yes,ni kweli kama waungwana wanavyosema, BEAUTY LIES IN THE EYES OF THE BEHOLDER,Hii ni kweli kabisa, kwani kila mtu ameumbwa na utashi wake na mtazamo wake,na wala huwezi lazimisha unachokiona wewe na kukidefine,basi na mimi niwe hivyo..........Lakini ningependa kwenda mbele zaidi ya hapo,Binafsi uzuri wa hawa dada zetu naweza uweka kwenye makundi mawili,mwonekano wa kitabia na umbo la nje,tukiacha unafiki hapa, kiukweli wanawake wanatofautiana sana kwenye tabia,yawezekana hii ikawa ni mwonekano wa ndani zaidi, lakini tutambue tu kuwa,kuna tabia alizo nazo mwanamke ambazo kiukweli zingeweza kumpendeza mwanaume yoyote yule,ambae angependa kuwa nae.Lakini hili la mwonekano wa kitabia mara nyingi huangaliwa sana pale kipindi mwanaume anahitaji kupata,mwenza wa maisha yake, kwahiyo ukipata huyo mwenye tabia ilo safi na ya kumpendeza mungu,basi hapo waweza sema kuwa umepata mwanamke mzuri.Umbo la nje mara nyingi ni sababu tosha ya kumvuta mwanaume kabla hujaingia kwa ndani zaidi kutaka kumjua,katika kuchunguza hiyo tabia, lakini vile vile inategemea na mahusiano yanayohitaji kujengwa hapo,Hebu tuwe wakweli hapo na tuendelee kutupa kuleeee unafiki,wapo wanawake wazuri bana kwa umbo na sura, hata wadada wenyewe wanajijua bana,sitaki kulisemea sana hili kwani linajulikana wazi tu.Mara nyingi wanaume wanaokimbilia mwanamke mwenye umbo zuri, huwa wanaongozwa na katamaa fulani hivi,(ingawa so wote)Sikumbuki mara ya mwisho sijui ilikuwa lini tu, nilibahatika kumwona mwanamke mwenye umbo zuri,sambamba na tabia ilo safi ni aghalabu sana kukutana na viumbe wenye sifa zote hizi kwa pamoja kwa sasa hivi!!!!!!!MUNGU AWABARIKI NYOTEBWANA ASIFIWE SANA!!!!lol...ngoja niwahi kikombe cha kahawa, asubuhi yote hii nimeshaanza kuchonga mdomo wangu agggghrrrrr!!!!!!!