Uzinduzi wa Sinodi ya 16 ya Maaskofu Katoliki Duniani: Homilia ya Askofu Mkuu Ruwaichi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478

Askofu Mkuu Jude Thadeus Ruwaichi, wa JImbo Kuu la Dar es Salaam, akitoa homilia

Usuli

Tarehe 17 Oktoba 2021, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam Mhasham Jude Thaddeus Ruwaichi aliongoza Ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya Uzinduzi wa Sinodi ya 16 ya Maaskofu Katoliki.

Ibada hiyo ilifanyika katika viwanja vya Kituo cha Msimbazi, kilichoko eneo la Ilala katika Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Kaulimbiu inayonogesha mchakato wa Sinodi hii ni: “Kwa Ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume.”

"Napenda niseme kwa kusisitiza, katika mwendo wa sinodi hakuna tofauti kati ya Askofu, Padre, Mtawa, Mlei. Wote mtashiriki kwa usawa kama wana Kanisa, na kama wafuasi na wajumbe wa Kristo," alisema Askofu Mkuu Ruwaichi.

Kwa mujibu wa miongozi ya Kanisa Katoliki, swali la msingi linaloongoza mashauriano katika sinodi hii ni:

Katika kutangaza Injili, kwa njia ya Kanisa la Sinodi, waumini “husafari pamoja.” Je, huku “kusafiri pamoja” kunafanyikaje leo katika Kanisa lako mahalia? Na je, ni hatua gani ambazo Roho Mtakatifu anatualika kuchukua ili tuweze "kusafiri pamoja” na kukua wakati wa “kusafiri pamoja”?

Kwa ajili ya kuwasaidia waumini kuchangia kwa njia bora zaidi katika mashauriano haya, swali hili limegawanywa katika maeneo kumi ya mada ambazo zinaelezea nyanja tofauti za maisha ya Kanisa.

Maeneo hayo kumi (10) ni Sinodi kama safari ya Pamoja, Utamaduni wa kusikiliza, Utamaduni wa kuzungumza, Kuadhimisha Ekaristi, Kuwajibika kwa pamoja katika utume, Mazungumzo katika kanisa na jamii, Kushirikiana na madhehebu mengine ya Kikristo, Mamlaka na ushiriki, Kutambua na kuamua, na Kujiunda katika sinodi.

Kwa ujumla, swali kuu lililotajwa hapo juu limefafanuliwa kwa njia ya kugawanywa katika maswali madogo 50, kama nitakavyoonyesha hapa chini baadaye kidogo.

Kiini cha homilia

Sehemu muhimu ya homilia ya Askofu Ruwaichi, kama video hapo juu inavyoonyesha, kuanzia dakika ya 11, ni kauli zake zifuatazo:

"Nudugu zangu, Sinodi tunayozindua leo, ni safari ya miaka mitatu.

"Safari inayoanza mwmezi huu wa kumi mwaka 2021, na ambayo itafikia kilele chake mwezi wa kumi mwaka 2023.

"Katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kama mlivyoelezwa katika utangulizi aliotoa Baba Askofu Mshemba, tumeishaanza kwa kuunda jopo la kuhamasisha, tumeishaanza kwa kutoa semina katika dekania zote 12.

"Kwa hiyo, mnalo wazo kuhusu sinodi. Kuna wanaonipelekea meseji wakiuliza maswali kama, “Hivi kwa nini sinodi ya maaskofu?”

"Ndugu zangu, hilo sitalijibu leo. Maanake, jopo la sinodi litaendelea kufanya kazi kati yenu na Pamoja nanyi likijibu maswali yenu, likichukua mawazo yenu, likipokea ushiriki wenu katika mwendo wa sinodi.

"Mwaliko wangu kwa kila mwana Dar es Salaam, Baba, Mama, mzee, kijana, mtoto, yeyote mwenye changamoto ya Maisha au ya kivile, kila mmoja ajisikie kwamba hii ni fursa yake ya kushiriki ipasavyo katika kuchangia mawazo kuhusu Kanisa na utume wake.

