Uzi Maalum Wa Kujadili Shule Mbali Mbali

Changamoto ni nyingi sana.
Zile gheto zilikuwa zinapangishwa watoto wa kike na wakiume.
Mfano wewe unajenga nyumba yako vyumba kama kumi halafu unawapangishia wanafunzi.
Sasa unakuta mlango huu ni ghetto la wadada na mlango unaofuata ni ghetto la wakaka.
Kutokana na uduni wa maisha pia ililazimu kila ghetto tuishi hadi watu wanne wanne.

Changamoto.
Nilivyofika form 1 (njuka) nilipata ghetto ambalo pembeni yake palikuwa ghetto la wakaka ambao walikuwa form 4. Daah changamoto niliyopata pale haihathiki yaani.

Changamoto nyingine ni kusulubiwa na wana kijijini. Aisee kile kijijini wanakijiji wanapiga kama wanaua nyoka yaani. Ukikutwa unaenda dukani usiku au umevaa nguo za kimjini, au kuchota maji usiku (kumbuka hapo maji yanapatikana km kama 2 hivi) ni kupigwa na wengine walikuwa wanabakwa.

Kule pia tulikuwa karibu na kambi ya jeshi ya jkt oljoro nadhani. Sasa walikuwa wanawaita "makuruta'' wanatoroka wanakuja kule ni kubaka tuu.

Mungu mkubwa niliishi ghetto miezi mitatu tuu baba yangu akaja akanihamishia hostel ya kanisa ambayo ilikuwa ni private. Basi pale ikawa pona yangu.
N.B sikuwahi kubakwa, ila niliwahi kuchapwa fimbo kama mia na wanakijiji kwa kosa la kuvaa suruali na kitop (si unajua jamii za wamasai? Sasa Mimi nimetoka mjini nimezoea kuvaa vipedo). Na kesho yake ndiyo nilihama huko mtaani.

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.

Dah. Nimeogopa kiasi nikiwaza challenges of the girl child.

Mungu ni mwema alikulinda.
 
Olympio na Diamond Primary School Kipindi cha nyuma kidogo ada ilikuwa ni elfu hamsini na nadhani kabla ya hapo ilikuwa chini zaidi...Iliwezesha watu wengi kutoka familia za chini tuweze kupakimbilia....

Mambo yamebadilika pale nasikia wanakaribia hadi laki nne hvi kiasi kwamba masikini sisi wenye Ndoto japo ya kuwapa upeo kidogo wa lugha ya kiingereza watoto wetu waliotoka familia duni unazidi kuyeyuka...Inawezekana labda gharama za uendeshaji ni kubwa sana hvyo sitaliongelea sana hili...

Tambaza Sec school ni shule kongwe iliyokuwa bora sana Kipindi cha nyuma ila miaka ya karibuni imekuwa na kiwango kibovu cha ufaulu....kuna vitu naona vinavyosababisha hili mfano:

Suala la kuchelewesha wanafunzi kutoka shuleni mpaka saa tisa na ikiwa huduma ya elimu inayopatikana pale ni duni kama tujuavyo shule zetu za serikali walimu ni wavivu na hawawajibiki ipasavyo...Hivyo wanafunzi wanakosa muda wa kwenda kutafuta vyanzo vingine na kupelekea kutegemea elimu itolewayo shuleni tu.

Nitarudi tena baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Olympio na Diamond hawana usimamizi mzuri wa wanafunzi. Very risky wa watoto.
 
Naamini serikali inazifahamu changamoto zote juu ya elimu yetu, A to Z.

Kuna write-ups kibao juu ya elimu kuanzia primary mpaka chuo, na research kibao zinaendelea kifanyika.

Serikali imefumbia macho, siyo kipaumbele chao kwa sababu kuu kadhaa (mtazamo wangu);-
  • Walioko kwenye nafasi za maamuzi haiwaathiri kwa sababu wana uwezo wa kusomesha kwenye private schools
  • Haina 10%
  • Tukielimika itatufungua macho, hivyo wanaona ni bora tubaki mbumbumbu tuendelee kudanganyika (rejea tathmini ya Twaweza kuhusu correlation kati ya kuipenda CCM na ujinga/ukosefu wa elimu)
  • Tukielimika tutawapa competition kwenye kugombea nafasi za kutawala, hivyo wanaendelea kusomesha watoto wao ili wawarithishe vyeo vyao
 
Back
Top Bottom