Vatican inamiliki dunia

2013

2013

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
9,804
Points
2,000
2013

2013

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
9,804 2,000
Tuanze wewe mwenyewe basi! Kwa mujibu wa post yako hapo, Uislamu ulianzishwa kutokana na Mfumo wa Pope Bill. Mambo ya Pope yapo kwenye Ukatoliki! Wewe unajiita Jesuit ambayo na yenyewe ni mambo yaliyo kwenye Ukatoliki! Kwa maana nyingine, ni sawa na kusema wewe binafsi na Wakatolik mnaamini Pope Bill ambayo ni ya Kikatoliki ilianzisha dini ya Kiislamu ambayo ni ya Kishetani!!

Sasa dhehebu linaloanzisha dini ya kishetani linajitenga vp na ushetan, including wewe mwenyewe unayejiita jina linalotokana na mfumo ulioanzisha dini ya kishetani?!
Mkuu, majini si Mashetani?.
Na si mnasema majini yamesilimu?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
University_Promo

University_Promo

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2018
Messages
563
Points
500
University_Promo

University_Promo

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2018
563 500
Uzi wakijinga kuwahi kutokea.
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
2,570
Points
2,000
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
2,570 2,000
Mkuu, majini si Mashetani?.
Na si mnasema majini yamesilimu?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Quran Sura 72:1-2 inasema:
Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu! Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.
Kwamba, Mtume Muhammad anafundishwa aseme hayo hapo juu! Miongoni mwa makundi ya majini, moja wapo liliisikia Quran ikisomwa na kushuhudia jinsi inavyoongoza kwa uongofu, na kwahiyo wakaiamini!

Sura hiyo inaendelea: 72:4-6
Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
Kwamba, miongoni mwa hao majini palikuwapo na wale waliokuwa wanasema uongo uliopindukia kuhusu Mwenyezi Mungu! Na kwamba, palikuwapo hadi binadamu waliokuwa wakitafuta kujikinga kwa majini (hili hadi kesho lipo; rejea mafundisho ya Sheikh Yahya na uwezo wa majini kuwakinga watu)!

Kwa kuangalia maswali yako, nahitimisha kwa 72;11-14
Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali. Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia. Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki.
Turudi kwenye masuali yako!

Majini si Mashetani?! Sijui imani zingine zinatafsiri shetani ana sifa zipi lakini nadhani wengi wetu nadhani tunakubaliana kwamba Shetani ni yule ambae alimuasi Mwenyezi Mungu! Kutokana na kuasi kwake huko, amekuwa akifanya matendoi ya kumchukiza Mwenyezi Mungu!

Sasa basi, ukisoma vipengele hivyo vya Quran kwa makini utagundua Majini hawana tofauti na wanadamu! Mwanzo kabisa, Quran inaanza kwa kusema kundi moja la majini lilisikiliza Quran ikisomwa na wakaiamini. Kutamka "kundi moja", ina maana palikuwa na kundi zaidi ya moja!!

Na hata ukiangalia hiyo Aya ya 4, inasema "miongoni mwetu"! Kutumia neno "miongoni mwetu" ina maana wao (waliokuwa wameisikia Quran na kuiamini) ni sehemu tu ya majini wote.

Hii maana yake ni nini?! Sio majini wote ni shetani kwa sababu, according to Quran, miongoni mwao waliisikia Quran na wakaiamini! And according to Islam, aliyeiamini Quran hawezi kuwa shetani! Na Aya ay 14 inasema "Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki." Aya hiyo inajibu swali lako kwamba "si mnasema majini yamesilimu?" Kwa mujibu wa hiyo Aya, wapo waliosilimu na according to Islam, wapo ambao hadi leo hawajasilimu!

NOTE: Majini WOTE wanaowaingia wanadamu ni waovu!! Watakuwa ama ni wale ambao hawajamwamini Mwenyezi Mungu au wamemuamini lakini wakakengeuka!! Ukikutana na Sheikh akasema "huyu jini wako ni mzuri" basi fahamu huyo Sheikh nae ni miongoni mwa wale waliokengeuka!! Ukikutana na Sheikh akasema sijui jini anataka mbuzi, mara anataka shuka jeupe na bata, basi huyo Sheikh nae ni kizazi cha hao hao majini waliokengeuka!
 
