VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

Kwanza mleta mada ni muongo, hayo ya umasikini ni maneno yako. Kama u mkweli weka nukuu ya sentensi ya Maghembe.

Halafu, ni masikini yupi duniani anaeweza kumudu kutalii?
Soma comments za kijani mwenzio Barbarosa halafu urudi hapa.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, kuna watalii wengi sana choka mbaya wanakuja wanakaa beach wanaunua maji ya Kilimanjaro wanakula chips mayai na kuondoka lkn wanaingia kwenye takwimu hao hatutaki hao kwanza wanachafua na kuharibu mazingira yetu, tuwekeze kwa Watalii middle class na wenye fedha siyo watalii beach boy!

Hii ndiyo Serikali niliyokuwa naishubiria maisha yangu yote!​
Umeenda mbuga ngapi mpaka sasa? nina wasiwasi ata zoo ujawai fika.
 
Kwanza mleta mada ni muongo, hayo ya umasikini ni maneno yako. Kama u mkweli weka nukuu ya sentensi ya Maghembe.

Halafu, ni masikini yupi duniani anaeweza kumudu kutalii?
Wewe mama usidhani tunamwekea maneno mdomoni huyo Waziri wako wa serikali ya majipu, ni kweli kabisa maneno hayo kayatamka na tumemsikia kwa masikio yetu wenyewe na kumuona kwenye luninga saa 2 usiku huu kupitia Star TV.
 
hivi kati yake na hao wazungu anao waita maskini,nani ana maisha bora?cha kuchekesha huyu huyu katoka kupokea ndege za msaada ya kupatrol mbuga zetu hili kukamata majangiri na hao hao wazungu!
Mkuu kama umeumia kuwaita wazungu masikini nenda kawagawie number zako za Tigo,hata hivyo Ukawa mna ushirika na vyama vinavyo unga mkono ushoga na usagaji ndiyo maana umeumia sana wazungu kuitwa masikini
 
Watashukia uwanja mpya Chato International Airport.
 
Katika taarifa ya habari ya star TV prof maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti)
Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!??

kama ni kweli kasema hivyo,kweli majivuno na kiburi kwa v umeobgezeka kwa kiwango ch phd
 
Mwaka 2020 utasikia Arusha hakuna utali kwa jili ya fujo za Chadema tutakumbushana tu haya ya vat mungu akiniweka hai nitaenda Arusha kufanya kampeni mwaka huo
 
Hatutaki watalii masikini. Wanatuharibia mazingira yetu. Mlima Kilimanjaro upa TZ tu, Ngorongoro ipo TZ tu, Serengeti pia.
Masikini wabaki kwenye nchi zao. Sisi hatutaki Mass tourism.
 
Mkuu kama umeumia kuwaita wazungu masikini nenda kawagawie number zako za Tigo,hata hivyo Ukawa mna ushirika na vyama vinavyo unga mkono ushoga na usagaji ndiyo maana umeumia sana wazungu kuitwa masikini
Unatakiwa upigwe ban ya miezj sita
 
Mwaka 2020 utasikia Arusha hakuna utali kwa jili ya fujo za Chadema tutakumbushana tu haya ya vat mungu akiniweka hai nitaenda Arusha kufanya kampeni mwaka huo
Watalii watapitia Mwanza na Mara kwenda kufanya utalii. Na utalii sio Serenget na ngorongoro pekee. Ndio maana serikali inawekeza sana kwenye kusini.
 
Kwa bei ya entry fees inaangalia mtalii tajiri au maskini wote malipo yao yanafanana.

Halafu hao anaowazungumzia hulipia kila kitu kwenye makumpuni huko nje akika hapa ni kujiachia tu.
 
Kweli kabisa....tunawahitaji watalii wote bila kubagua

Industry inachukua watalii wa aina zote. Kuna watu wameekeza kwa ajili ya high-end, middle class na wengine low-income tourists.

Hao ambao waziri anawatukana wakija wanalala guests na mahostel ya watanzania na si high-end lodges (nyingi zinamilikiwa na wageni). Pia wanasaidia kwa kuwaleta wazee wao huku for tourism (pension money which is high-income).

Watu wanatetea ujinga huku watanzania ndugu zao wakija kuumia kutokana na kauli za kipuuzi.
 
Hatutaki ma beach boy hao kwanza wanachafua mazingira na kuambukiza dada zetu magonjwa pmj na kufundisha vijana wetu kubwia unga, tunataka watalii wastaarabu wenye fedha, mtalii ambaye anakuja TZ siku 10 anaacha dola 10 000 anaondoka na siyo wa kushinda coco beach na forodhani Zanzibar tangu asubuhi kanunua chupa ya maji ya Kilimanjaro kwa Mangi na kula chips mayai au mihogo coco hao hatutaki wabakie huko huko, tuna uwezo kabisa wa kuchagua na kuvutia watalii wenye fedha za ukweli!

kwa mazingira yapi na facilities zipi za kuchagua watalii

angalia south africa na dubai wenzenu walivyofanya, mtalii anachagua services na destinations kutokana na status yake.

maendeleo ni process mkuu kama ndo vision yetu hiyo tujipange taratibu sio kukurupuka na zima moto.. viongozi wetu wanajiaibisha sana
 
Acha tujioneee, huyu mtalii wa hali ya juu ambaye pengine anaweza ona twiga yule yule wa Serengeti kwa $ 50 arafu Kenya iwe $35 bado aje kwetu kwa kua sisi hatu hitaji mtalii maskini? Ina lojiki kweli hii ya waziri?

Bibo hivyo gari zenye namba za majini kupandishwa vile ina maana watu ndio wata vutiwa zaidi au hata hao wachache wanaweza wakajitoa?

Tanzania bana, Mungu atuhurumie
 
Back
Top Bottom