Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tafiti zimeonesha kwamba ulezi na mtama viliweza kuboresha afya ya moyo na mishipa ya damu kwa kupunguza mafuta mabaya ‘triglycerides’ kwa panya waliotumika kwenye majaribio. Mmh! Vipi kama haitokei kwa binadamu?
 
Kuna utafiti mwingine ulifanyika China, ulionesha kwamba kadri watu walivyokula jamii ya mtama hatari ya kufa kwa saratani ya koo ilipungua kadri mtu alivyokula zaidi. Hii ilifanyika kwa kulinganisha na watu ambao wanakula mahindi na ngano.
 
Wanasayansi wengine walieleza kuwa, shida ya mahindi na ngano huenda ni kwa sababu ya fangasi wanaoitwa fusaria C, ambao wanaweza kusababisha saratani, huwa wanapatikana kwenye mahindi yaliyotunzwa nyumbani kwa mazingira ya China (chang et al, 1985) na South Afrika (Marasasi et al, 1979) hatujui hapa kwetu haijafanyiwa utafiti.
 
Peroxidase ambayo ipo kwenye maganda ya jamii za mtama inasaidia kuzuia seli za saratani zisisambae kwenda sehemu nyingine ya mwili
 
Back
Top Bottom