2013

2013

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Messages
9,804
Points
2,000
2013

2013

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2013
9,804 2,000
Turudi kwenye masuali yako!

Majini si Mashetani?! Sijui imani zingine zinatafsiri shetani ana sifa zipi lakini nadhani wengi wetu nadhani tunakubaliana kwamba Shetani ni yule ambae alimuasi Mwenyezi Mungu! Kutokana na kuasi kwake huko, amekuwa akifanya matendoi ya kumchukiza Mwenyezi Mungu!
Kwa mujibu wa Imani ya Ukristo. Jehanam imewekwa mahsusi kwa ajili ya Shetani na Malaika zake. Na sio kwaajili ya Wanadamu. Hukumu ya kiyama itakua ni ya wanadamu. Tayari Yesu ameshampangia Shetani hukumu yake ambayo ni ziwa liwakalo moto na kiberiti. Na Yesu alimshinda Shetani.

Sasa basi, ukisoma vipengele hivyo vya Quran kwa makini utagundua Majini hawana tofauti na wanadamu! Mwanzo kabisa, Quran inaanza kwa kusema kundi moja la majini lilisikiliza Quran ikisomwa na wakaiamini. Kutamka "kundi moja", ina maana palikuwa na kundi zaidi ya moja!!

Na hata ukiangalia hiyo Aya ya 4, inasema "miongoni mwetu"! Kutumia neno "miongoni mwetu" ina maana wao (waliokuwa wameisikia Quran na kuiamini) ni sehemu tu ya majini wote.

Hii maana yake ni nini?! Sio majini wote ni shetani kwa sababu, according to Quran, miongoni mwao waliisikia Quran na wakaiamini! And according to Islam, aliyeiamini Quran hawezi kuwa shetani! Na Aya ay 14 inasema "Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki." Aya hiyo inajibu swali lako kwamba "si mnasema majini yamesilimu?" Kwa mujibu wa hiyo Aya, wapo waliosilimu na according to Islam, wapo ambao hadi leo hawajasilimu!
Nina maswali hapa?.

1. Kilitokea kitu gani hapo kabla kikundi hicho cha mashetwaini wakawa hawamuamini Allah mpaka ikaja Qur'an?.

2. Na kwanini Mohammad alikua kisumbuliwa na Mashetani?

Na akakiri kua anayo mashetani ndani yake hii unaizungumziaje?
Na akasema hakuna Muislamu asiye na mashetani?

Please No Offence.!!
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
2,570
Points
2,000
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
2,570 2,000
Nina maswali hapa?.

1. Kilitokea kitu gani hapo kabla kikundi hicho cha mashetwaini wakawa hawamuamini Allah mpaka ikaja Qur'an?.
Kwanza tuwekane sawa, ni majini na sio mashetani, ingawaje kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha hawa viumbe, kwa sababu miongoni mwa majini pia wapo wenye sifa za ushetani kama tulivyo binadamu tu! Nachelea

Na kama nilivyosema hapo awali, kwa mujibu wa Uislamu, kuna kushabihiana fulani kati ya majini na wanadamu; kwamba wote hawa wana utashi!

Sasa kama ilivyo kwa wanadamu kwamba kabla ya ujio wa Quran walikuwa na imani zao ikiwa ni pamoja na imani za kipagani; na majini ndivyo hivyo hivyo! Na baada ya kushuka kwa Quran, kama ambavyo ilivyo kwa wanadamu kwamba wapo walioipokea Quran na kuiamini; na majini nao ndiyo hivyo hivyo! Kwenye hizo aya hapo juu zimeeleza wazi kwamba, kuna kundi liliisikia Quran na kuiamini, na wengine hawakuiamini kama ilivyo kwa wanadamu!

Sasa wale ambao hawakuipokea Quran na kuiamini, na pia hata wale ambao waliipokea na kuamini lakini wakakengeuka kama ilivyo kwa wanadamu, ndio hao kwenye Uislamu inaamini ni majini waliotoka kwenye ulimwengu wa kijini na kuja kwenye ulimwengu wa wanadamu na kuwaingia kwa namna mbalimbali kama vile majini mahaba n.k! Ndo hawa, ukienda kwa waganga na hata kwa baadhi ya masheikh, watakuambia jini anataka damu kwahiyo achinjiwe mbuzi!

Kwa mujibu wa Uislamu, yote hayo ni batili!
2. Na kwanini Mohammad alikua kisumbuliwa na Mashetani?

