Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Barcelona ina matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ataamua kutotia saini kandarasi mpya na Man United , ijapokuwa watakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu za PSG , Juventus na Real Madrid . (Fichajes - in Spanish)
 
Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner ,25, ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaonyatiwa na Borussia Dortmund iwapo mshambuliaji matata wa klabu hiyo Erling Braut Halaand ataondoka katika klabu hiyo msimu ujao.(SportBild - in German)
 
Kandarasi ya beki wa Ujerumani Antonio Rudiger katika klabu ya Chelsea inakamilika msimu ujao na mazungumzo ya kuiongeza yamegonga mwamba. (Times - subscription required)
 
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anatarajiwa kumkuza kiungo wa kati wa timu ya wachezaji chipukizi katika klabu hiyo Charlie Patino katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku kukiwa na ripoti kwamba klabu ya Barcelona inamnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 wa England.. (Mirror)
 
Mmiliki wa klabu ya Fiorentina Rocco Commisso hajui iwapo mshambuliaji wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 Dusan Vlahovic , ambaye amehusishwa na klabu ya Manchester City , Atletico Madrid na Juventus , ataongeza mkataba wake zaidi ya mwezi juni 2023 na klabu hiyo ya Itali. (Calciomercato, via Goal)
 
FB_IMG_1631876661091.jpg
 
Back
Top Bottom