Uzuri/urembo/utanashati. Vs Jamii



Niliwahi kwenda ofisi fulani huko Dar (posta) ambapo nitaka kupewa data fulani. Mara ya kwanza niliulizwa maswali na mdada fulani aliyekuwa masjala, na akasema kuwa niende kuleta barua toka kwa boss wangu (Morogoro) ndipo niruhusiwe kuonana na boss wa hiyo ofisi. Mara ya pili nilienda na barua yangu nikakuta kuna watu wengi wanasubir kumuona yule boss, na nilipoulizia kwa yule dada, akaangalia haraka haraka barua yangu akasema haijielezi vizuri, na hata hivyo boss wao alikuwa na shughuli nyingi siku hiyo. Nili-note kuwa yule dada alikuwa hajaniangalia sana usoni. Nilikuwa nimevaa t-shirt. Nilipiga mahesabu ya kurudi tena hadi Moro, nikaona ni usumbufu mkubwa, so nitafute namna.
Nilitoka pale ofisini, nikaenda internet cafe fulani nikai-type ile barua kwa kiingereza, nikaiprint na kusaini sehemu ya boss wangu kwa sahihi ya kuforge.

Nilienda kwenye duka la kuuuza nguo, hapo hapo posta nikanunua shati na tai, na nikavivaa pale pale. Nilitoka nje nikazunguka nikaona jamaa anauza miwani, nikanunua moja plain (kama ya matatizo ya macho) nikavaa. Nilirudi pale ofisini baada ya kama saa moja, nikamkuta yule dada kama kawaida anahoji na kuwarudisha watu huku wachache wakiruhusiwa kumuona boss.
Nilianza kujieleza upya kwa yule dada lakni wakati huu nikitumia kiingereza. Yule dada alijaribu kujibizana na mimi kwa kiswahili, lakini nilijifanya sielewi, huku nikisisitiza natokea south africa, na nilijitahidi kuongea mambo mengi sana kumchanganya. Aliiangalia barua yangu, hata hakugundua kuwa haikuwa na muhuri, akaniambia 'wait there', na baada ya kama dk mbili akaniambia you can enter.

Nikachoma zangu ofisini kwa boss, nikalonga nae kiswahili. akanielewa akaniprintia data zangu nikatimua huku najisifu kuwa pamoja na ushamba wangu wa mikoani, leo nimefanikiwa kumuingiza mjini wa Dar.
 
Mbu hivi mimi ni Architecture nikienda site nimevaa suti kuna kosa kweli lol!!

...lol...hakuna kosa kabisa ndugu yangu, ila ukimkuta mjenzi wako kavaa suti, tai, na skuna huku anachanganya zege ujue umeliwa!
 


Hii kitu imenikumbusha nisha wahi itwa ofisi moja nikiwa msibani kati kati ya shuguli za sie akinia mam... Huyo nikachomoka na kuenda moja kwa moja katika hio ofisi kubwa hapa mjini... Well kufika hapo huyo dada alinipokea kwa pozi mno kana kwamba she is doing me a favour, kisa nimevaa Dera na vilemba... The next time (a week later in fact...) nikaenda ofisi hio hio kwa dada yule yule (nikiwa nimevalia kimjini mjini...).... alivyonipokea/ku smile na ile ya slight kunyanyuka as if her world revolved around solving my problem.... Yaani alikua amenisahau kabisa kua ndie yule ali mistreat just a week before.... yaani hata sikuangaika kumkumbusha....
 
Reactions: Mbu
Ashadii una maana Kikwete naye alibebwa kuupata Urais kwa vile Hendisamu? hahaha acha utani wewe...


Magulumalu naona tu wanitafutia BAN hapa....lol... Sio kweli bana ila tu wale viti maalum..... mmmmmh!!!
 
Magulumalu naona tu wanitafutia BAN hapa....lol... Sio kweli bana ila tu wale viti maalum..... mmmmmh!!!

Nikusaidie tu kujibu. Ndio... alichaguliwa kutokana na sura yake, tena kura nyingi alipata kutoka kwa wanawake...
 



Tuko hii Kali..... Khaaa!! What an experience.... it is worth it.... and Speaks volumes.....

Na bana sio woote tuliopo mikoani ni washamba....lol... wengine ni wajanja kuliko hata wa town....
 

...lol...hakuna kosa kabisa ndugu yangu, ila ukimkuta mjenzi wako kavaa suti, tai, na skuna huku anachanganya zege ujue umeliwa!



ha ha ha.... wapi PA??? aje aone suti site!!! lol
 
Reactions: Mbu
Nikusaidie tu kujibu. Ndio... alichaguliwa kutokana na sura yake, tena kura nyingi alipata kutoka kwa wanawake...




lol...............lol................lol............

Wamama tupendavyo ma HB!!!
 

post #51 sorted.


Hio statement in purple has made my eveninng....lol...

Kwa hiyo ile first glance inakushawishi but akija vibaya haudanganyiki?? really funny!

...lol...hapana bana, namaanisha najipa muda kumjua mtu than 1st appearance...he he
...ila huyu kwa mtazamo wa kwanza tu najua ni mjeuri, ona kimdomo chake!
 
Magulumalu naona tu wanitafutia BAN hapa....lol... Sio kweli bana ila tu wale viti maalum..... mmmmmh!!!


lkn mie na wewe tena? Haya tumwache Mkulu wetu maana mhhh no coment mie...Kumbe ndo maana mie kazi sipati, misura hii bwana, dah lkn Nafurahi my honey wangu ananizimikia nilivyo maana hana wasiwasi wa kuporwa...
 
 
Tuko hii Kali..... Khaaa!! What an experience.... it is worth it.... and Speaks volumes.....

Na bana sio woote tuliopo mikoani ni washamba....lol... wengine ni wajanja kuliko hata wa town....

Na mara nyingi mtu analazimika kuwa mjanja kutokana na shida anazokutana nazo. Dar kuna shida nyingi sana?
 

post #51 sorted.




...lol...hapana bana, namaanisha najipa muda kumjua mtu than 1st appearance...he he
...ila huyu kwa mtazamo wa kwanza tu najua ni mjeuri, ona kimdomo chake!

Mbu naona na wewe ushaanza kujudge book for its cover sasa
Kimdomo tuu umeshamjua ni jeuri
 
Reactions: Mbu
Nikusaidie tu kujibu. Ndio... alichaguliwa kutokana na sura yake, tena kura nyingi alipata kutoka kwa wanawake...


mkuu inakuwaje? unatumiaga kale ka mbuzi ketu? tukutane tukale lini? maana umemwokoa Ashadii..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…