jipange..usikurupuke!!ujue asilimia kubwa ya wabonge kitu tusipokifaham vyema huwa tunakimbilia kwa suluhisho kuwa ni kibovu au hakifai au hakitengenezeki. Ni kweli kila kitu kina uzuri wake na ubaya wake ila kwa kweli kwa madereva wa sasa wengi wao ni madereva wa magari ya automatic na kama utawapa manual basi ujue watashindwa kuendeshga au kuua gear box kabisaa na wengi wao wangepata sana ajari na kusababisha ajali. Ili kwa mim naona gari ya manual ni nzuri kawa sababau na vigezo vifuatavyo ............................................................ Nitarudi baadae kidogo ngoja nikaswali kwanza
Habari wana JF??
Sie wengine magari ya manual tulijifunzia tu lakini tumekuwa tukitumia automatic kwa muda mwingi sana.
Ok, issue iko hivi...nimekuwa nikitumia gari yenye automatic transmission, sasa kuna jamaa yangu yupo Ulaya nikaomba aniangalizie gari ingine kutoka huko na kanitafutia gari nzuri sana ya 2008 ila ni manual. Kiukweli nimeipenda ila nilihofu kuhusu hiyo transmission yake na kila ninayemgusia ananiambia gari za manual si nzuri ukilinganisha na automatic. Swali ni je kwa nini bado zinatoka na Ulaya wanapenda manual zaidi kuliko Africa na Asia???
Tatizo ni kwamba sijapata mtaalam wa kunifafanulia hasa uzuri na ubaya wa gari za manual kushinda automatic.
Wataalam tumwagieni maujuzi kuhusu hii kitu ili niondoe hii conflict niweze kuchukua kitu nikiwa na raha kumoyo!!!!
Nawasilisha
hii thread haipaswi kuwa hapa jamani
Source??...hapana mkuu,autos zimeanza kutengenezwa toka 80s huko,wangekuwa wana plan ya kuacha wangeacha long t..mimi nimejifunzia auto lakini saivi niko addicted na manual,huwezi kujiita dereva unless umeendesha manual..autos hata mwanangu wa miaka mitano Marcus naweza kumuelekeza akaendesha,you can't take any pride out of it..
siyo kuwa discourage. Maana ya AT ni kuwa na vitu vingi mfano unakuwa na GPS ipo incorporated, n.k.
Watengeneza magari wako kibiashara zaidi na c kwamba lengo kuu ni kurahisisha maisha la hasha japo yote yana uzito tofauti.
Ukweli ni kwamba gari za Auto hazidumu muda mrefu ku compare na Manual so kwao ni biashara tayari na ndo maana gari za cku hizi ikisha pata mzinga basi kwishney wakat rover 109 au scania 111 au Fiat unaweza kukaa nayo mpaka vitukuu maana zinatengenezeka na spare ya chochote zipo wakati auto kama gia zinasumbua badala ya ku replace kinasombua unaambiwa ununue complete gear box....bush shit!!! Imagine Vitz ipate ajari...yaan hakuna ambacho kinatengenezeka...Manual haina ujinga huo.
Binafsi niko addicted na magari ya kizamani maana sina pressure ya spare parts na fundi yeyote anaweza kulitengeneza tena kwa garama nafuu sana.
Kwa taarifa yenu magari ya cku hizi yana time window (yana expire hahaha)
Inategemea unaongelea uzuri gani. kama ni urahisi wa kuendesha sawa ni automatic. kama ni ubora automatic hamna kitu ndugu. Wamezitengeneza kibiashara tu. Ndio mana nchi zilizoendelea hawatengenezi wala hawanunui.
kama unafanya kazi ya kukaa sana nakushauri ununue manual kwani inakufanya uwe bize barabarani kuliko ukiwa AT na kingne manual uaribikaji wake huwa ni mgumu sio sawa na AT na vile vile manual hadi upate ajali ni ngumu sana..
Nimejiuliza sana hilo swali coz nchi zilizoendelea kuna gari manual ya mwaka 2012 sisi huku tunaona kama ni old fashion, naona umezidi kunifunua ufahamu wangu bro, thanx sana!!
Source??...hapana mkuu,autos zimeanza kutengenezwa toka 80s huko,wangekuwa wana plan ya kuacha wangeacha long t..mimi nimejifunzia auto lakini saivi niko addicted na manual,huwezi kujiita dereva unless umeendesha manual..autos hata mwanangu wa miaka mitano Marcus naweza kumuelekeza akaendesha,you can't take any pride out of it..
aa mm naipenda Manual kwani muziki wake naupenda unaweza kwenda mpaka 4, halafu ukarudi 3, lakini ukapitia clutch na ress kama 2 hivi ni lazima utanyanyuka katika kiti kidogo basi usingizi hauji, unakaa kidogo unaitupia 4, halafu ress 2 unaingia over (5)
Lakini AT unalikanyagia weeee watu watadhani ww ni mDADA Du shit
Mkuu gari ni Manual achana na automatic za kike.Nilikuwa na ka-automatic basi ilikuwa kila siku ugomvi na wife yaani gari ikiwepo home tu yeye keshapata safari sasa tangu ninunue automatic aaahh raha tu manake ni mimi tu ndo nayeweza kuizungusha yeye zake lawama tu.