Uzi maalum wa kushare habari mbalimbali kuhusu ushamba kwenye vitu mbalimbali

Black poison The Factor

JF-Expert Member
May 31, 2020
1,048
1,526
Mimi vitu vya kishamba ambavyo nimewahi kuviona ni kama ifuatavyo.

1. Hii ilikua kipindi Cha redio za cassette msukuma ameweka Kanda na amenyanyua antenna kana kwamba anasikiliza radio stations.

2. Mzee mmoja alipeleka radio kwa fundi ili apate radio taifa (tbc) maana zilikua zinasikika radio za kimataifa tu. Akahisi ni mbovu. Kumbe alibadilisha masafa tu

3.Hii inanihusu Mimi niliambiwa nikazime radio (cassette) Sasa badala nizime nikatoa sauti ikabaki vile ile mpaka jioni battery zikaisha nilitukanwa mbaya kabisa.

4. Kuna msukuma alinunua simu sasa akawa hajui kutumia, baada ya muda akapigiwa mwenzake akamwambia pokea simu inaita.

Yeye akaichukua akaweka mfukoni, mwenzake akamwambia mbona hujapokea akasema si nimepokea nimeweka mfukoni.

Akamwambia pokea muongee akaitoa mfukoni akasema aloo bila kupokea aisee tulicheka mbaya kabisa.

4. Hii ni Mimi tena nilikuaga sielewi namna ya kuchati nilikuaga naona tu baba anasoma ikabidi nimuulize, alinicheka sana alafu akanifundisha kwenye simu yake, mi nilikua bado mdogo.

5. Tunarudi kwenye cassette tena ilikua mtu akiweka Kanda ikifika mwisho anaitupa anafikiri imeisha kumbe ni kugeuza tu upande wa pili.

6. Mara yangu ya kwanza kuona mtu akiongea kilugha kwenye simu nikajua wametengeneza za kuongea kilugha tu. Na za kiswahili ni tofauti pia ni mengi sana wadau, nanyie leteni visa vyenu
 
Basi, haya ya kichina lilisimama njiani kupakia abiria fulani, mlango ulipofunguliwa yule abiria akawa anakomaa kuingilia kule ulikofungukia, sio pale tunapopita wote. Amepambana sana apenye pale, sikumuelewa. Mpwapwa Dodoma huko kwenye barabara za vumbi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom