• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Viatu vya mchuchumio vinavyowatesa wanawake…..!

Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000


Viatu vya kisigino kirefu au mchuchumio vimekuwa ni maarufu sana siku hizi, karibu kila mwanamke anavutiwa na aina hiyo ya viatu, awe ni mwembamba au mnene, mrefu au mfupi wote wanavutiwa na viatu hivyo. Lakini wale wanawake wafupi ndio zaidi, hupenda aina hiyo ya viatu ili kuonekana ni warefu, ufupi umekuwa kero kwao, ajabu eh…!

Lakini kwa bahati mbaya uvaaji wa viatu vya mchuchumio huwa unawasumbua sana wanawake wengi, sio tu kuwasumbua, bali hutokea kutembea vibaya kiasi cha kuwafanya kuwa kichekesho na hata ule uzuri walioutarajia unakuwa haupo. Kwa hiyo mwanamke anakuwa kituko badala ya kupendeza.

Tafiti mbalimbali zimebainisha kwamba, viatu hivi vimewahi kuwaumiza sana wavaaji na hata kuwauwa pia. Pamoja na kuumia au kufa, kuna kuingia katika aibu kwa kushindwa kutembea vizuri na kugeuka kituko.

Inashauriwa kwamba ni vyema wanawake wanaopenda kuvaa viatu hivyo wafanye mazoezi ndani kabla hawajaanza kuvaa viatu hivyo vya mchuchumio hadharani. Kwa kufanya mazoezi kutawaepusha na ajali au fedheha watakapokuwa wanatembea barabarani……….

Ujumbe huu uwafikie wafuatao:
cacico, gfsonwin, snowhite, lara 1, Lisa, Ciello, charminglady, nivea, FirstLady, sweetlady, AshaDii, King'asti, @FP, Preta, marejesho, Madame B, na wanyange wengine watumiao aina hiyo ya viatu..............

 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Ni hatari kwa kweli............!

 
Z

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2007
Messages
9,381
Points
0
Z

Zero One Two

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2007
9,381 0
Ni hatari kwa kweli............!

Huyu nime mtamani kweli ili anapatikana wapi? Ndio mambo ya fashion mzee wangu, ila tatizo watumiaji hawjijui aina ya vitu vya kuvaaa
 
Fixed Point

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
11,312
Points
1,225
Fixed Point

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2009
11,312 1,225
hayo uliyoyasema yapo sana na madhara yake ni makubwa mno, watu hawajui tu......
mimi huwa navaa viatu virefu kwenye hafla ambayo najua sitakuwa na mizunguko mingi. na kama kwenye sehemu ambayo nitakuwa na mizunguko sana na ni lazima nivae viatu virefu sababu ya nguo ambayo nimevaa basi nitavaa viatu ambavyo vipo comfortable sana, kiasi kwamba hata naweza kukimbia navyo......
pamoja na hayo madhara uliyoyasema, hivi viatu huwa vinaumiza sana migongo ya wamama hapo baadae
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Huyu nime mtamani kweli ili anapatikana wapi? Ndio mambo ya fashion mzee wangu, ila tatizo watumiaji hawjijui aina ya vitu vya kuvaaa
Mimi wakati mwingine huw anacheka sana huko barabarani, ukiwaona dada zetu kwenye mitoko jinsi wanavyotembea utadhani bata...
Yaani mpaka unajiuliza, 'kavalishwa...!'

Najua ni mambo ya fasion, lakini fasion si kuvaa tu, bali pia na kumiliki kile unachokivaa sio kikumiliki wewe..........!
 
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,229
Points
1,500
AshaDii

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,229 1,500
Mtambuzi,

Kiatu hufanya nguo uliyovaa ishuke thamani ama ionekane ya thamani zaidi. Na kiatu pia huchukuliwa kawaida na watu wengi but viatu iwe kwa mwanamke ama mwanaume huongea lugha yake ya kipekee kabisa. Huwezi vaa viatu virefu kila mahala, ila bana mahala ambapo kiatu kirefu kinatakiwa ni kujikaza kwenda mbele but unakufa navyo hadi huko unakoenda kieleweke. Hiyo picha umeweka hapo, pamoja na uzuri wote na figure iliyo Perfect, kiatu kimecheza nafasi ya yeye kuwa more hot..

