Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usijiachilie sana na kuwa wazi sana kwa mtu huyu. Sio eti kila unachosikia au kuwanacho moyoni ndiyo yeye wa kwanza kuitwa na kuambiwa. Sio eti siri unayoiona ina mhitaji mtu wako wa karibu ndiye yeye unampigia simu akushauri na unamfunulia moyo wako. Chunga sana, unaweza kujikuta unamwalika joka ndani ya uvungu wako
 
Pima ushauri wake na ikiwezekana uliza mtu mwingine pia. Sisemi kwamba ukatae kila anachokushauri, lakini maadam kuna taa nyekundu imeshaanza kukuwaka ndani ya moyo wako kuhusu yeye, basi kila ushauri akupao usiuchukue mzimamzima na kuuweka kwenye matendo, tafuta mtu wa pili au watatu mweleze uone kama majibu au ushauri unaoupata kwingine unalandana na ule aliokupa yule rafiki umhofuye.
 

Dr Benson Bagonza (Bishop)

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
Bangoza ni haki yake kuongea alichoongea, nami/nasi ni haki yangu/yetu kumshangaa profesa anayejipuuza mpaka akapuuzwa, kisa? Mshahara? .Uprofesa ameutoa thamani mbele ya wajinga
 
Back
Top Bottom