Asilimia karibu 80 ya magari yote madogo yanayotengenezwa sasa ni AT.
Kuna viwanda vya magari vimeacha kabisa kutengeneza manual, wao ni AT tu
Baada ya miaka kadhaa mbeleni magari yote madogo yatakuwa AT na manual itabaki hadithi tu
Dunia inasonga mbele na teknolojia inakuwa, manual inapitwa na wakati sasa.
Watu wanasumbua vichwa kurahisisha maisha na si kupigana kubadilisha gia,
Unaweka kitu kwenye D unaondoka na si mara klachi,mafuta na kuingiza gia kila mara
Ninakuunga Mkono.
Dunia Inaendelea na teknolojia inakua na soon, magari ya manual yatakuwa-phased out.
Kwa nini? Kanuni kuu ya uvumbuzi wa magari ilikuwa ni kumsafirisha binadamu kutoka point A kwenda Point B kwa njia rahisi na nyepesi bila usumbufu mkubwa kadri inavyowezekana.
Tukumbuke kwamba hawa wanaotuletea AT sasa hivi ndio walianza na farasi, wakavumbua mikokoteni inayovutwa na ng'ombe na farasi, wakavumbua yale mastage-coach tuliyokuwa tukiyaona kwenye sinema za Cowboys na ndio waliovumbua magari ambayo mwanzo hayakuwa na tairi zenye upepo bali matairi magumu tu ambayo yalipkanyaga jiwe dogo tu yangeweza kupindua gari!
Hawa ndio ambao magari yao ya mwanzo ilibidi kupigwa 'hendel' ili kuwaka lakini sasa unaweza kuiwasha hata ukiwa nje hujaingia ndani ya gari! Yote haya ni maendeleo ya kumfanya binadamu asafiri kwa raha kutoka point A kwenda B kwa tabu ndogo kadri inavyowezekana.
Ni wazi kwamba katika muda mchache ujao watu hawa watataka binadamu kusafiri bila haja ya kutoka jasho na mapovu kugombana na gia na klachi za gari!
Pale ujerumani kuna mji ambao jina lake limenitoka kidogo ambao umetengwa maalumu kwa ajili ya majaribio ya kumuwezesha mmiliki wa gari kutoka ndani nyumba kuingia ndani ya gari na kusema tu "TO THE OFFICE" ama kuminya kuingiza tu data kwenye comp na gari hilo likakata mitaa kumpeleka ofisini huku yeye akiwa amekaa nyuma ya gari akisoma gazeti bila kuhangaika kufanya kitu chochote! Ndiko tunakoelekea.
Kuna mdau amesema kuwa kama makampuni ya magari yalikuwa yanataka ku-phase out Manual basi wangeishafanya hivyo maana magari ya AT yameanza miaka ya 80!
Tukumbuke kwamba tofauti na sisi ambao mipango yetu haivuki miaka 10 mbele, wenzetu hawa wanaweza kupaga jambo hata miaka 40 ama 100 mbele!
Isingekuwa rahisi katika kipindi cha miaka 30 tu kuanzia miaka ya 80 waweze kuyatoa barabarani magari yote ya Manual lakini ukweli wanafanya hivyo taratibu kiasi kwamba wakati mwingine inachukua muda kutambua hili.
Tukumbukeni tu kuwa miaka 20 tu nyuma tulikuwa na mabasi ya Leyland Albion ambayo dereva wake alipaswa kuwa na kifua kutokana na sukani yake na gia yake (ambayo ilikuwa inaanzia mgongoni kwa dereva!) kuwa ngumu na nzito kama zege! sasa mabasi haya ni historia na vijana wanaendesha scania na yu tong zenye vigia unavyoweza kubadilisha kwa ncha za vidole kama sio za kucha!
Mifano ipo mingi. Tulikuwa na treni za mvuke unaotokana na makaa, zikaja za dizeli na sasa wenzetu wana si tu treni za kasi za umeme bali kuna hata za sumaku ambazo treni haina magurudumu lakini inavutwa na vipande vya sumaku na kuwa 'inaelea' kwenye njia zake badala ya magurudumu ya vyuma!
Tulianza na 'glamaphone' ambazo ilibidi uweke 'ufunguo' ndipo icheze santuri zako, ikaja 'changer' ambazo tulipanga santuri sita zikawa zinadondoka moja moja na kucheza lakini sasa ninaamini kuna nyumba chache sana ambazo zina kitu kinachoitwa Record Player wakati watoto wetu sasa wanatunza hata nyimbo 100 kwenye IPod IPad na I nini sijui zao na kuzicheza wakati wowte na mahali popote wapendapo!
Na Remote Control je? Katika vifaa mbavyo mwanzo nilivipiga vita kwa kuona ni kwa ajili ya Wavivu tu,ilikuwa ni remote control! Lakini imebidi nikubaliane tu kwamba haya ni maendeleo ambayo yananifanya niweze kubadilisha stesheni, kupandisha na kupunguza sauti nikiwa nimelala kivivu kwenye kochi bila kulazimika kunyanyuka ama kumuita mtu anifanyie hivyo!!
Kwa hiyo tutake tusitake, miaka si zaidi ya 25 tu ijayo magari ya Manual yatakuwa kwenye majumba ya makumbusho na pengine tutakuwa tunabishana kuhusu Uzuri wa magari kati ya yale ya AT na yanayoendeshwa kwa kupewa amri tu na mdomo; "Kata kushoto!", "Simama!" "Piga hon!" "Ongeza Spidi!" na kadhalika na kadhalika!
Mabadiliko ni lazima. Tujiandae tu kuyapokea.