mtu kama huyo ana mda marefu kazini kwa nn awe na pressure kiasi hicho,watu wajifunze kuishi kwa tahadhari unless hajawahi Fanya kazi private sector kule kuna pressure na kudhalilishana kuliko huko.
Nimewahi kutumbuliwa na boss na matusi juu, salary ilikuwa million moja kwa mwezi,kosa operator alizembea,piston za grader ziliungua coz maji yaliisha,kosa sikufanya mm but kwa kuwa nilikuwa boss wao wakanitumbua tena baada ya miezi 5 tu.So tujifunze kukabiliana na pressure na njia nzuri ni kuiweka akili ikubali kuwa wakati wwte ulichonacho kinaweza kuwa upside down.This goes hata kwenye mambo ya mahusiano kujinyonga sio dili,tuishi kwa tahadhari na matumaini yanayohimilika
 
Mie sijaelewa, aliyeshushwa cheo mwingine ilipofika zamu yake kavunga kufa ujanja wa kishamba sana
 
Kumbe na huyu Muro inaelekea maelekezo alikuwa anapata kutoka kwa Bashite, make namuona naye anajimwayamwaya! Bashite yeye alipewa madaraka ya kulevya sasa kasahau kwamba Baba yake hawezi kutawala kifalme ni miaka kumi tu kama akienda zaidi. Na hapo ndo watamgeukia aliokuwa kazoea kuwageukia.
 
Hayo mambo yalishapitwa na wakati, kama hutaki kudhalilishwa, timiza wajibu, au achia ngazi, sio kila ukiulizwa wewe hujui.
Wanaofutilia haki kwenye ofisi zao huwa wanakatibishwa chai!?
Kwani we unafikiri huyo bashite zero nayeye ukimkazia ukamuuliza maswali kwenye hiyo nafasi yake atakujibu yote??!,, si na yeye ataanza tu kutetemeka tetemeka???
 
Watumishi wa umma wakivurunda lawama inabebeshwa ccm ipambane nao tu, haiwezekani watu wakauke koo majukwaani wakisaka kura mwingine alete mambo ya kijinga ofisini kamtu hata elimu hakana angekafukuza na viboko juu
 
Nimesikitika na kuhuzunika sana nilijaribu kuwa ktk viatu vya huyu mkuu wa idara wallah imenisononesha. Inawezekana kuna majibu mazuri angeweza kuwa nayo na pengine ni mtendaji mzuri aliekosa kueleza anayoyataka muheshimiwa. Najua kuna uwezekano mkubwa wa huyu mkuu wa idara kukosea data lkn haikupasa afanyiwe haya. Tunao utaratibu maalum wa kushughulikia mambo kama haya. Hivi tujiulize kama mkuu wa mkoa angewapa nafasi ya kumpa data kamili ingeharibu nini. Kisha nashindwa kuelewa hivi kila lalamiko ni mgogoro? Maana kama nimesikia vizuri mkuu wa idara kaulizwa kuhusu Migogoro na si malalamiko ambayo mkuu wa mkoa anatakwimu zake. All in all RC hakuitendea haki nafasi yake. Hakuthamini thamani ya utu wa mtu kwani hata pale mtu alipoanguka bila kujua amepata athari kwa kiasi gani aliimba nyimbo kuonesha alichokifanya yuko sahihi. Wananchi pia wamenifedhehesha sana wakati mtu ameanguka akipigania uhai wake watu wamekosa ubinaadamu wakaanza kushangilia... Upo wapi upendo wetu....
Msimlaumu makonda,mbona hii serikali ya sasa kuanzia kichwani hadi miguuni ina staili hii ya utendaji,why watendaji wasicheze kwa step zake,kuwa mkubwa kwa sasa si salama
 
Back
Top Bottom