VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

Nyongeza ni sahihi ila Wadau wangepewa notisi ya mwaka moja kwani wageni wengi hufanya booking na kulipa fedha mapema. Waziri aingilie kati hii nyongeza ya Ngorongoro Conservation Area Authority.

Tatizo wazir anapewa sector ya utalii wakat hajui utalii. .
 
No clear regulations on how to apply VAT

Regulations have to be provided....Example, package contains Lodge also, so if you apply 18% VAT generally on Package, it means you have charged VAT 18 Twice on Lodge..

Cars uses fuel, fuel also paid VAT

Actually it is Tax on Tax
 
Katika taarifa ya habari ya star TV, prof. Maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti).

-----------------------

Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!?

KAMA WAZIRI HATAKI WATALII MASKINI (BUDGET) NI HATARI:
Awali ya yote nielezee aina ya watalii wanaokuja Tanzania, nchi yetu inapata/pokea watalii aina nne:
1. Kuna watalii wa bajeti (budget), 2. Watalii wa Kati (mid class), 3.Watalii wa Juu (high class) & Watalii wa juu zaidi (High end).
Kimsingi Watalii wa bajeti na wakati ndo wengi wanaweza kuwa 75% - 80% na wanaobaki ndo watalii wa juu na juu zaidi, na ukitaka kulijua hili ni utafiti mdogo sana (hahitaji kuwa na digrii); kwa watalii wa bajeti na mid class angalia low (budjet) class na mid class accommodations ziko ngapi; utakuta ziko nyingi sana na angalia camp site za basic camping ziko ngapi; utaona ziko nyingi na
Katika taarifa ya habari ya star TV, prof. Maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti).

-----------------------

Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!?

KAMA WAZIRI HATAKI WATALII MASKINI (BUDGET) NI HATARI KWA TAIFA NA WATU WAKE.

Awali ya yote nielezee aina ya watalii wanaokuja Tanzania, nchi yetu inapata au kupokea watalii aina nne:

1. Kuna watalii wa bajeti (budget), 2. Watalii wa Kati (mid class), 3.Watalii wa Juu (high class) na Watalii wa juu zaidi (High end).

Watalii wa bajeti na wakati ndo wengi ni kati ya 70% - 80% na wanaobaki ni watalii wa juu na juu zaidi, na ukitaka kulijua hili ni utafiti mdogo sana (hahitaji kuwa na digrii); kwa watalii wa low class na mid class; angalia low (budjet) class na mid class accommodations ziko ngapi; utakuta ziko nyingi sana na angalia camp site za basic camping ziko ngapi; utaona ziko nyingi, sasa tugeukie high class & high end accommodations; utakuta ni chache sana! Kama waziri anasema anahitaji watalii matajiri yaani high end ni kwamba hataki visa, park fee, camping fee ya watalii wa low class, mid class ama high class, kwa msingi huu serikali itakusanya tu visa, park fee na camp fee za watalii matajiri sana (high end). Nashindwa kuelewa kwanini Waziri hataki watalii ambao si matajiri ili hali visa, park fee na camping fee inalipwa sawa kwa Makundi yote yaani watalii wote wanalipa visa na park fee inayolingana, haimanishi akiwa top end analipa visa au park fee zaidi! Mimi ningemuelewa waziri kama angesema watalii matajiri (high end) walipe visa na park fee kubwa zaidi ya wengine.

KUPANDA KWA TOZO NGORONGORO: Mimi sina ubishi sana na ongezeko husika hususan entry fee lakini sikuona umuhimu wa kuongeza carter service fee. Sasa tatizo yangu kubwa ni taarifa ya muda mfupi mno! Haingii akilini taarifa ya tozo mpya inatolewa tarehe 25 Juni na inatakiwa ianze kutumika julai mosi, ni siku sita tu zimebaki tozo mpya ianze kutozwa! Hili linasikitisha sana; kwanini iwe gafla hivyo? Kwanini basi taarifa haikutolewa angalau miezi 2 au 3 nyuma? ikumbukwe kwamba mtalii anapopanga safari anakuwa ameshapanga bajeti sasa unavyomuongezea gharama analalamika na anakosa furaha na hamasa ya holiday yake yamkini anaanza kupata stress! Haiwezekani mwenye nyumba akampandishia mpangaji kodi ya mwezi ujao wakati imebaki siku sita, kwa kawaida na kistaarabu anatakiwa ampe mpangaji taarifa mapema si chini ya mwezi ili mpangaji ajiandae na ajipange. Kila kitu kina utaratibu na mipango hata Mungu wetu ni wa utaratibu na mpango, hivyo hili swala la ongezeko la tozo ngorongoro ni vyema likawekewa utaratibu mzuri.

