Vibanda vya Machinga Complex vyabomolewa, Machinga wahaha

Vibanda vya Machinga Complex vyabomolewa, Machinga wahaha

Nadhani tunafanya makosa kuhusisha siasa kwenye kila kitu.
Haiwezekani Machinga wajengewe jengo la kufanyia biashara kisha wao walikache na kujijengea vibanda ili wasilipe kodi. Kama tatizo ni bei juu basi wangeunda timu ya kukutana na mamlaka husika kulalamikia hilo lakini si kujiamlia kujenga wakati vyumba bado vipo.
Tabia ya watu kujiamlia kufanya wanayotaka hata wasiporuhusiwa imeshamiri. Ukichunguza kwenye vituo vya daladala, daladala nyingi hazipendi kusimama na kupark kwenye vituo. Nyingi zinavizia pembeni kabla ya kutuo na wakati mwingine zinapiga foreni barabara kila mmoja akitaka kuwa nyuma ya mwingine huku sehemu za vituo zikiwa wazi. Inashangaza kweli. Ukienda kwenye vituo ambavyo vimejengwa mahususi kwa ajili ya abiria, tayari vimevamiwa na wafanyabiashara ndogo. Utakuta wamepanga bidhaa zao na wengine wameweka meza na mianvuli huku sehemu za abiria zikiwa ndo seat za kukaa au meza.
Nadhani ifike mahali watu waheshimu taratibu bila itikadi. Mji lazima uonekane ni mji kwa mpangilio na taratibu.
 
Hao wametokea mikoani, wanajisaidiaga vichakani eti mizimu inawazuia kujisaidia chooni
 
Kwanza wangerudishwa huku vijijini .Uchuuzi huu unaliangamiza taifa kwa njaa.Vijana wenye nguvu wanashinda brbrn, mashamba hayana watu wa kuyahudumia, chakula kinapanda bei tunalalama, wazalishaji hakuna.Haiwezekana kila mtu anataka kuwa na duka au kuwa machinga.
 
Je walikuwa wanafanya biashara kwenye majengo yaliyoidhinishwa?? ama kutusumbua.
 
Aisee mbona mkulu alisema wasiondolewe mpaka watakapo pewa maeneo ya kuhamia, au ilikuwa ahadi hewa
Alikuwa anatafuta kiki na aliipata sasa swali lilipo aulizwe je hawa watu wamepewa nafasi kuingia ndani wamekata.nachofahamu mimi nafasi zote zimejaa ila ukienda ndani ya machinga vibanda vingi viko tupu.
 
Kwa kweli machinga wapo huru sana siku hizi, wanaziba barabari na huwambii kitu. Jeuri wameitoa kwa Pombe.

Sifurahishwi na shaghala bhagala iliyopo DSM kwa sasa. NI UCHAFU UCHAFU UCHAFU MPAKA NJIA YA KWENDA IKULU
 
Inasikitisha sana kwa kweli. Na wengi waliokuwa na vibanda pale ni walemavu
Nilikuwa nawaonea huruma sana walemavu na ni vema huruma kwao iendelee. Lakini kuna hawa walemavu bazazi waendesha bajaji za kariakoo-feri ni balaa. Wana matusi, jeuri, sheria za barabarani wao kama haziwahusu. Navichukia sana hivi vijamaa. Kuna mtu alichukizwa na kilema mmoja akasema labda Mungu alikupa kilema kwa vile ungekuwa mzima ungesumbua zaidi.
 
Zoezi la ubomoaji vibanda vyote vya biashara katika jengo la Machinga Complex Ilala , Dar es salaam, limewaacha wengi kwenye majonzi.

Wafanyabiashara hao kwa masikitiko zaidi wanasema kubomolewa vibanda vyao vya biashara na uharibifu wa Mali zao ni uonevu na wao hawana la kufanya.

Kuna taarifa zingine zinasema wafanyabiashara hao walitafadhalishwa na uongozi tokea awali kwamba wabomoe vibanda vyao na wahamie ndani ya Jengo hilo la Dar es salaam Business Park, au Machinga Complex.

Wafanyabiashara wamewasha moto katikati ya barabara eneo la Machinga Complex jijini Dar baada ya kukuta vibanda vyao vimevunjwa.



View attachment 490617 View attachment 490618

Hiyo ndio hapa kazi tu
" policy implementation"
 
Nilikuwa nawaonea huruma sana walemavu na ni vema huruma kwao iendelee. Lakini kuna hawa walemavu bazazi waendesha bajaji za kariakoo-feri ni balaa. Wana matusi, jeuri, sheria za barabarani wao kama haziwahusu. Navichukia sana hivi vijamaa. Kuna mtu alichukizwa na kilema mmoja akasema labda Mungu alikupa kilema kwa vile ungekuwa mzima ungesumbua zaidi.
Kwa hilo la Bajaj za feri nakuunga mkono
 
Na kodi wamepandishiwa na TRA toka 300,000 kuwa 800,000
 
Na kodi wamepandishiwa na TRA toka 300,000 kuwa 800,000
 
Back
Top Bottom