"Nawaombeni msiogope, msijifiche, na msiache kutumia fursa hii.

"Napenda niseme kwa kusisitiza, katika mwendo wa sinodi hakuna tofauti kati ya Askofu, Padre, Mtawa, Mlei.

"Wote mtashiriki kwa usawa kama wana Kanisa, na kama wafuasi na wajumbe wa Kristo.

"Kwa hiyo, tambua fursa yako.

"Msikilize Roho Mtakatifu, na twambie yale ambayo unadhani Roho Mtakatifu anakutuma katika ukweli, katika unyofu, katika uadilifu, ulishirikishe Kanisa.

"Na unaposhirikisha shirikisha kwa unyofu, shirikisha kwa unyeyekevu.

"Usishirikishe kama mtu ambaye ndiye peke yako tu umepewa ukweli wote.

"Maana wapo na watu wa hivyo hivo pia.

"Ukidhani kwamba ni wewe tu unapewa ufunuo unaweza kusema sasa mimi nimefunuliwa hivi, kwa hiyo nawaagiza fanyeni vile.


"Hapana.

"Sema kile ambacho roho anakutuma useme katika unyofu, katika ukweli, katika unyenyekevu na katika Imani safi na Takatifu ya KIkatoliki."


Dodoso la maswali kwa ajili ya waumini

Tayari Jimbo Kuu la Dar es Salaam limeandaa dodoso lenye maswali kadhaa na kuyasambaza kwa waumini kupitia parokia na Jumuiya Ndogo Ndogo ili kukusanya mawazo yao juu ya Kanisa.

Swali la msingi katika dodoso

Swali la msingi katika dodoso hilo ni hili lifuatalo:

Katika kutangaza Injili, kwa njia ya Kanisa la Sinodi, waumini “husafari pamoja.” Je, huku “kusafiri pamoja” kunafanyikaje leo katika Kanisa lako mahalia? Na je, ni hatua gani ambazo Roho Mtakatifu anatualika kuchukua ili tuweze kukua wakati wa “kusafiri pamoja”?

Maeneo Kumi ya dodoso


Kwa ajili ya kurahisisha ukusanyaji wa mawazo ya waumini, swali kuu limegawanywa katika maswali madogo 50 yanayoanguka katika maeneo yafuatayo:

  1. Sinodi kama safari ya Pamoja,
  2. Utamaduni wa kusikiliza,
  3. Utamaduni wa kuzungumza,
  4. Kuadhimisha Ekaristi,
  5. Kuwajibika kwa pamoja katika utume,
  6. Mazungumzo katika kanisa na jamii,
  7. Kushirikiana na madhehebu mengine ya Kikristo,
  8. Mamlaka na ushiriki,
  9. Kutambua na kuamua, na
  10. Kujiunda katika sinodi.

Kwa ujumla, swali kuu limefafanuliwa kwa njia ya maswali madogo 50, na maswali ya dodoso kwa kila mada iliyotajwa hapo juu ni kama ifuatavyo:

Maswali kuhusu Sinodi kama safari ya Pamoja


Ikizingatiwa kwamba, katika Kanisa na katika jamii, tuko bega kwa bega katika safari ile ile:

  1. Katika Kanisa lako mahalia, ni akina nani “wanaosafiri pamoja”?
  2. Tunaposema: “Kanisa letu,” ni nani aliye sehemu yake?
  3. Ni nani anayetuuliza tusafiri pamoja?
  4. Watu tunaoandamana ap kwa pamoja barabara ni akina nani?
  5. Je Watu tunaoandamana ap kwa pamoja wanahusisha wale walio nje ya mipaka ya kanisa?
  6. Ni watu au makundi gani yameachwa pembeni, kwa uwazi au kwa hakika?
Maswali kuhusu Utamduni wa kusikiliza

