Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

567df4322e3a187d45be3b2b14229522.jpeg
 
Sharti la kwanza la Zidane ni kuhakikishiwa staa wa Chelsea, Eden Hazard atabakishwa klabuni hapo wakati huu ambao inasemekana amekata shauri kuondoka Stamford Bridge baada ya kuchoshwa na maisha ya klabu hiyo.
 
Hazard ni mmoja kati ya mastaa wanaowindwa na klabu ya zamani ya Zidane, Real Madrid na inadaiwa klabu hiyo imeandaa kitita cha Pauni 100 milioni kwa ajili ya kumtwaa staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, ambaye anaonekana kama mmoja kati ya watu ambao watapunguza maumivu ya Madrid kuondokewa na Cristiano Ronaldo katika dirisha kubwa la mwaka jana.
 
Zidane pia ametoa sharti la tatu ambalo ni kuachiwa maamuzi ya manunuzi na mauzo ya wachezaji sambamba na Mkurugenzi wa ufundi wa sasa wa Chelsea, Marina Granovskaia ambaye kwa sasa ana kauli ya mwishoni klabuni hapo akiwa ameaminiwa na tajiri, Roman Abramovich.
 
Hata hivyo licha ya masharti hayo, Zidane anaamini Sarri bado anaweza kuendelea kuwa kocha wa Chelsea msimu ujao kama ataweza kurekebisha mambo ikiwemo kushinda pambano gumu la jana dhidi ya Manchester United michuano ya FA na pia kutwaa taji la Kombe la Ligi ambapo wanatazamiwa kucheza na City mwisho wa mwezi huu.
 
Mpaka sasa kwa mujibu wa Sarri, tajiri Abramovich hajawasiliana naye kufuatia kichapo cha aibu cha mabao 6-0 ambacho Chelsea walipokea wiki iliyopita kutoka kwa Manchester City ugenini lakini ni wazi kichapo hicho kimeanza kuashiria mwanzo wa mwisho wake Stamford Bridge.
 
Back
Top Bottom