Na akakiri kua anayo mashetani ndani yake hii unaizungumziaje?
Na akasema hakuna Muislamu asiye na mashetani
Ni maneno ya watu tu hayo na wala hayana ukweli wowote! Chanzo cha uzushi huo ni asili ya utume wa Muhammd mwenyewe! Hadi anafikia umri wa miaka 40, tunaweza kusema Muhammad bado alikuwa ni mtu wa kawaida tu hadi umri huo! REMEMBER, hadi anapata utume, Muhammad alikuwa hajui kusoma wala kuandika!!

Na wakati huo jamii ya Waarabuilikuwa very corrupted kwa mambo ya kipagani na kishirikina! Aidha, ilikuwa ni jamii ambayo kwa mfano, Mtoto wa Bakhresa akiua mtu kapuku kama mimi, basi katika "kutenda haki", Mzee Bakhresa angeweza kumtoa housegirl ili auwawe kama malipo ya kisasi badala ya kumtoa mwanae aliyefanya kosa husika!!!!

Sasa kutokana na hilo, Muhammad akawa amejenga tabia ya kujitenga na wenzake na wakati mwingine akawa anaenda pangoni kufanya ibada na meditation na kujiweka mbali na yale yanayofanywa na jamii yake!

Sasa siku moja akiwa pangoni, Muhammad akatokewa na Malaika Jibril na kumwambia Muhammad "SOMA" Muhammad akajibu Siwezi kusoma! Kwa mujibu wa Imam Ahmad, kusikia vile Malaika akambana Mtume Muhammad hadi Muhammad akahisi kama anataka kuishiwa na pumzi, kisha akamwachia na kumwambia tena SOMA, na hapo ukawa ndio mwanzo wa Sura ya kwanza kabisa kushushiwa Muhammad ambayo alianza kukaririshwa na Malaika! Hii ni Sura ya 96 inayosema:

1. Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba.
3. Alimwumba mwanadamu kwa tone la damu iliyoganda.
4. Soma! na Mola wako ni Mbora kuliko wote.....

Baada ya Muhammad kukaririshwa hizo aya, Malaika akasepa zake! Baada ya kuachwa huru, ikabidi Muhamadi atoke nduki kurudi nyumbani huku akihema kweli kweli!

Sasa baada ya hilo tukio, hakuwa tena Muhammad yule aliyezoeleka hapo kabla! Akaanza kuhubiri Quran na imani kwa Mungu Mmoja badala ya miungu iliyokuwa inaabudiwa na Waarabu wengi!

Kutokana na hilo, ndipo watu wakaanza kuvumisha kwamba Muhammad kapandwa na mashetani! And it's understandable kwa sababu Muhammad wanayemjua fika kwamba hakusoma, from nowhere wanaanza kumuona akihubiri na kusoma! Kwanini wasivumishe kwamba kapandwa na mashetani hasa ukizangatia walikuwa wanatafuta kila namna ya kum-discredit kwa sababu, hawakutaka kusikia lolote kuhusu hayo mahubiri yake!

Suala hilo limetajwa hadi kwenye Quran Sura ya 81, kuanzia aya ya 19 kwamba:-

19. Kwa hakika hii ni kauli ya Mtume mtukufu,
20. Mwenye nguvu, mwenye cheo cha heshima Mwenye enzi,
21. Anayetiiwa kisha mwaminifu
22. Na mwezenu si mwenda wazimu.
23. Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
25. Wala yeye si bahili kueleza mambo ya ghaibu.
26. Wala hii si kauli ya Shetani afukuzwaye.

Hiyo ni kauli ya Muhammad ambayo imekaririwa kwenye Quran akiwaambia wale waliokuwa wanasema amepandwa na mashetani! Muhammad anasema "mimi sio mwenda wazimu bali nimemuona Malaika kwa macho yangu, na hii wala sio kauli ya shetani!"
 
smaki

smaki

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2019
Messages
680
Points
500
smaki

smaki

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2019
680 500
Hizi conspiracies za kitoto na zinawaandama wavivu wa kufikiri. Tumeshazielezea sana humu na kutoa fafanuzi mbalimbali lakini, kila amezeshwae sumu huja tena na thread akidhani ni habari mpya.
Acha udwanzi wa kizee huo kwani ulipoona wewe ni wote tumeona? watu wengine mko ivoivo tu, wengine wakipata unaumia nini kwani. si upite tuu.