Kwa kuzingatia kwamba, kusikiliza ni hatua ya kwanza, lakini inahitaji kuwa na akili na moyo wazi, bila chuki:

  1. Je, Kanisa letu “linahitaji kumsikiliza nani”?
  2. Je, Walei, hasa vijana na wanawake, wanasikilizwa vipi?
  3. Je, tunaunganishaje mchango wa Wanaume na Wanawake Waliowekwa wakfu?
  4. Je, kuna nafasi gani kwa sauti ya walio wachache, waliotupwa na waliotengwa?
  5. Je, tunatambua chuki na fikra potofu zinazozuia usikilizaji wetu?
  6. Je, tunayasikilizaje mazingira ya kijamii na kitamaduni yanayotuzunguka?
Maswali kuhusu Utamaduni wa kuzungumza

Kwa kuzingatia kwamba, wote wanaalikwa kuzungumza kwa ujasiri na kwa kuunganisha uhuru, ukweli, na upendo:

  1. Tunakuzaje mtindo huru na wa kweli wa mawasiliano ndani ya jumuiya na mashirika yake, bila undumilakuwili na ukinyonga?
  2. Tunakuzaje mtindo huru na wa kweli wa mawasiliano katika jamii ambayo sisi ni sehemu yake?
  3. Ni lini na jinsi gani tunaweza kusema yaliyo muhimu kwetu?
  4. Je, uhusiano na mfumo wa vyombo vya habari (sio vyombo vya habari vya Kikatoliki pekee) hufanya kazi vipi?
  5. Ni nani wanaozungumza kwa niaba ya jumuiya ya Kikristo, na wanachaguliwa jinsi gani?
Maswali kuhusu Kuadhimisha Ekaristi

Kwa kuzingatia kwamba, "kusafiri pamoja" kunawezekana tu ikiwa kunategemea kusikiliza Neno la jumuiya na adhimisho la Ekaristi:

  1. Je, sala na maadhimisho ya kiliturujia hututia moyo na kuelekezaje “kusafiri pamoja”?
  2. Je, sala na maadhimisho ya kiliturujia yanahimizaje maamuzi muhimu Zaidi miongoniwetu?
  3. Je, tunakuzaje ushiriki hai wa Waamini wote katika liturujia na utendaji wa kazi ya kutakatifuza ulimwengu?
  4. Je, ni nafasi gani zinatolewa kwa ajili ya watoa huduma za usomaji wa masomo Kanisani?
Maswali kuhusu Kuwajibika kwa pamoja katika utume

Kwa kuzingatia kwamba, sinodi iko katika huduma ya utume wa Kanisa, ambapo washiriki wake wote wameitwa kushiriki, kwa vile sisi sote ni wanafunzi wa kimisionari:

  1. Ni kwa jinsi gani kila mtu aliyebatizwa anaitwa kuwa mhusika mkuu katika utume?
  2. Je, jumuiya inaunga mkono vipi wanachama wake waliojitolea kutumikia katika jamii (jitihada za kijamii na kisiasa, katika utafiti na mafundisho ya kisayansi, katika kukuza haki ya kijamii, katika ulinzi wa haki za binadamu, na katika kutunza Nyumba ya Pamoja, n.k.) ?
  3. Je, unawasaidiaje kuishi ahadi hizi katika mantiki ya utume?
  4. Je, utambuzi kuhusu maamuzi yanayohusiana na utume hufanywaje, na ni nani anayeshiriki katika hilo?
  5. Ni kwa jinsi gani mapokeo mbalimbali yanayounda urithi wa Makanisa mengi, hasa yale ya Mashariki, yanaunganishwa na kurekebishwa, kuhusiana na mtindo wa sinodi, kwa mtazamo wa ushuhuda mzuri wa Kikristo?
  6. Je, ushirikiano hufanyaje kazi katika maeneo ambako Makanisa tofauti yapo?
Maswali kuhusu Mazungumzo katika kanisa na jamii

