Uzuri wa magari ya automatic na manual...!!

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,503
6,374
Habari wana JF??

Sie wengine magari ya manual tulijifunzia tu lakini tumekuwa tukitumia automatic kwa muda mwingi sana.

Ok, issue iko hivi...nimekuwa nikitumia gari yenye automatic transmission, sasa kuna jamaa yangu yupo Ulaya nikaomba aniangalizie gari ingine kutoka huko na kanitafutia gari nzuri sana ya 2008 ila ni manual. Kiukweli nimeipenda ila nilihofu kuhusu hiyo transmission yake na kila ninayemgusia ananiambia gari za manual si nzuri ukilinganisha na automatic. Swali ni je kwa nini bado zinatoka na Ulaya wanapenda manual zaidi kuliko Africa na Asia???

Tatizo ni kwamba sijapata mtaalam wa kunifafanulia hasa uzuri na ubaya wa gari za manual kushinda automatic.

Wataalam tumwagieni maujuzi kuhusu hii kitu ili niondoe hii conflict niweze kuchukua kitu nikiwa na raha kumoyo!!!!

Nawasilisha
 
ujue asilimia kubwa ya wabonge kitu tusipokifaham vyema huwa tunakimbilia kwa suluhisho kuwa ni kibovu au hakifai au hakitengenezeki. Ni kweli kila kitu kina uzuri wake na ubaya wake ila kwa kweli kwa madereva wa sasa wengi wao ni madereva wa magari ya automatic na kama utawapa manual basi ujue watashindwa kuendeshga au kuua gear box kabisaa na wengi wao wangepata sana ajari na kusababisha ajali. Ili kwa mim naona gari ya manual ni nzuri kawa sababau na vigezo vifuatavyo ............................................................ Nitarudi baadae kidogo ngoja nikaswali kwanza
 
well manual cars seem to have issue when driving upside on slopy area you have to accelarate too much to go further,while in manual you can easily go anywhere, manual cars make driver to be very busy during driving, automatic cars are for lazy people and girls.
 
Inategemea unaongelea uzuri gani. kama ni urahisi wa kuendesha sawa ni automatic. kama ni ubora automatic hamna kitu ndugu. Wamezitengeneza kibiashara tu. Ndio mana nchi zilizoendelea hawatengenezi wala hawanunui.
 
Twaendelea kuvuta subira Sheikh!!! Walisema subira yavuta kheri, tupo pamoja mkuu....!!
 
well manual cars seem to have issue when driving upside on slopy area you have to accelarate too much to go further,while in manual you can easily go anywhere, manual cars make driver to be very busy during driving, automatic cars are for lazy people and girls.

:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:

Hapo bolded, Lugha Gongana!!
 
Inategemea unaongelea uzuri gani. kama ni urahisi wa kuendesha sawa ni automatic. kama ni ubora automatic hamna kitu ndugu. Wamezitengeneza kibiashara tu. Ndio mana nchi zilizoendelea hawatengenezi wala hawanunui.

Nimejiuliza sana hilo swali coz nchi zilizoendelea kuna gari manual ya mwaka 2012 sisi huku tunaona kama ni old fashion, naona umezidi kunifunua ufahamu wangu bro, thanx sana!!
 
kama unafanya kazi ya kukaa sana nakushauri ununue manual kwani inakufanya uwe bize barabarani kuliko ukiwa AT na kingne manual uaribikaji wake huwa ni mgumu sio sawa na AT na vile vile manual hadi upate ajali ni ngumu sana..
 
Mkuu asiyejua gari ya manual hataweza kukupa uzuri wake, hasa kama wewe ni mpenzi na una interest na operation ya gari.

Ukilijulia gari la manual na gear zake gari waweza kulipeleka kwa spidi uipendayo kulingana na operation ya engine na gearbox.

Siyo rahisi kunielewa lakini kama una a powerful engine( hata gari ya kawaida kama 1S engine ya six cylinder Toyota Chaser) unaweza chezea power ya engine upendavyo.

Niliwahi jaribu hilo kuna jamaa, na najua ana automatic gearbox,alitaka tupimane ubavu kuanzia SalendeR mpaka St Peters miaka ya nyuma kidogo na kulikuwa hakuna foleni.

Nilipiga gia ya kwanza mpaka rev. Elfu sita kabla ya kuingia gear ya pili na baadaye ya tatu.
Hapo gari inachomoka kama mshale na hakuna automatic inaweza hilo maana yenyewe itajiregulate kabla revs hazijazidi elfu nne au tano.
Angalizo tu ni kuhakikisha unafunga mkanda maana gari literally linapaa!
 
Yaaaaaaaaaaaaap. Gari ni manual mkuu asikudanganye mtu. Manual ni imara na hautakuwa na urafiki wa karibu sana na gereji kama automatic. Ila inahitaji muda kulizoea kuliendesha na pia linahitaji stamina maana ukiwa kwenye foleni na uko kwenye mwinuko kama hujuwi ku-balance clutch na accelerator litakuwa linarudi nyuma kila utakapo kuondoka na waweza kumgonga aliye nyuma yako kama kakaa karibu sana na wewe. Pia mwanzoni litakusumbua kwa kuzimikazimika hasa kwenye mataa na kwenye foleni ila ukijazoea ukamudu hayo wewe ni derava hasa na utalifurahia gari lako.
 
