binafsi nafagilia sana MANUAL haswa huku mikoani kusiko kua na foleni utaipenda.
1. wese inakula kidogo coz inakupa great control kwenye gia. mfano kwenye kilima kikubwa unapanda na namba 2 na manual lakini ikiwa AT lazma ijiset kwenye gea namba 1 ambayo ina nguvu zaidi na inakula wese.
2. manual ni nzuri kwa sehemu zisizo na foleni kama dar, wakati AT ni nzuri kwenye foleni kali, haupati maumivu ya kucheza na clutch, accelerator na breki kwa wakati mmoja.
3. vyuma vya mjapani vya manual ni cheap kuliko ATs!
4. manual ukiendesha kweli unajiona unaendesha gari na sio AT (kwa kina mama, wadada na watoto!)
hahahaaa, kweli wewe sio dereva!.
kama mlima ni mkali kama ile ya kule kimara bonyokwa au kilungule lazma likushinde, kubalance clutch na accerator its too simple than using the handbrake, maana ukicheza kidogo ikakushinda wakati wa kuachia handbrake lazma gari litazima. sasa pata picha gari ndio limeshazima linaanza kurudi nyuma halafu linatumia hydraulic, means breki hazikamati, stering inakua ngumu vibaya mno!.
uko sawa kabisa mkuu!, foleni za dar ni nuksi, ukifika home mguu wa kushoto unauma balaa kwa kucheza na clutch na breki always si unajua zile daladala linataka kukuchomekea na wewe unalibania kwa hiyo hapo lazma ufanye kazi ya ziada kucheza na clutch na breki!, lakini ukiwa na AT aaah wala haikupi shida.
kuna siku bwana nilikua naendesha manual, sasa kumbe brake fluid ilikua imevuja na ikawa imepungua sana halafu mbele yangu ndio foleni imeanza kila nikikanyaga breki nakuta holaaaa, kilichonisaidia ni kupunguza mwendo kwa kutumia gea, assume ingekua AT hapo nini kingetokea kwa gari ilokua mbele yangu.
karibu asilimia 99 ya magari ya serikali ya JMTz ni MANUAL especially kama limenunuliwa likiwa jipya kabisa!. si unajua lazma wafuate mchakato wa manunuzi, so lazma mzabuni anaeiuzia ataambiwa apeleke kitu cha manual wakijua kuna kukabiliana na barabara mbovu.
mengine yanayotolewa kama misaada au yaliyotumika kwenye miradi ndio wakati mwingine huwa AT
aaah wewe utaua gear box, yani kutoka gea namba tano uingize gea namba wani kweli!??.
unapoingiza gea lazma uingize moja baada ya nyingine KIUSALAMA na UTUNZAJI wa gearbox, hata kushusha gea pia lazma ushushe moja baada ya nyingine (labda kama una dharura endapo breki zitafeli unaweza toa 5 ukashusha mpaka moja kupunguza kasi ya injini ingawa gea itakua NGUMU sana kuingia!).