Kwa kuzingatia kwamba, mazungumzo ni njia ya ustahimilivu inayojumuisha pia ukimya na mateso, lakini yenye uwezo wa kukusanya mang’amuzi ya watu na watu:

  1. Je, ni maeneo gani na njia gani za mazungumzo ndani ya Kanisa letu mahalia?
  2. Je, tofauti za maono, migogoro na matatizo yanatatuliwa vipi?
  3. Je, tunakuzaje ushirikiano na Dayosisi jirani, pamoja na miongoni mwa jumuiya za kidini katika eneo hili, pamoja na miongoni mwa vyama na mienendo ya walei, n.k.?
  4. Je, ni uzoefu gani wa mazungumzo na ahadi ya pamoja tuliyo nayo na waumini wa dini nyingine na wasioamini?
  5. Je, Kanisa linajadiliana vipi na kujifunza kutoka sekta nyingine za jamii: ulimwengu wa siasa, uchumi, utamaduni, jumuiya za kiraia, maskini?
Maswali kuhusu Kushirikiana na madhehebu mengine ya Kikristo

Kwa kuzingatia kwamba, mazungumzo kati ya Wakristo wa maungamo mbalimbali, yaliyounganishwa na Ubatizo mmoja, yana nafasi ya pekee katika safari ya sinodi:

  1. Tuna uhusiano gani na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo?
  2. Je, ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo wanahusika na maeneo gani?
  3. Tumepata matunda gani kutokana na ‘kusafiri pamoja’ na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo?
  4. Kuna matatizo gani kutokana na ‘kusafiri pamoja’ na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo?
Maswali kuhusu Mamlaka na ushiriki

Kwa kuzingatia kwamba, Kanisa la Sinodi ni Kanisa shirikishi na linalowajibika pamoja:

  1. Tunatambuaje malengo ya kufuatwa, njia ya kuyatimiza, na hatua zinazopaswa kuchukuliwa?
  2. Je, mamlaka yanatekelezwaje ndani ya Kanisa letu mahalia?
  3. Je, ni kazi gani hufanyika kwa njia ya uwajibikaji wa Pamoja ndani ya kaniza mahalia?
  4. Je, huduma za walei na utekelezaji wa wajibu kwa Waamini walei hukuzwaje?
  5. Je, vyombo vya sinodi hufanya kazi vipi katika ngazi ya Kanisa mahalia?
  6. Je, vyombo vya sinodi ambavyo hufanya kazi katika ngazi ya Kanisa mahalia vinatoa ushuhuda wenye manufaa?
Maswali kuhusu Kutambua na kuamua

Kwa kuzingatia kwamba, kwa mtindo wa sinodi, maamuzi hufanywa kwa njia ya utambuzi, kulingana na maafikiano yanayotokana na utii wa kawaida kwa Roho:

  1. Je, kwa taratibu na mbinu gani tunatambua pamoja na kufanya maamuzi?
  2. Je, taratibu hizo zinaweza kuboreshwaje?
  3. Je, tunakuzaje ushiriki mpana katika kufanya maamuzi ndani ya jumuiya zenye uongozi ulio na muundo wa hierakia?
  4. Je, tunaelezaje uhalali wa mfumo wa maamuzi ndani nya Kanisa unaotenganisha awamu ya walei kutoa ushauri kwa makleri na awamu ya makleri kufanya maamuzi?
  5. Je, ni kwa jinsi gani na kwa zana zipi tunakuza uwazi na uwajibikaji katika mfumo wa maamuzi ndani nya Kanisa unaotenganisha awamu ya walei kutoa ushauri kwa makleri na awamu ya makleri kufanya maamuzi?
Maswali kuhusu Kujiunda katika sinodi

Kwa kuzingatia kwamba, hali ya kiroho ya kusafiri pamoja inaitwa kuwa kanuni ya kielimu kwa ajili ya malezi ya utu wa kibinadamu na ya Mkristo, ya familia na jumuiya:

