VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Katika taarifa ya habari ya star TV, prof. Maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti).

-----------------------

Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!?
 
Katika taarifa ya habari ya star TV prof maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti)
Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!??
Siamini kwamba tumefikia level hii. Hivi mtalii anayechangia 500 USD kwenye pato la taifa na anayechangia 10,000 USD hawaitaji kuthaminiwa kila mmoja kwa nafasi yake.

Hivi nchi za wenzetu huwa wanatoa maneno ya kejeli kama haya. Kweli unaweza ukasoma hata degree 200 ila still bado hospitality concept usielewe.
 
Vijinchi vidogo dogo tena maskini vina hulka ya majigambo usiseme. Oh we are greatest nation on earth : barabara mbovu, ajira mashaka, afya mgogoro, ufisadi balaa, makazi duni, utawala hovyo etc etc


Umemaliza, na Mara nyingi watu wafupi ni watata na kijiona ni warefu kama ngongoti
 
Katika taarifa ya habari ya star TV prof maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti)
Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!??


Naunga mkono hoja kwa 100%, kuna watalii wengi sana choka mbaya wanakuja wanakaa beach wanaunua maji ya Kilimanjaro wanakula chips mayai na kuondoka lkn wanaingia kwenye takwimu hao hatutaki hao kwanza wanachafua na kuharibu mazingira yetu, tuwekeze kwa Watalii middle class na wenye fedha siyo watalii beach boy!

Hii ndiyo Serikali niliyokuwa naishubiria maisha yangu yote!
 
Hajui utalii Maghembe wala haangalii statistics.
Angekaa chini na wadau wa utalii wangemwambia ni intineraries zipi zinauza zaidi na kwanini.
Kwanza the whole set up ya biashara ya utalii Tanzania hai incourage luxurious tours na ndio maana tunauza zaidi customer tailored intineraries na group tour.
Kuna nchi ambazo zimejipanga vizuri kuhudumia top income tourists na hatuwezi kuzi outcompete kwa usiku mmoja.
Hii serikali inajiaibisha and in the process inatuaibisha.
 
Back
Top Bottom