VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

VAT katika Utalii: Prof. Maghembe asema hatuhitaji watalii masikini

Katika taarifa ya habari ya star TV prof maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti)
Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!??
Magufuli anaendesha team yenye Ph D holders masters holders, kwa kweli ni wasomi wakubwa wenye CV kubwa kubwa Africa na Duniani, sasa ni zamu yetu kujua kuwa ni wasomi kweli au ni wasomi kwenye makaratasi tu? haya tutayajua miaka michache ijayo, nadhani prof mmoja alipiga kitwanga akazama bunge na hangover huyo tumeshamuondoa kwenye kundi la wasomi bali ni kwenye makaratasi na kumbi za kitwanga tu tusubiri na wengine nao tutawajua hivi karibuni kama kweli ni wasomi wa kutatua matatizo ya watu au ni wasomi wa makaratasi.
 
Sijui ni kwa nn lazima tupingekila kitu !

Pamoja na vat : naamini still mtalii anekwenda Kenya atalipa zaidi kama unakumbuka exchange rate ya ksh na tsh !
 
Hao watalii maskin ndio wengii na wakija tunapata ajira watu wengi,mfano watalii wanao lipia camping safaris.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, kuna watalii wengi sana choka mbaya wanakuja wanakaa beach wanaunua maji ya Kilimanjaro wanakula chips mayai na kuondoka lkn wanaingia kwenye takwimu hao hatutaki hao kwanza wanachafua na kuharibu mazingira yetu, tuwekeze kwa Watalii middle class na wenye fedha siyo watalii beach boy!

Hii ndiyo Serikali niliyokuwa naishubiria maisha yangu yote!​
Dah....akili zako unazijua mwenyewe... hivi hao watalii wa middle class unawakaribisha kwa miundombinu gani uliyonayo...barabara...ndege...hotel???

Hivi kauli ikitolewa na mwana ccm mwenzako unafungwa na akili zako.
 
Sijui ni kwa nn lazima tupingekila kitu !

Pamoja na vat : naamini still mtalii anekwenda Kenya atalipa zaidi kama unakumbuka exchange rate ya ksh na tsh !
Hueleweki......mtalii analipa kwa USD au Kenyan shilling?
 
N.B:Kenya wanaokimbiza kwenye uchumi afrika mashariki na kati wamewapokea hao watalii kwa kutoweka VAT,Tanzania tunakosea wapi?
Kuna siku nilimsikia sikuamini nikadhani amekosea tu. Kwamba hatutaki watalii wa kubeba vibegi mgongoni tunataka watalii matajiri. Sijui mambo ya utalii hivyo siwezi kusema sana ila nitasema kidogo hasa kuhusu watalii wa ndani.

Katika budget ya 29.5 tril every cent will count hivyo tusiache hata senti moja ambayo tuna fursa nayo. Hao masikini waje tu ili mradi tunawakamua na wanatuachia vijisenti vyao. Wizara pia ihamasishe utalii wa ndani ili napo tupate mapato. We need every single cent to be credited to our government coffers.

Kuna siku nilipita Serengeti nikalipa kwa kutumia VISA kadi lakini nilipofika lango la Ngorongoro naambiwa ati lazima niwe na kadi yao ama ningelipia bank niende na payslip, hawakubali VISA card! Hiyo gharama ya kulipa sijui ningeijuaje na kadi zao zinapatikana Arusha wakati mimi natokea Bunda. Hawataki VISA wakati ni kadi ambayo inatumika dunia nzima. Hii inaleta ukakasi wa bure. Turekebishe kasoro ili tupate maduhuli! Tusiwanyanyapae watalii wawe wa ndani wenye kulipa Tshs. 1,500.00; wawe matajiri toka nje wanalipa €2,000 kuua swala ama wale wanaokuja toka nje na wanalipa $130.
 
Katika taarifa ya habari ya star TV prof maghembe amesema Tanzania inahitaji watalii wa hadhi ya juu na sio masikini(wa bajeti)
Watanzania tuna mbwembwe,huu uchumi unaochechemea ndio tunaoringia!??
Maghembe ni mzigo mzito!
 
Waziri kiazi kweli. Yaani yule mzee ni mzigo serikali zote sijui hata kwanini anatoboaga kwenye uwaziri!!
 
Kama kweli katamka ashauliwe aombe msamaha mapema sana, wenzentu wanaumoja sana sector ya utalii inaweza kuchafulowa vibaya sana
 
Mh. Rais amwangalie vizuri huyu mtu anachemka sana kwenye hii wizara. Ataifanya idorore sana.