  1. Je, tunaundaje watu, hasa wale wanaoshikilia majukumu ndani ya jumuiya ya Kikristo, ili kuwafanya wawe na uwezo zaidi wa “kusafiri pamoja,” : kusikilizana na kushiriki katika mazungumzo?
  2. Je, ni malezi gani tunayotoa kwa ajili ya utambuzi na utumiaji wa mamlaka?
  3. Ni zana gani hutusaidia kusoma mienendo ya utamaduni ambamo tumezama na athari zake kwa mtindo wetu wa Kanisa?
Mwongozo kwa ajili ya kujaza dodoso

Katika mchakato wa tafakari na ushiriki wenye kuchochewa na swali la msingi, waumini wanaalikwa kuzingatia miongozo sita ifuatayo:

1. Jiulizeni ni matukio gani katika Kanisa lenu swali la msingi linawakumbusha;

2. Soma tena matukio haya yaliyoonwa kwa kina zaidi kwa kujiuliza:

  • Yameleta shangwe gani?
  • Je, yameleta magumu na vikwazo gani?
  • Yameleta majeraha gani?
  • Je, yametoa maarifa gani?
3. Orodhesha mafanikio ili kushirikisha wengine kwa kujiuliza haya:
  • Ni wapi, katika matukio haya, sauti ya Roho Mtakatifu inasikika?
  • Roho Mtakatifu anatuomba nini?
  • Ni mambo gani yanahitaji kuthibitishwa, mabadiliko yanayohitajika, na hatua za kuchukuliwa ili kuleta mabadiliko hayo?
  • Tunakubaliana katika masuala yapi na wapi hatukubaliani?
  • Ni njia zipi zinafunguliwa na Kanisa letu mahalia kwa ajili ya kutafuta mwafaka mpana?
4. Katika kusoma tena uzoefu, ni muhimu kukumbuka kwamba "kusafiri pamoja" kunaweza kueleweka kwa njia ya mitazamo miwili tofauti, ambayo inahusiana sana.

Mtazamo wa kwanza wa “kusafiri pamoja” unatazama maisha ya ndani ya Makanisa mahalia, mahusiano kati ya Waamini, Wachungaji wao na jumuiya ambazo wamegawanyika, hasa maparokia.

Kisha mtazamo huu unazingatia mahusiano kati ya Maaskofu na Askofu wa Roma, pia kwa njia ya Sinodi za Maaskofu wa Makanisa ya Patriaki na Makuu ya Jimbo kuu, Mabaraza ya Viongozi wa Makanisa na Mabaraza ya Mabaraza ya Makanisa, na Mabaraza ya Maaskofu, katika sura ya kitaifa, kimataifa na kibara.

Kisha mtazamo huu unagusia njia ambazo kila Kanisa linajumuisha ndani yake mchango wa aina mbalimbali za maisha ya kimonaki, ya kidini, na ya kuwekwa wakfu, ya vyama vya walei na mienendo, ya taasisi za kikanisa na kikanisa kama vile shule, hospitali, vyuo vikuu, misingi; mashirika ya hisani na msaada, n.k.

Hatimaye, mtazamo huu pia unajumuisha mahusiano na mipango ya pamoja na ndugu na dada wa madhehebu mengine ya Kikristo, ambao tunashiriki zawadi ya Ubatizo huo.

5. Mtazamo wa pili wa “kusafiri pamoja” unazingatia jinsi Watu wa Mungu wanavyosafiri pamoja na familia nzima ya wanadamu.

Kwa hivyo, macho yetu yatazingatia hali ya mahusiano, mazungumzo, na mipango inayowezekana ya pamoja na waumini wa dini zingine, na watu walio mbali na imani, na mazingira maalum ya kijamii na vikundi, na taasisi zao katika sekta anwai za ulimwengu wa maisha ya watu.

