..nimeanza kusikiliza wakati wa hotuba ya Mbowe.
..samahani lakini naona kama ilikuwa imekosa maandalizi.
..halafu hotuba yake sikuipenda na zaidi ilinichosha.
..binafsi sipendi kusikia MUNGU akitajwa, tena mara nyingi, katika mikutano ya kisiasa.
..zaidi, ingependaza kama Joshua Nassari, mgombea ubunge, angepewa muda mrefu zaidi kuzungumza.
..hata Nassari naye hotuba yake ilikuwa ya kulipua-lipua tu.
..hili ilikuwa ni nafasi ya kipekee kwa Nassari kuwapa wananchi wa Arumeru sababu za kwenda kumpigia kura.
..sote tujiulize, wananchi waliohudhuria mkutano ule wameondoka na kitu gani cha kuwahasisha na kuwasimulia wenzao waliokosa kuhudhuria mkutano ule kiasi kwamba siku ya uchaguzi wataacha shughuli zao na kwenda kumpa kura Joshua Nassari?
NB:
..the +ve thing ni kwamba muda wa kujirekebisha bado upo.