Hawa jamaa wa backpackers wakisikia na wakaanza kutangaza kuwa Tanzania imetangaza haihitaji watalii na kuanza kutuponda kwenye mitandao ya internet nakuhakikisheni hata hao matajiri hawatakuja. Hakuna kitu wenzetu wazungu wanakiweza kama umoja wa kupinga jambo fulani. Tena wanafanyiwa wao wakati kuja kwao tu wanachangia pato lako la Taifa🙁🙁🙁

Tukumbuke mfumo wa mawasiliano sasa hv ni through internet. Taarifa zinasambaa kwa haraka mno kama moto wa petrol. Tutapatwa na janga la hatari ambalo hatutalisahau. Wenzetu Kenya utalii wao umeenda chini kwa sababu ya terrorism, ndo maana hata wale wengi ambao wangeenda kenya wapo Tz. Wakishaanza kwenda hapo jirani na hivi viongozi wanasema hawawahitaji tutegemea angako kubwa sana.

Maghembe ayakane hayo maneno na si kukana tu aangalie namna ambavyo wizara itawavutia zaidi hawa watalii wa chini. Kwa ujumla hawa ndo watangazaji wakubwa wa Utalii katika nchi. Na ndo watoaji wazuri wa taarifa wanaosababisha hao matajiri kuja kutembelea Tanzania.

Siyo wa kudharau hata kidogo. Waziri kateleza hapo. Na kama anamaanisha ni kwamba wizara imeshamshinda akae pembeni apewe mwenye uwezo. Otherwise ataharibu kabisa.
 
Hata hii vat inayopendekezwa nafikiri wataalamu wa bajeti hawakushauriana kabisa na TANAPA na TTB kwasababu nimeona gazeti la mwananchi la juzi mkurugenzi wa TTB haungi mkono uwepo wa vat na anasema Kenya wameondoa vat na hivi sasa wanadili zaidi na utangazaji wa vivutio vyao.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%, kuna watalii wengi sana choka mbaya wanakuja wanakaa beach wanaunua maji ya Kilimanjaro wanakula chips mayai na kuondoka lkn wanaingia kwenye takwimu hao hatutaki hao kwanza wanachafua na kuharibu mazingira yetu, tuwekeze kwa Watalii middle class na wenye fedha siyo watalii beach boy!

Hii ndiyo Serikali niliyokuwa naishubiria maisha yangu yote!​

Ungekua unajua namna hiyo pesa wanavyolipa, wanamlipa nani na sisi kama taifa tunapata ngapi usingesema maneno hayo
Watalii wote ambao ni high class wanalipia safari zao kupitia wakala wa utalii nchini kwao wanakotokea na hao wakala wanatuma pesa ambayo inatosha kufanyia oparesheni tu, kama kodi za serikali inamaana park fees na kodi zenginezo ikiwa na maana high class na back pecker wanalipa kiwango sawa kwa serikali yetu.
Tena ni bora ya back packers ambao unasema wanakula chips maana wao wanalipa direct kwa watanzania lkn hao high class wanalipa kilakitu ulaya na wanaka kwenye hotel zinazomilikiwa na wazungu wenzao kimsingi pesa yote wanaicha ulaya
 
Hata hii vat inayopendekezwa nafikiri wataalamu wa bajeti hawakushauriana kabisa na TANAPA na TTB kwasababu nimeona gazeti la mwananchi la juzi mkurugenzi wa TTB haungi mkono uwepo wa vat na anasema Kenya wameondoa vat na hivi sasa wanadili zaidi na utangazaji wa vivutio vyao.

Kenya wame-exempt VAT kwenye park entry fees. Sisi huku tumeondoa exemption. Waziri alitamka dhumuni la kuondoa exemption ni kulingana na wenzetu kama Kenya (wakenya wametugeuka).

Pia Kenya wameenda mbali na ku-exempt VAT kwenye commissions za Tour operators.

Badala ya kubadilisha mambo na kwenda sawa na soko huku tunatoa kauli kwamba hatuwataki watalii maskini na tunamshangilia waziri.
 
Na hii ndio sekta inayochangia sana pato la taifa karibu asilimia 25
 
Na hii ndio sekta inayochangia sana pato la taifa karibu asilimia 25

A major source of foreign currency (Source).

Nchi inayoagiza vitu nje kuliko kuuza vitu nje inapaswa kuheshimu industry inayoleta pesa za kigeni.

Lakini kwa sababu waziri hata uchumi hajui, yeye kupayuka tu bila kujua multiplier effect ya kauli zake.
 
Back
Top Bottom