Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fanya Manunuzi Katika Tovuti Salama Tu



Kabla ya kuingiza taarifa zako za kadi ya benki au miamala ya simu, hakikisha umekagua kuwa tovuti unayoitumia kufanya manunuzi yako ni halali na ina ulinzi. Njia rahisi ya kutambua hili ni kwa kuangalia alama ya ‘https’ mwanzo wa anuani ya tovuti hiyo.
 
Kama hiyo tovuti haina alama ya ‘s’ baada ya ‘http’ basi jua kuwa tovuti hiyo haijahakikiwa na si salama kuingiza taarifa za miamala yako ya kifedha. Tovuti za mitandao yote lazima iwe na ‘s’, kifupi cha neno ‘secured’ mwishoni mwa anuani ya tovuti hiyo. Mfano tazama namna ya tovuti salama na ambayo sio salama itakavyoonekana.

https://www.jinalatovuti.com (tovuti hii ni salama)
http://www.jinalatovuti.com (tovuti hii si salama). Haina ‘s’ baada ya neno http
 
Mfahamu Muuzaji na Hadhi Yake

Kama tayari unafahamu duka la bidhaa unazozipenda, basi kufanya malipo katika tovuti yao ili kununulia mtandaoni sio shida sana. Ni rahisi kwenda moja kwa moja katika duka lao endapo shida yeyote itatokea.
 
Mfano, unajua kabisa duka fulani la kuuza saa lipo Mlimani City, na pia wana website inayotambulika. Hivyo unaweza kufanya malipo mtandaoni kwa uhakika kwani unajua kabisa lolote likiwa ndivyo sivyo basi ni rahisi kwenda kuripoti dukani kwao.
 
Epuka Kutumia Internet ya Umma (Public Wi-Fi) Kufanya Manunuzi



Wote tunazijua hizi. Unafika sehemu, mfano Viwanja vya Ndege au baadhi ya Migahawa. Unakuta wameweka alama ya ‘Free Wi-Fi’ au ‘Internet ya Bure Hapa’. Hizi zinakua sawa kama unaperuzi mtandaoni au kuangalia video. Lakini si salama kuingiza nyaraka zako za siri mfano taarifa za kifedha.
 
Mara zote unapoingiza taarifa binafsi katika ‘Internet za bure’ basi unafungua mlango kwa wezi wa mtandaoni. Intaneti nyingi za bure huwa hazijaandaliwa kulinda taarifa zako (unencrypted), hivyo wezi wanaweza kukuibia kirahisi ikiwa watajiunga kwenye Internet ya bure kama wewe.
 
Kuwa Mjanja Dhidi ya Apps za Manunuzi



Apps za manunuzi zinafanya mambo kuwa rahisi sana, ikiwemo pia kuibiwa. Ukiwa na App, unapata urahisi wa kuperuzi na kufanya maamuzi ya kulipia n.k. Lakini pia, App zinatengenezwa kwa namna ambao ni rahisi kuiba taarifa zako na za kwenye simu yako. Mara zote hakikisha unapakua (download) App zako kutoka katika vyanzo vya kuaminika, mfano Google PlayStore na Apple App Store.
 
Weka umakini pia wakati wa kuruhusu App hiyo kufanya baadhi ya vitu. Kama ukiona kitu hakileti maana, mfano App inaomba ku’access’ orodha ya namba zako za simu, lazima uwe makini. . Pia soma maoni (reviews) yanayotolea na watumiaji wengine kabla ya kuhifadhi App hiyo katika simu yako.
 
Back
Top Bottom