Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaposikia au unapogundua kuwa rafiki yako anakusema vibaya kwa wengine wakati anapokuwa na wewe anajifanya malaika. Labda mmezoea kuongea mengi pamoja lakini baadaye unakuja kugundua yote hayo mliyokuwa mnaongea yeye anaongea kinyume akiwa na wengine na labda sio tu anaongea kinyume, yamkini anakupinga na hata kusema vibaya kuhusu wewe.
 
Unapohisi au unapogundua rafiki yako anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani. Yamkini kuna mambo mnafanya kwenye ushirikiano wenu, tena mnafanya ukijua mnapendana, lakini kuna wakati unaona vijidalili vya kukuonyesha kuwa huyu unayedhania ni rafiki yako mara kwa mara hakubaliani na badhi ya vitu unavyoviwaza au kuvipendekeza na zaidi ya hapo kuna hali ya kukuonea wivu kwenye baadhi ya vitu kwenye maisha yako.
 
Upohisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako. Inatokea kuna vitu mnavipanga au kuviongelea katika miradi au mikakati ya kimaisha, lakini katika hali zote mnazohusiana kwazo unakuja kugundua anapenyeza kwa wazi au kwa sirisiri kiu yake ya kupata zaidi yako, kiu yake ya kukushinda, kiu yake ya kukuongoza, kiu yake ya kuwa mbele zaidi yako.
 
Kwa mfano mnataka kufungua kampuni, labda lilikuwa wazo lako lakini yeye anafanya juu chini awe kiongozi, au mtu wa kusimamia fedha. Labda mnampango wa kukutana na watu fulani wa muhimu katika mikakati fulani, ghafla anakwambia ameshaonana nao na wameongea bila hata wewe kujua, ukimuuliza anakwambia alihisi wewe utakuwa umebanwa akaamua kufanya ili aje kukupa taarifa. Hali hii sio ya kutaka kukusaidia bali kukufunika. Nia yake hii niyauovu kabisa. Kuwa macho sana.
 
Unapohisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni. Mara nyingine unaona wazi kuwa anakushauri, tena ushauri mzuri, ukidhani nia yake ni kuona unapenya kwenye maisha, hii ni kwasababu haujafungua macho yako vema, kila unapofuata ushauri wake mambo hayaendi.
 
Anakushauri kitu, kesho au keshokutwa biashara yako inashindwa na inakufa ghafla unaona mazingira ya yeye kuwachukua wateja wako au kulichukua soko lako. Wakati haya yanapokuja kutokea yeye haumpati tena na ukimpata na kumuuliza anaweza kukwambia kuwa yeye hakuwa na nia mbaya. Fahamu kwamba huyu alikuwa adui tokea muda sana sema wewe hukuwa macho vya kutosha.
 
Back
Top Bottom