Uliposoma sisi tulikuwa ulaya na jamii forum ya huko, tulisoma ya huko.

Mlleta uzi akhsante sana na ubarikiwe. niliyajua haya ila umeniongezea sana nyama, nimeshiba kwa kweli usikate tamaa na mtu km huyu.
 
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Messages
493
Points
250
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2018
493 250

Good Mr
 
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Messages
493
Points
250
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2018
493 250
Kwanza tuwekane sawa, ni majini na sio mashetani, ingawaje kuna mstari mwembamba sana unaotofautisha hawa viumbe, kwa sababu miongoni mwa majini pia wapo wenye sifa za ushetani kama tulivyo binadamu tu! Nachelea

Na kama nilivyosema hapo awali, kwa mujibu wa Uislamu, kuna kushabihiana fulani kati ya majini na wanadamu; kwamba wote hawa wana utashi!

Sasa kama ilivyo kwa wanadamu kwamba kabla ya ujio wa Quran walikuwa na imani zao ikiwa ni pamoja na imani za kipagani; na majini ndivyo hivyo hivyo! Na baada ya kushuka kwa Quran, kama ambavyo ilivyo kwa wanadamu kwamba wapo walioipokea Quran na kuiamini; na majini nao ndiyo hivyo hivyo! Kwenye hizo aya hapo juu zimeeleza wazi kwamba, kuna kundi liliisikia Quran na kuiamini, na wengine hawakuiamini kama ilivyo kwa wanadamu!

Sasa wale ambao hawakuipokea Quran na kuiamini, na pia hata wale ambao waliipokea na kuamini lakini wakakengeuka kama ilivyo kwa wanadamu, ndio hao kwenye Uislamu inaamini ni majini waliotoka kwenye ulimwengu wa kijini na kuja kwenye ulimwengu wa wanadamu na kuwaingia kwa namna mbalimbali kama vile majini mahaba n.k! Ndo hawa, ukienda kwa waganga na hata kwa baadhi ya masheikh, watakuambia jini anataka damu kwahiyo achinjiwe mbuzi!

Kwa mujibu wa Uislamu, yote hayo ni batili!
Ni maneno ya watu tu hayo na wala hayana ukweli wowote! Chanzo cha uzushi huo ni asili ya utume wa Muhammd mwenyewe! Hadi anafikia umri wa miaka 40, tunaweza kusema Muhammad bado alikuwa ni mtu wa kawaida tu hadi umri huo! REMEMBER, hadi anapata utume, Muhammad alikuwa hajui kusoma wala kuandika!!

Na wakati huo jamii ya Waarabuilikuwa very corrupted kwa mambo ya kipagani na kishirikina! Aidha, ilikuwa ni jamii ambayo kwa mfano, Mtoto wa Bakhresa akiua mtu kapuku kama mimi, basi katika "kutenda haki", Mzee Bakhresa angeweza kumtoa housegirl ili auwawe kama malipo ya kisasi badala ya kumtoa mwanae aliyefanya kosa husika!!!!

Sasa kutokana na hilo, Muhammad akawa amejenga tabia ya kujitenga na wenzake na wakati mwingine akawa anaenda pangoni kufanya ibada na meditation na kujiweka mbali na yale yanayofanywa na jamii yake!

Sasa siku moja akiwa pangoni, Muhammad akatokewa na Malaika Jibril na kumwambia Muhammad "SOMA" Muhammad akajibu Siwezi kusoma! Kwa mujibu wa Imam Ahmad, kusikia vile Malaika akambana Mtume Muhammad hadi Muhammad akahisi kama anataka kuishiwa na pumzi, kisha akamwachia na kumwambia tena SOMA, na hapo ukawa ndio mwanzo wa Sura ya kwanza kabisa kushushiwa Muhammad ambayo alianza kukaririshwa na Malaika! Hii ni Sura ya 96 inayosema:

1. Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba.
3. Alimwumba mwanadamu kwa tone la damu iliyoganda.
4. Soma! na Mola wako ni Mbora kuliko wote.....

Baada ya Muhammad kukaririshwa hizo aya, Malaika akasepa zake! Baada ya kuachwa huru, ikabidi Muhamadi atoke nduki kurudi nyumbani huku akihema kweli kweli!