TOZO YA ONGEZEKO LA DHAMANI KWENYE UTALII (VATA 18%): Mimi nafikiri viongozi wetu hawajafanya utafiti mzuri au wakutosha na hili linatokana na kutoshirikisha wadau na kama wadau wanashirikishwa basi nikwamba yale wanayoshauri yanapuuzwa na yanadharauliwa. Kimsingi Tanzania imekuwa eneo ambalo ni ghali sana kusafiri au kuja kutalii ukilinganisha na nchi zingine nyingi za Africa hususan nchi za Africa Mashariki; na baaadhi ya maeneo ambayo yanafanya utalii kuwa juu ni flight tickets (Local & international flight fare), accommodations, park fee, camping fee n.k.

Hii hapa chini ni Kauli ya Waziri wa fedha:

Akizungumzia VAT katika utalii, Dk Mpango alisema kodi hiyo haihusiani na ongezeko au kupungua kwa watalii nchini kwa kuwa watalii hao hawatazami kodi hiyo kama kigezo kikuu cha kwenda kuangalia vivutio vya utalii.

Alitoa mfano wa idadi ya watalii waliotembelea mbuga za wanyama kwa kipindi 2011 hadi 2014 katika nchi za Tanzania, Kenya na Afrika Kusini, ambayo inaonesha Tanzania licha ya kwamba haikuwa ikitoza VAT, bado ilitembelewa na watalii wachache kuliko nchi hizo ambazo zilikuwa zikitoza kodi.

Kama waziri anatuambia na anakiri kwamba Tanzania ilitembelewa na watalii wachache ukilinganisha na nchi ambazo zina VAT basi ni vizuri akatuambia ni sababu zipi zilifanya Tanzania ipate watalii wachache ili hali haina tozo ya ongezeko la dhamani na atuambie ni kitu gani sasa kitafanya mwaka huu (2016/2017) watalii waongezeke baada ya gharama kupanda kwa ongezeko la VAT. Pia atuambie ni kwanini hizo nchi zenye VAT zilipata na zinaendelea kupata watalii wengi kuliko nchi hii. Tanzania inapata watalii wachache si kwasababu haina VAT bali ni kwasababu gharama ziko juu na hili linazungumzwa na watalii wenyewe.

Hivyo kama kweli serikali inataka watalii waongezeke basi haina budi kupunguza tozo na kodi lukuki ambazo mwisho wa siku ana beba mtalii. Lakini endapo serikali itaendelea kulazimisha VAT basi itapata majawabu muda si mrefu. Nchi ambazo waziri ametolea mfano kuwa zina VAT kwenye utalii na na bado zinapata watalii wengi ni sawa kabisa LAKINI ni ukweli kwamba pamoja na hizo nchi kuweka VAT bado gharama (safari package) ziko chini ukilinganisha na Tanzania, na mfano mzuri ni nchi ya Kenya; kwa mfano; safari ya siku saba mbuga za Kenya iko chini kwa 10 -15% ukilinganisha na Tanzania. Na ijulikane kuwa wanyama na vivutio ambavyo viko kwetu na jirani zetu wanavyo pia na wanafanya jitiada kila kukicha ili wapate watalii wengi zaidi na ndo maana wenzetu wameondoa VAT kwenye utalii.

Leo niliwasiliana na mkenya mmoja kumwabarisha ongezeko la tozo ngorongoro na VAT kwenye utalii; jamaa alifurahi sana akasema sasa biashara ya utalii Kenya itakuwa nzuri kwani watalii waliyokuwa waje Tanzania watageukia Kenya! Na huu ndo ukweli wenyewe, sasa kama VAT itaendelea kuwepo kwenye Utalii basi Tanzania itaambulia tu wale wageni anaohitaji waziri wa utalii (Mh. Magembe) ambao ni matajiri (top end) na sioni wakizidi 15% ya watalii wote Tanzania.