Mahala kama mtoko mkubwa wa usiku, Mkutano hasa hii ya Co-operate world, na sherehe mbali mbali hasa hizi za Cocktail ni lazima utokelezee na kiatu kirefu. Umuhimu huu ndio hasa unaeleza why akina dada/mama siku hizi wanatembea na viatu pair mbili, flat (sandals) na heels, akitoka tu nje ya mahala husika anaweka mbadala. Kiatu kirefu makes akina dada aonekane sexy and extra hot pia hata kuwa upo sophisticated Siku moja nikipata nafasi nitatoa viatu vya kike na kiume vya aina mbali mbali hutoa ujumbe gani kuhsu mhusika... Lol.
 
Neylu

Neylu

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
2,831
Points
1,500
Neylu

Neylu

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
2,831 1,500
Mimi na huu ungongoti nilionao nikivaa viatu virefu nakuwa kama jini..!

Viatu hivyo huwa navivaaa pale tuu inapobidi..!

Ila ni kweli huwa vinanikong'oli sana viatu vya mchuchumio..!!
 
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Messages
4,131
Points
0
Songoro

Songoro

JF-Expert Member
Joined May 27, 2009
4,131 0
Inaharibu shepu ya mguu ukipendelea kuvaa mara nyingi.
 
Tized

Tized

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Messages
4,023
Points
2,000
Tized

Tized

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2012
4,023 2,000
Bora sisi wanaume hatuvai, maana akina sisi tuna matege, viatu soli zinalala 45 degree na daladala zetu kupata siti labda uwahi ya dereva. yaani Mtambuzi 'Mzee wa kalma' sipati picha ingekuaje? lol.
 
Dero

Dero

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2010
Messages
329
Points
225
Dero

Dero

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2010
329 225
Ninaelewa mimi, mchuchumio humfanya mwanamke aonekane sexy na k-lady zaidi, hasa akitembea unless mtu hajazoea high heels.
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Mtambuzi,

Kiatu hufanya nguo uliyovaa ishuke thamani ama ionekane ya thamani zaidi. Na kiatu pia huchukuliwa kawaida na watu wengi but viatu iwe kwa mwanamke ama mwanaume huongea lugha yake ya kipekee kabisa. Huwezi vaa viatu virefu kila mahala, ila bana mahala ambapo kiatu kirefu kinatakiwa ni kujikaza kwenda mbele but unakufa navyo hadi huko unakoenda kieleweke. Hiyo picha umeweka hapo, pamoja na uzuri wote na figure iliyo Perfect, kiatu kimecheza nafasi ya yeye kuwa more hot..

Mahala kama mtoko mkubwa wa usiku, Mkutano hasa hii ya Co-operate world, na sherehe mbali mbali hasa hizi za Cocktail ni lazima utokelezee na kiatu kirefu. Umuhimu huu ndio hasa unaeleza why akina dada/mama siku hizi wanatembea na viatu pair mbili, flat (sandals) na heels, akitoka tu nje ya mahala husika anaweka mbadala. Kiatu kirefu makes akina dada aonekane sexy and extra hot pia hata kuwa upo sophisticated Siku moja nikipata nafasi nitatoa viatu vya kike na kiume vya aina mbali mbali hutoa ujumbe gani kuhsu mhusika... Lol.
Heshima kwako Da AshaDii......

Ahsante kwa maoni yako mazuri, nadhani sasa ni wakati muafaka kwa Mods kuangalia uwezekano wa kuweka jukwaa la fashion ili members wapate kuelimishana humo kuhusu aina ya mavazi ya kuvaa na how to practice. jamani huko maofisini ninakopita, (msishangae mimi ni MACHINGA) nakutana na vituko kila uchao, hususan kwenye majengo marefu halafu ukute hakuna elevator siku hiyo utachoka jinsi wanyange wanavyoziparamia ngazi na hivyo viatu.........Ye uuuwi...!!!!!!!

Wengine mpaka wakifika juu, utawaonea huruma..................
 
Last edited by a moderator:
Fixed Point

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
11,312
Points
1,225
Fixed Point

Fixed Point

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2009
11,312 1,225
Halafu uwe na usafiri wa Tz 11 ikisaidiwa na treni ya mwakyembe mbona utakoma...ndio maan wanawake siku hizi tuna vigimbi
sasa rafiki mchuchumio kwenye treni unafanya nini tena? lol!
mimi huwa nashangaa wadada wanaosafiri na michuchumio, yaani natamani kuwaamkia, lol!
hivyo viatu vinapendeza sana ila sheshe lake nalo si mchezo
 
Asnam

Asnam

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Messages
4,261
Points
1,225
Asnam

Asnam

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2012
4,261 1,225
afadhali hujanitaja mbona yangekushuka shuuu
 

Forum statistics

Threads 1,402,829
Members 530,989
Posts 34,406,243
Top