Sasa baada ya hilo tukio, hakuwa tena Muhammad yule aliyezoeleka hapo kabla! Akaanza kuhubiri Quran na imani kwa Mungu Mmoja badala ya miungu iliyokuwa inaabudiwa na Waarabu wengi!

Kutokana na hilo, ndipo watu wakaanza kuvumisha kwamba Muhammad kapandwa na mashetani! And it's understandable kwa sababu Muhammad wanayemjua fika kwamba hakusoma, from nowhere wanaanza kumuona akihubiri na kusoma! Kwanini wasivumishe kwamba kapandwa na mashetani hasa ukizangatia walikuwa wanatafuta kila namna ya kum-discredit kwa sababu, hawakutaka kusikia lolote kuhusu hayo mahubiri yake!

Suala hilo limetajwa hadi kwenye Quran Sura ya 81, kuanzia aya ya 19 kwamba:-

19. Kwa hakika hii ni kauli ya Mtume mtukufu,
20. Mwenye nguvu, mwenye cheo cha heshima Mwenye enzi,
21. Anayetiiwa kisha mwaminifu
22. Na mwezenu si mwenda wazimu.
23. Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
25. Wala yeye si bahili kueleza mambo ya ghaibu.
26. Wala hii si kauli ya Shetani afukuzwaye.

Hiyo ni kauli ya Muhammad ambayo imekaririwa kwenye Quran akiwaambia wale waliokuwa wanasema amepandwa na mashetani! Muhammad anasema "mimi sio mwenda wazimu bali nimemuona Malaika kwa macho yangu, na hii wala sio kauli ya shetani!"
Js
 
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
1,138
Points
2,000
Loeb S Mpalasinge

Loeb S Mpalasinge

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
1,138 2,000
Mkuu myplusbee unaelewaje kipengele hiki cha 72:11-14????

""Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia.""

Je neno hili halionyeshi kulikuwa na wakati ulipita uliokuwa na historia ya hawa viumbe??

Hatuwezi ikiwakilisha jaribio lililopita na Hatutomshinda ikiwakilisha ukweli waliokuja kuugundua Baadae.
 
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2016
Messages
2,570
Points
2,000
M

myplusbee

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2016
2,570 2,000
Mkuu myplusbee unaelewaje kipengele hiki cha 72:11-14????

""Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia.""

Je neno hili halionyeshi kulikuwa na wakati ulipita uliokuwa na historia ya hawa viumbe??

Hatuwezi ikiwakilisha jaribio lililopita na Hatutomshinda ikiwakilisha ukweli waliokuja kuugundua Baadae.
Sio kwa mujibu wa Quran! Kwa mujibu wa Quran, majini ni miongoni tu mwa viumbe wa Mwenyeji Mungu vilivyoumbwa nae huku wakiwa wamefanana na binadamu kwenye suala la utashi! Lakini kwa kukengeuka tu, wakawa wanafanya yale yanayomchukiza Mwenyezi Mungu hadi pale miongoni mwao siku moja waliposikia Quran na kutoa hiyo kauli kwamba "Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia." Kauli hiyo inaonesha kwamba, pamoja na uovu waliokuwa wanafanya lakini walifahamu uwepo wa Mungu na nini wajibu wao mbele ya Mwenyezi Mungu! Ni kama ambavyo leo hii wanadamu tunavyofanya uovu usiomithirika wakati tunafahamu tufanyayo ni machukizo kwa Mwenyezi Mungu! Na pia tunafahamu katu hatuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, sema ndo vile tumekuwa Watumwa wa Shetani kuliko kuwa watumishi wa Mwenyezi Mungu!

Sasa katikati ya uovu wetu huu, watokee wengine miongoni mwetu watubie kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo! Waamue kuacha yale yote yaliyo machukizo kisha ndipo wanakuja kusema "Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani,wala hatuwezi kumponyoka kwa kumkimbia." Kwamba, twafanya uovu wote huu sio kwamba hatujui uwepo wa Mwenyezi Mungu na yale yamchukizayo; au si kwamba wakati uliopita palikuwa na historia inayotuhusu watu kama sisi, bali ni vile tu tumeshukiwa na maono na kuamua kwa dhati kurejea kwa Mwenyezi Mungu!
 
Forum statistics

Threads 1,315,053
Members 505,131
Posts 31,846,577
Top