Kwa mfano kama Tanzania inapata watalii 2,000,000 kwa mwaka basi itapata watalii 15% ambayo ni watalii 300,000 tu, kwa msingi huu kampuni za kitalii zaidi ya 50% zinazotegemea wageni ambao si matajiri zitakosa wageni hivyo zitakufa na zikifa serikali itakosa mapato makubwa (mfano mdogo tu ni leseni ya utalii ambao ni US$2000 kwa kila kampuni kwa mwaka), watu wengi watakosa ajira, wafanya biashara wengi watakosa biashara na wateja (mfano wauza mafuta ya magari, wauza spea, wauza vitu sokoni, wauza vifaa vya ujenzi na vitu madukani, wenye migahawa, wenye bar na wauza vinywaji vyote n.k) hoteli nyingi zinazotegemea watalii ambao si matajiri zitakosa wageni, Serikali itakosa mapato ya visa na park fee!! Kimsingi hili litaleta madhara makubwa na kwa wengi. Baada ya wageni /watalii wengi kusikia kutakuwapo na ongezeko la VAT wameanza ku- cancel safari!

NINAOMBA SANA SERIKALI KW AUJUMLA WAKE NI PAMOJA NA WAZIRI MWENYE DHAMANA, WAZIRI WA FEDHA, WAZIRI MKUU NA MH. RAISI; WAANGALIE TENA VIZURI HILI SWALA LA VAT KWENYE BIASHARA YA UTALII.
 
Bei ya sukari ilikuwa 2000 kawaida, wakaja na matamko ya kukataza sukari na bei elekezi

Ikawa Tabu nchi nzima....Sasa sukari bei ni ngumu, inaumiza wananchi ---2500

Sasa wamekuja na VAT on Tourism, another grave mistake
 
Waziri aongee na wadau wa utalii, bila research you speak wrong

Minister, please speak to tourism stakeholders like TTB, TANAPA, Travel agents, Hotels na Tour Operators.

Watalii walikuwa wachache kwa Sababu ya poor marketing of Tanzania destinations

Pia watalii walikuwa wachache kwa sababu ya bei kubwa ya ndege to fly to Tanzania, caused by Expensive landing fee na high jet fuel.

Flight from Europe to Nairobi or JOburg is much cheaper than to Dar esalaam

Ndo maana watalii wanapitia Kenya

"Alitoa mfano wa idadi ya watalii waliotembelea mbuga za wanyama kwa kipindi 2011 hadi 2014 katika nchi za Tanzania, Kenya na Afrika Kusini, ambayo inaonesha Tanzania licha ya kwamba haikuwa ikitoza VAT, bado ilitembelewa na watalii wachache kuliko nchi hizo ambazo zilikuwa zikitoza kodi" Waziri akutanishe wadau/tourism stakeholders kama TTB, TANAPA< Tour Operators na Travel Agents

Kauli za Kisiasa za jumla jumla zitaua utalii....Economy will drop

Soko la mboga mboga na matunda

Ajira zitapungua

Government will loose revenue

Pesa ya kigeni itakuwa adimu

Thamani ya shillingi itadondoka
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, kuna watalii wengi sana choka mbaya wanakuja wanakaa beach wanaunua maji ya Kilimanjaro wanakula chips mayai na kuondoka lkn wanaingia kwenye takwimu hao hatutaki hao kwanza wanachafua na kuharibu mazingira yetu, tuwekeze kwa Watalii middle class na wenye fedha siyo watalii beach boy!

Hii ndiyo Serikali niliyokuwa naishubiria maisha yangu yote!​
hahahahah mwenyewe si ajabu hata kwenda kwenye hizo mbuga hujawai sembuse kuwa mtalii nchi nyingine na kwenda kununua maji huwezi hahahaha kweli maskini jeuri hufa na tai shingon .Subirini hao kina billgate.
 
Waziri aongee na wadau wa utalii, bila research you speak wrong

Minister, please speak to tourism stakeholders like TTB, TANAPA, Travel agents, Hotels na Tour Operators.

