Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi Arumeru (CHADEMA)

Sijapata ona uzinduzi wa kisayansi kama huu nchi hii,hakuna tusi wala kashfa ya uongo.Na kama wakati umefika wafanya biashara kusimama hadharani na kuchangia upinzani bila woga basi mjue hofu na dola imekwisha
 
Nashukuruni sana kwa aliyetupa link ya kusikia matangazo ya moja kwa moja, niko mbali sana ya Arusha lakini nimesikiliza hotuba zote. Hii imetulia na naamini CHADEMA wanaendelea vizuri.
 
dubu. Mgombea wa Zccm ametoboa sikio maans yake ni nini?.

yaani ni kwamba mgombea wa ccm katoga sikio, so wanasema ni muhuni hafai kuwa mbunge wa watu wastarabu kama wameru so wasimchague.
 
Nimefurahi ujumbe wa M/kiti kuwa mbunge mmoja wa CDM ni sawa na wabunge 30 wa magamba,hapa mwenyekiti alitaka kuwalindia heshima tu,mbunge mmoja wa CDM ni sawa na wabunge wote 250 sijui..anasema wabunge wa CCM ni wepesi munoooooo!!!
 
dubu unatisha mkuu'umenifanya nitulie hapa muda mrefu bila kuondoka'unaonaje idadi ya watu na mwitikio hasa wakati Kamanda Mbowe anaongea?
 
Yanga 1, AZAM 3


Mkuu yani Yanga wameharibu furaha yangu leo....nilikuwa nakula hotuba za m/kiti nafurahi huku Yanga wapuuzi wanaharibu..ila refa kapewa kichapo kwa ajili ya ujinga wake wa kuwapendelea Azam na hiyo ikasababisha wachezaji muhimu Cannavaro na Frabregas aka Haruna kutolewa kwa kadi...Yanga imecheza zaidi ya dk 70 wakiwa pungufu...ILA CHADEMA wamenikosha,furaha ya CHADEMA imekosha moyo wangu.
 
dubu unatisha mkuu'umenifanya nitulie hapa muda mrefu bila kuondoka'unaonaje idadi ya watu na mwitikio hasa wakati Kamanda Mbowe anaongea?

pamoja na jua lilokuwa linawaka hakika watu walikuwa wengi sana. watu walitulia, wale wa mbele walikaa na wanyuma kusimama huku wengine wakiwa juu ya majumba na juu ya miti.
 
Najua magamba wamekasirika kwasababu ya lile nyomi...sasa maroli na mabasi yatafanya kazi J3 tutegemee nyomi la kuundwa(artificial nyomi) la CCM siku ya J3.Na nahisi CCM walikuwa wanataka kuona CDM tutakavyo lianzisha...ili waje na watu wao wanaowabeba kwa malori na kuwalisha wali maharage.Na napenda niwaambie watanzania na nyie watu mlio na ndugu wanaobebwa kwenda kwenye mikutano ya CCM lile ni tusi kubwa sana kwao..ni kama wanawaambia umaskini wenu mtaji wetu..kataa hii mtanzania.
 
Hongera Dubu, nilipo ni mbali sana sana, lakini ulicholeta kimenisogeza kama niko huko Arumeru..asante sana!Vipi, hapakuwa na utumbuizaji kama wa comedy i.e kina masanja, wafanyavyo ccm?
 
..nimeanza kusikiliza wakati wa hotuba ya Mbowe.

..samahani lakini naona kama ilikuwa imekosa maandalizi.

..halafu hotuba yake sikuipenda na zaidi ilinichosha.

..binafsi sipendi kusikia MUNGU akitajwa, tena mara nyingi, katika mikutano ya kisiasa.

..zaidi, ingependaza kama Joshua Nassari, mgombea ubunge, angepewa muda mrefu zaidi kuzungumza.

..hata Nassari naye hotuba yake ilikuwa ya kulipua-lipua tu.

..hili ilikuwa ni nafasi ya kipekee kwa Nassari kuwapa wananchi wa Arumeru sababu za kwenda kumpigia kura.

..sote tujiulize, wananchi waliohudhuria mkutano ule wameondoka na kitu gani cha kuwahasisha na kuwasimulia wenzao waliokosa kuhudhuria mkutano ule kiasi kwamba siku ya uchaguzi wataacha shughuli zao na kwenda kumpa kura Joshua Nassari?

NB:

..the +ve thing ni kwamba muda wa kujirekebisha bado upo.
 
Back
Top Bottom