Yaani, ulimwengu wa siasa, utamaduni, uchumi, fedha, kazi, vyama vya wafanyakazi, na vyama vya biashara, mashirika yasiyo ya kiserikali na ya kiraia, vuguvugu la watu wengi, walio wachache wa aina mbalimbali, maskini na waliotengwa, n.k.

6. Kumbuka kwamba kuna ngazi tatu za kimantiki ambamo sinodi inatekelezwa kama chombo muhimu cha Kanisa.

(i) Kuna ngazi ya mtindo ambao Kanisa huishi na kufanya kazi nao, unaodhihirisha asili yake kama Watu wa Mungu wanaosafiri pamoja na kukusanyika katika kusanyiko lililoitwa na Bwana Yesu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kutangaza Injili.

Mtindo huu unatambulika kwa njia ya “jamii kusikiliza Neno na kuadhimisha Ekaristi, udugu wa komunyo na uwajibikaji na ushiriki wa Watu wote wa Mungu katika maisha na utume wake, katika ngazi zote na kupambanua huduma na majukumu mbalimbali. ;”

(ii) Kuna ngazi ya miundo na taratibu za kikanisa, kama inavyoamuliwa kutokana na mtazamo wa kitheolojia na kisheria, ambamo asili ya sinodi ya Kanisa inaonyeshwa kwa njia ya kitaasisi katika ngazi ya mtaa, kikanda, na ya ulimwengu wote;

(iii) Na kuna ngazi ya michakato ya sinodi na matukio ambamo Kanisa linaitishwa na mamlaka husika, kulingana na taratibu maalum zinazoamuliwa na nidhamu ya kikanisa.

Kwa ujumla, ingawa, kwa mtazamo wa kimantiki, ngazi hizi tatu ni tofauti, ngazi hizi zinarejelea moja hadi nyingine na lazima zishikane kwa Pamoja muda wote, vinginevyo ushuhuda wa kupingana utapitishwa, na uaminifu wa Kanisa utadhoofishwa.

Kwa kweli, ikiwa sinodi haijajumuishwa katika miundo na michakato, mtindo wa sinodi hushuka kwa urahisi kutoka kiwango cha nia na matamanio hadi kile cha balagha, wakati michakato na matukio, ikiwa havijahuishwa kwa njia ya mtindo mahususi, hugeuka kuwa taratibu tupu zisizo na maana yoyote.

1640632596038.png

Picha ya Papa Francis wakati wa uzinduzi wa Sinodi huko Vatican
 

Askofu Mkuu Jude Thadeus Ruwaichi, wa JImbo Kuu la Dar es Salaam, akitoa homilia

Usuli

Ifuatayo ni homilia ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam Mhasham JudeThaddeus Ruwai'chi kweny Ibada ya Misa takatifu ya Uzinduzi wa Sinodi ya Maaskofu, Ibada ambayo ilifanyika katika viwanja vya Msimbazi centre Jimbo kuu la DSM, tarehe 17 Oktoba 2021.

"Napenda niseme kwa kusisitiza, katika mwendo wa sinodi hakuna tofauti kati ya Askofu, Padre, Mtawa, Mlei. Wote mtashiriki kwa usawa kama wana Kanisa, na kama wafuasi na wajumbe wa Kristo," anasema Askofu Mkuu Jude Thadeus Ruwaichi. Endelea kujisomea ...

Homilia yenyewe

Nudugu zangu, Sinodi tunayozindua leo, ni safari ya miaka mitatu.

Safari inayoanza mwmezi huu wa kumi mwaka 2021, na ambayo itafikia kilele chake mwezi wa kumi mwaka 2023.

Katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kama mlivyoelezwa katika utangulizi aliotoa Baba Askofu Mshemba, tumeishaanza kwa kuunda jopo la kuhamasisha, tumeishaanza kwa kutoa semina katika dekania zote 12.

Kwa hiyo, mnalo wazo kuhusu sinodi. Kuna wanaonipelekea meseji wakiuliza maswali kama, “Hivi kwa nini sinodi ya maaskofu?”