Mi binafsi napenda manual simply because likizimika sitalala niani, ntasukumwa ntaondoka especially kama ni la petroli. Pia si complicated sana kama automatic transmission ambalo kila kitu kinategemea umeme wa gari. Nadhani hii inalifanya gari la manual kudumu zaidi kuliko automatic. Pia gari la manual for rough roads kama hapa kwetu haina shida kama automatic. Lichukue kama utaweza kuliendesha kwani utakuwa busy sana na usukani na miguu yote kuliko automatic ambalo ni la kivivu sana.Mimi nikiambiwa nichague gari ni MANUAL.
Habari wana JF??

Sie wengine magari ya manual tulijifunzia tu lakini tumekuwa tukitumia automatic kwa muda mwingi sana.

Ok, issue iko hivi...nimekuwa nikitumia gari yenye automatic transmission, sasa kuna jamaa yangu yupo Ulaya nikaomba aniangalizie gari ingine kutoka huko na kanitafutia gari nzuri sana ya 2008 ila ni manual. Kiukweli nimeipenda ila nilihofu kuhusu hiyo transmission yake na kila ninayemgusia ananiambia gari za manual si nzuri ukilinganisha na automatic. Swali ni je kwa nini bado zinatoka na Ulaya wanapenda manual zaidi kuliko Africa na Asia???

Tatizo ni kwamba sijapata mtaalam wa kunifafanulia hasa uzuri na ubaya wa gari za manual kushinda automatic.

Wataalam tumwagieni maujuzi kuhusu hii kitu ili niondoe hii conflict niweze kuchukua kitu nikiwa na raha kumoyo!!!!

Nawasilisha
 
mpango mzima manual bana mkuu......asikwambie mtu...unapiga gia hadi unasikia kuwa kweli unaendesha gari....kama unataka fanya safari kidogo atleast hapa na chalinze na kurudi ukiwa na manual na ndo utajua utamu wake hasa hasa kama una injini powerful kiaina mkuu....
 
manual ndio mpango mzima coz hata kwa swala la fuel consumption manual is the best one coz wewe ndio unaipima, pili manual hata inapotokea brake zimeferi unaweza kupunguza gear mpaka speed ikawa ambayo ni salama kabisa, tatu kwa wanaopenda hata racing manual ni nzuri sana.......weakness yake kama sio muangalifu kuua gear box ni easy, pia kuna imani manual delay to speed up from the starting point tofauti na auto, thou kwa new model cars zipo faster pia
 
Manual au automatic inategemea na matumizi ya mtu anayenunua , na zote zina umuhimu wake katika matumizi, kama unahitaji gari kwa matumizi ya safari zenye kuhitaji max power output kama vile milima matope au racing nunua manual ,kama unatcumia kwenye barabara zenye foleni safari fupi fupi automatic ni chaguo sahihi.
 
ujue asilimia kubwa ya wabonge kitu tusipokifaham vyema huwa tunakimbilia kwa suluhisho kuwa ni kibovu au hakifai au hakitengenezeki. Ni kweli kila kitu kina uzuri wake na ubaya wake ila kwa kweli kwa madereva wa sasa wengi wao ni madereva wa magari ya automatic na kama utawapa manual basi ujue watashindwa kuendeshga au kuua gear box kabisaa na wengi wao wangepata sana ajari na kusababisha ajali. Ili kwa mim naona gari ya manual ni nzuri kawa sababau na vigezo vifuatavyo ............................................................ Nitarudi baadae kidogo ngoja nikaswali kwanza

Na vigezo hivyo ni;
1. Unakuwa na nafasi ya kui-control mwenyewe pale unapopanda mlima au kushuka tofauti na automatic
2. Ikizima au betri imeleta shida unaomba msaada wa kusukumwa inawaka
3. Nyingi zinasukuma tairi kwa nyuma hivyo zile barabara zetu za utata zenye mawe mengi na makubwa ni rahisi kupita
4. Inakufanya unakuwa na concetration kubwa huwapo barabarani maana unacheza na gia, clutch, brake na accelerator
5. Ina nafasi kubwa ya kudumu muda mrefu kwa kuwa hutopata usumbufu wa watu kukuazima kwa kuwa wengi ni wataalamu wa automatic
 
Yaaaaaaaaaaaaap. Gari ni manual mkuu asikudanganye mtu. Manual ni imara na hautakuwa na urafiki wa karibu sana na gereji kama automatic. Ila inahitaji muda kulizoea kuliendesha na pia linahitaji stamina maana ukiwa kwenye foleni na uko kwenye mwinuko kama hujuwi ku-balance clutch na accelerator litakuwa linarudi nyuma kila utakapo kuondoka na waweza kumgonga aliye nyuma yako kama kakaa karibu sana na wewe. Pia mwanzoni litakusumbua kwa kuzimikazimika hasa kwenye mataa na kwenye foleni ila ukijazoea ukamudu hayo wewe ni derava hasa na utalifurahia gari lako.

Unapiga hand brake tu alafu wakati wa kuondoka unakanyaga accelerator kwanza ikishitua kuondoka unaitoa handbrake maana ku-balance clutch na accelerator kwa sie madereva wa kichina hukawii kuunguza clutch
 
Nimejiuliza sana hilo swali coz nchi zilizoendelea kuna gari manual ya mwaka 2012 sisi huku tunaona kama ni old fashion, naona umezidi kunifunua ufahamu wangu bro, thanx sana!!

si unajua wengi wanapenda AT kwa kuwa wanatumia na wake zao hivyo kumchosha mtoto wa kike na manual inakuwa ni noma
 
Back
Top Bottom