Watalii walikuwa wachache kwa Sababu ya poor marketing of Tanzania destinations

Pia watalii walikuwa wachache kwa sababu ya bei kubwa ya ndege to fly to Tanzania, caused by Expensive landing fee na high jet fuel.

Flight from Europe to Nairobi or JOburg is much cheaper than to Dar esalaam

Ndo maana watalii wanapitia Kenya

"Alitoa mfano wa idadi ya watalii waliotembelea mbuga za wanyama kwa kipindi 2011 hadi 2014 katika nchi za Tanzania, Kenya na Afrika Kusini, ambayo inaonesha Tanzania licha ya kwamba haikuwa ikitoza VAT, bado ilitembelewa na watalii wachache kuliko nchi hizo ambazo zilikuwa zikitoza kodi" Waziri akutanishe wadau/tourism stakeholders kama TTB, TANAPA< Tour Operators na Travel Agents

Kauli za Kisiasa za jumla jumla zitaua utalii....Economy will drop

Soko la mboga mboga na matunda

Ajira zitapungua

Government will loose revenue

Pesa ya kigeni itakuwa adimu

Thamani ya shillingi itadondoka
sitaki kuamini kama waziri tena prof.hawezi kujua vitu kama ivi kweli dah so sad.Sifa ni mbaya mno.
 
Umelewa uccm. Najua haya uliyoyaandika si dhamira yako halisi, bali utumwa wa tumbo lako tu. Huyo mtalii unayemuita "beach boy" analala bure au anakula bure? Kama siyo, je haingizi kipato kwa watanzania kupitia huduma anazopata? na serikali haipati kodi yake? Watu kama wewe ndio wanarudisha taifa hili nyuma.
Kabisa kalewa achana nae anaweza akawa mmoja wawalio fukuzwa kule st.Joseph mana si kwa kutema pumba hizo.
No research no right to speak.
 
Kila serikali ina sera zake. Tanzania iliamua karibu miaka 10 sasa kama siyo zaidi kuachana na bag pack tourists na wanalipa ada ya visa. Pia Hoja tukakataa kuingia kwenye mkumbo was visa ya pamoja Afrika Mashariki. Kitakwimu Tanzania imekuwa inapokea watalii wachache ikilinganishwa na Kenya lakini mapato yanalingana kama hatuazidi. Ili hoja iwe na mashiko bora kuweka takwimu za mapato yanayopatikana badala ya kumkebehi Prof Maghembe. Tujaribu kulitendea haki jukwaa hili
Ndugu hatupaswi kuwa karibu na kenya au kuwazidi kidogo tunatakiwa kuwaacha mbali sana ukilinganisha na namba ya watalii na income inayopatikana .Kama tunasema tunaongoza kwa vivutio duniani why watalii wachache wakati tuna vivutio vya kutosha?Tuacheni masihari hii sekta ingetendewa haki ingesaidia sana .Lakini ni sawa na mwenye nyumba kuongeza kodi ya nyumba bila maborsho yeyote just tu kaamua sababu nyumba yake.
 
Nimefika Mikumi, Bonde la Ngorongoro, kwingine bado!
Hahahaha na kukaa kote Tanzania mbuga mbili ungekua unatakiwa kusafiri si ndo ungeishia kuzisikia darasani tu mana kuwa beach boy kwa watu huwezi sembuse huyu anayekuja na kuspendi $ 500
 
Sijui ni kwa nn lazima tupingekila kitu !

Pamoja na vat : naamini still mtalii anekwenda Kenya atalipa zaidi kama unakumbuka exchange rate ya ksh na tsh !
mkuu tuacheni ushabiki si kupinga tunatakiwa kwanza tuwe na strategies za kuwavutia zaidi bf ya kuimpose tax zaidi before hatujafanya maboresho yoyote.Kuna thread moja humu nimesoma jana kuwa watalii waliofanya deposit tayari wanataka wawe refunded na safari zao wanataka ziwe canceled due to kile walichoambiwa kuhusu Tax mana inaonekana kuna mkanganyiko kwenye kila sekta inayohusu utalii tafuta uisome.Mimi sibishi maana hainisaidii waje wasije hainisumbui maana tushazoea maisha yetu .
 
