Uzi wa vyakula tu

Njaanuary..nyama hadi March katikati hapoView attachment 1672800
Huu Mlo wako nimeutamani kupita maelezo.


2662280_IMG_20210109_134916_972.jpg
 
Bila shaka bila shaka.

Simply nunua maziwa fresh ya ngombe ambayo hayajatiwa maji, chuja katika sufuria chemsha na yaache yapoe. Ukihakikisha yamepoa kabisa chuja katika bakuli safi then tia chachu, (chachu yaweza kuwa maziwa ya mtindi uliyonunua ya pakti, au hamira kidogo sana), then yaache bila kuyagusa/tikisa/sumbua labda kwa usiku mzima. Kesho ukiyaangalia unakuta yameshakua mtindi mzuri kabisa. Then unaweza badili chombo au kuweka katika fridge tayari kwa kuliwa.

Wengine katika kuchachua huwa waweki chochote wanayaacha yalale hivyo hivyo yataanza kuganda na kutengeneza mtindi yenyewe, sijui kwa wao lakini kwa mimi huwa naona yanatengeneza kaharufu fulani hivi kabaya. Kwahiyo njia yangu ya kuyachachua ni kuweka mtindi ule wa pakti kidogo tu kama robo kikombe. Same as hamira pia ukitumia italeta kiharufu fulani.

NB: 1. Kuwa na vyombo viwili maalumu kwaajili ya maziwa tu, kimoja gandishia, asubuhi yakishaganda hamisha kwenye chombo kingine, kile cha mwanzo osha kausha subiri routine nyingine utaanza nacho. Mzunguko unakua huo huo, isipite siku mbili bila kubadili na kuosha chombo chako.

2. Harufu husabishwa na uchafu wa chombo cha maziwa, au maziwa yalianza kugandishwa yakiwa bado ya uvuguvugu.
Una roho nzuri sana mkuu wa kutoa msaada wa recipe kama mtu akikuomba endelea na moyo huo huo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom