Unaukanda mpaka ukiunyanyua unabebeka wote kwenye kikandio usinate, kama unakandia kidish mpaka kibaki kisafi kabisa kama kimeoshwa na mkono ubaki msafi hapo ndio unakuwa umelainika.
Usiweke maji mengi sana ukawa laini utasumbua na wala usiwe mgumu sana. Kwa kg 1 mm huwa naweka vikombe viwili vya maji/maziwa ( vikombe vya chai vingi kipimo kinafanana).
Ingredients mikate haina mbwembwe ni maji, mafuta, amira na chumvi tuu. Ila kunogesha kandia maziwa, weka na vanila kidogo unaweza weka yai pia.
Vanilla inaongeza radha na harufu nzuri.