'professor' inatokana na neno 'prophecy' ambalo nalo ni kielelezo cha Prophet.
Prophet maana yake ni Nabii kwa maana kwamba anajua past, present na future ya anayoongea, hivyo hivyo professor inabidi pia ajue 'past, present na future' kwenye field au professional anayosimamia.
Huyu ndiye Professor Magembe sijui professional yake ni kitu gani!!!!!!
 
ukiomba visa ya kwenda US lazima uonyeshe uwezo wako wa kifedha ikiwemo kuonyesha bank statement huko si kuchuja masikini?
pye we nawe sasa utafananisha wazamiaji na wataalii?wao hawana shida na hela zako bali nyie ndo mna shida na hela zao .na hawataki bugdha ya wakimbizi au waganga njaa.
 
Tuache hizi "fear mongering!"; dunia ni tofauti hatuwezi kuwa na mbinu zinazofanana. Kenya wameondoa VAT sababu ya kujaribu kuondoa tatizo la kushuka kwa utalii sababu ya "fear of terrorism". Watanzania wanataka tufuate Kenya wanachofanya!!! Nadhani huu upinzani dhidi ya VAT hautokani na watanzania hasa, unatokana na wafanyabiashara ya utalii.

Hakuna aliyekuja na "facts and figures" za kuonesha VAT itashusha watalii Tanzania kwa kiasi gani!! Mapato ya serikali yatakayoongezeka ni kiasi gani na yatakuwa na impact gani overall kwenye uchumi. Let's face it - tunataka maendeleo. Tunataka serikali ifanye kila kitu - ijenge bara bara, iweke umeme wa uhakika, iweke mfumo bora wa maji, n.k. lakini bado tunafikiria kutoa "tax incentives". Mapato ya serikali yatatokana na nini? Watu wameng'ang'ania tax zaidi kwenye Mining wakati hawajui chochote kuhusu Mining operations. Mining hata kama serikali ikichukua 50% ya mapato ya madini bado contribution yake kwenye uchumi itakuwa ndogo - halafu ikifanya hivyo hiyo migodi nani ataiendesha? Kodi ni lazima ikusanywe kwenye kila industry ili isiwaelemee watu wachache tu. Hiyo ndo logic. Utalii sasa hivi unaongoza kwa kuleta fedha za Kigeni, kwa nini kusiwe na kodi huko??

Serikali huendeshwa na kufanya mambo yake kwa kutumia kodi. Ikiwa tunataka hatimaye mzigo wa kodi usielemee kikundi kidogo cha watanzania ni lazima tufikie mahali tuone kuwa kila mtu analazimika kulipa kodi - huo ndo uzalendo. Kama kuna VAT, sioni kwa nini anayenunua gari alipe VAT + import duty + Registration fees, halafu mtalii anayekwenda kula bata Serengeti asilipe VAT. Hii ni twisted thinking - ni mawazo ambayo mwenye nayo inabidi umuonee huruma kwa kweli. Concept ya kutumia kodi kama kivutia cha uwekezaji imeshaonekana ina madhara mengi kwa nchi na wengi tunaiona na kuendelea kuilalamikia kwenye "mining". Ni jambo la kushangaza kuwa wale wale wanaolalamikia misamaha ya kodi kwenye madini ndo hao hao wanaotaka misamaha ya kodi kwenye utalii - double standards? Au watu wanapinga tu kinachofanywa na walioko madarakani ili wakishindwa nao wachaguliwe? ....... Ni ajabu na kweli!!
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, kuna watalii wengi sana choka mbaya wanakuja wanakaa beach wanaunua maji ya Kilimanjaro wanakula chips mayai na kuondoka lkn wanaingia kwenye takwimu hao hatutaki hao kwanza wanachafua na kuharibu mazingira yetu, tuwekeze kwa Watalii middle class na
wenye fedha siyo watalii beach boy!
Pumba tupu


Hii ndiyo Serikali niliyokuwa naishubiria maisha yangu yote!​
 
Huyu maghembe ndio maana machali na mkosamali walikua wanamtukana mjengoni
 
Back
Top Bottom