Ndugu zangu, hilo sitalijibu leo. Maanake, jopo la sinodi litaendelea kufanya kazi kati yen una Pamoja nanyi likijibu maswali yenu, likichukua mawazo yenu, likipokea ushiriki wenu katika mwendo wa sinodi.

Mwaliko wangu kwa kila mwana Dar es Salaam, Baba, Mama, mzee, kijana, mtoto, yeyote mwenye changamoto ya Maisha au ya kivile, kila mmoja ajisikie kwamba hii ni fursa yake ya kushiriki ipasavyo katika kuchangia mawazo kuhusu Kanisa na utume wake.

Nawaombeni msiogope, msijifiche, na msiache kutumia fursa hii.

Napenda niseme kwa kusisitiza, katika mwendo wa sinodi hakuna tofauti kati ya Askofu, Padre, Mtawa, Mlei. Wote mtashiriki kwa usawa kama wana Kanisa, na kama wafuasi na wajumbe wa Kristo.

Kwa hiyo, tambua fursa yako. Msikilize Roho Mtakatifu, na twambie yale ambayo unadhani Roho Mtakatifu anakutuma katika ukweli, katika unyofu, katika uadilifu, ulishirikishe Kanisa.

Na unaposhirikisha shirikisha kwa unyofu, shirikisha kwa unyeyekevu. Usishirikishe kama mtu ambaye ndiye peke yako tu umepewa ukweli wote. Maana wapo na watu wa hivyo hivo pia.

Ukidhani kwamba ni wewe tu unapewa ufunuo unaweza kusema sasa mimi nimefunuliwa hivi, kwa hiyo nawaagiza fanyeni vile. Hapana. Sema kile ambacho roho anakutuma useme katika unyofu, katika ukweli, katika unyenyekevu na katika Imani safi na Takatifu ya KIkatoliki.


Nyongeza ya mwandishi

Tayari Jimbo Kuu la Dar es Salaam limeandaa maswali ya dodoso na kuyasambaza kwa waumini kupitia parokia na Jumuiya Ndogo Ndogo ili kukusanya mawazo yao juu ya Kanisa. Mwaswali hayo ni kama ifuatavyo:

View attachment 2060346
Picha ya Papa Francis wakati wa uzinduzi wa Sinodi huko Vatican
Wenye akili wameshausoma.upepo na kuona kuna uturn inatakiwa kufanyika.

Hongereni Katoliki kwa kuanza kujitazama kutokea ndani.

Maoni na maoni ya waumini yatasaidia kuujenga mwili wa Kristo.

Neno la Mungu ni Taa daima
 
Wenye akili wameshausoma.upepo na kuona kuna uturn inatakiwa kufanyika.

Hongereni Katoliki kwa kuanza kujitazama kutokea ndani.

Maoni na maoni ya waumini yatasaidia kuujenga mwili wa Kristo.

Neno la Mungu ni Taa daima
Nikupinge au niache fujo..?
 
Wenye akili wameshausoma.upepo na kuona kuna uturn inatakiwa kufanyika.

Hongereni Katoliki kwa kuanza kujitazama kutokea ndani.

Maoni na maoni ya waumini yatasaidia kuujenga mwili wa Kristo.

Neno la Mungu ni Taa daima
HIYO U TURN HAITAHARIBU MISINGI YA KANISA KATOLIKI LAKINI...
 
Kuna Chochote nyuma ya matembezi hayo..?
YEAH KAMA NI MUELEWA ILA KAMA NI MBISHI HUTAELEWA

NGOJA NIKUPE UZI WA MAREJEO USOME UELEWE

 
YEAH KAMA NI MUELEWA ILA KAMA NI MBISHI HUTAELEWA

NGOJA NIKUPE UZI WA MAREJEO USOME UELEWE

Nishaelewa mkuu toka huko juu ulivyoandika kwa maherufi makubwa! Sema nina vurugu tu..😂
 
Back
Top Bottom