Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

bfaf75a6b43f893eb2522aeda466f302.jpg
 
Massata ni mfanyabiashara jijini Dakar, mji mkuu wa taifa la Senegal. Anasema kuwa alianza kufanya mazoezi ili kuboresha hali yake ya afya. Uamuzi huo umebadilisha maisha yake. Anasema kuwa, miaka sita iliyopita alikumbwa na ugonjwa. Ugonjwa huo huathiri maini. "Nilikuwa nahisi maumivu mgongoni." Anasema Massata, huku akiwa ametulia.
 
Ugonjwa aliokuwa akiugua ni kuwa ini huzungukwa na mafuta. Mara nyingi watu wenye ugonjwa huo, huwa hawaoneshi dalili zozote.

Hadi kufikia sasa hakuna dawa au matibabu ambayo yamethibitishwa kuponya ugonjwa wenyewe. Hata hivyo mabadiliko ya tabia ya kula pamoja na mazoezi ya mara kwa mara ni dawa mjaarabu kwa mujibu wa matabibu.
 
Kabla nianze kufanya mazoezi, nilikuwa na uzani wa kilo 86, lakini sasa uzani wangu ni kilo 76. Mazoezi yalinasaidia kupoteza kilo 10 kwa kipindi cha miezi mitatu." Massata anasema huku akionekana akiridhishwa na hali yake sasa.

Anaafiki kuwa mazoezi yana nafasi kubwa sana maishani mwake sasa. Zamani hakuwa na muda alioutenga kwa ajili ya mazoezi lakini sasa anasema, "mimi hufanya mazoezi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
 
Tangu agundue umuhimu wa kufanya mazoezi, Massata, hajawahi kuwa mvivu katika maisha mapya aliyoanza kuyaishi. "Hapa huwa ninakuja kufanya mazoezi kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, isipokuwa mwishoni mwa juma. Misuli inahitaji kupumzika ili ikue." Massata ananifahamisha huku akiwa kwenye eneo ambalo hufanyia mazoezi akiwa na nguo za mazoezi.
 
Kisha kocha wake anafika huku akiwa mwingi wa tabasamu, "wakati mwingine sikumuona akija kufanya mazoezi. Ukweli ni kuwa alikuwa anatibiwa hospitalini. Aliporejea mazoezini aliniambia alikuwa ana furaha kubwa." Lamine anasema, kisha anaendelea kuzungumza, "nilimuuliza, nini kilichofanyika?"
 
Back
Top Bottom