Uzi Maalum Wa Kujadili Shule Mbali Mbali

me sitaki kuwa specific na shule moja, lakini ningependa kuwa general kwa shule zote za kata. Kulingana ma maana halisi ya elimu na kipimo cha kutahini watahiniwa kuwa ni mitihani, na kwa vile elimu yetu imekuwa ikapambanuliwa kwa mfumo wa serikali na shule binafsi huku pia serikali kukiwa na shule za mkoa, wilaya na shule za kata. Lakini pia hapohapo serikali inajipambanua kuwa na shule zake kongwe na shule za vipaji huku treatments na ruzuku zikitofautiana kati ya madaraja ya shule hizo. Basi ninapendekeza mitihani itungwe kulingana na nature ya mazingira na uhalisia wa maisha ya elimu inayotolewa kwa wanafunzi hao, haiwezekani mwanafunzi asiye na walimu wa kutosha, asiye na vitabu unampima sawa na mwanafunzi wa Marian, Mzumbe, St thomas feza n.k. Maon; mitihani itofautishwe kati ya shule za kata na shule zingize ili kuweza kuacess kile mwanafunzi amejifunza.
 
Bonge la point yaani.

Kuna watoto wanasoma kwa shida sana yaani. Hawana hata gari la kuzuia mvua na jua, waalimu hakuna ilmradi shida.
 
Nijadili PAMBALU shule ya msingi,

shule yetu iko very smart, Iko MKOA WA MWANZA, SENGEREMA jirani na wilaya ya NYAMAGANA na MISUNGWI ambako stand maarufu ya NYEGEZI inapatikana.

inawanafunzi 3500 na usheheeee.

kila darasa wanakaa wanafunzi 180 na wote wanakaa kwenye dawati!! Dawati la watu wa tatu wao hukaa watano kama kwenye hice!

Shule inawaalimu 150 wanao fundisha vizuri kwa lugha ya kiswahili na kiingereza wakiwa na vitabu vya kutosha kwa masomo yote.

Shule yetu hii ina matundu ya vyoo 24 hali inayo sababisha wanafunzi wote 3500 na ushehe kujisaidia vizuri sana na vyoo kubaki visafi kiasi unaweza lia pilau ndani ya vyoo vile.

Hatuna swiming lessons, ila tuna mpira wa sembo (chandimu) kombolela na hata kadome

Hatuna school bus tuna magari yetu yaasili TZ11 (miguu yetu)

Watoto wetu ni wasafi sana, maana wana nguo pea moja wanayo vaa january mpaka disemba.

wengi huja na daftari mkononi, kidumu cha maji na fagio la chelewa la mkono!!

Shule yetu ina toa huduma ya maji ya bomba ambayo nisafi na salama kwa watoto wetu kunywa kipindi cha mapumziko.

Karibuni PAMBALU,

Nishule bora sana ambayo watoto wamefundishwa ABCD EFG HIJK ELOMENOPNQU,

Hawa ndio taifa bora la kesho,

karibuni sana PAMBALU

Kengele yetu ni chuma chakavu,

sisi watoto wetu huingia shuleni kuanzia saa moja mpaka saa nne za asubuhi na huondoka pale wanapo hisi njaa au wamechoka,

hii inathibitisha uhuru wa uhakika kwa wanafunzi wa pambalu!!

Si lazima mwanafunzi awe na proper uniform, huku pambalu hatakama una ndala suruali ya home, sketi ha kanisani unakaribishwa sana

Shule yetu ina wakuu wa shule 10, hawa ni :-

waziri wa elimu, mbunge wa jimbo, diwani wa kata, afisa mtendaji, mwenye kiti wa bodi, mkurugenzi wa halmashauri, mkuu wa mkoa, rasi mkoa, na wengineo.

hawa wote ni wakuu wa shule maana muda wowote wanatoa maamuzi kuhusiana na shule yetu popote walipo!!

PAMBALU wanafunzi wote HUFAULU, Na wooooooote hufaulu kwenda PAMBALU SECONDARY SCHOOL, ambako huko hufika wakiwa ni wataaalamu wa kuongea kiingereza na kusoma.

hivyo wote hufaulu kwa kiwango cha dv zero!!!

Wazazi wako komited sana, wakishaleta watoto january huonekana january ingine kuwaleta wengine kama wapo!!

Wazazi wahuku ni wazalendo sana, kwani watoto wao wanapo kaachini wakiambiwa kutafuta kiti cha mtoto wake, wao husema serikali itawaletea viti.

Inapendeza kwa kweli!!

Waalimu wetu huku hufundisha wajiskiavyo, ivyo wapo huru kwa kuwa wanamishahara mizuri na minono na ya kutosha kiasi cha wao kufungua biashara zingine waweze kukuza kipato!!

KARIBUNI PAMBALU SHULE BORA TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What a way to start the morning and the week. 🤣🤣🤣🤣🤣
 
me sitaki kuwa specific na shule moja, lakini ningependa kuwa general kwa shule zote za kata. Kulingana ma maana halisi ya elimu na kipimo cha kutahini watahiniwa kuwa ni mitihani, na kwa vile elimu yetu imekuwa ikapambanuliwa kwa mfumo wa serikali na shule binafsi huku pia serikali kukiwa na shule za mkoa, wilaya na shule za kata. Lakini pia hapohapo serikali inajipambanua kuwa na shule zake kongwe na shule za vipaji huku treatments na ruzuku zikitofautiana kati ya madaraja ya shule hizo. Basi ninapendekeza mitihani itungwe kulingana na nature ya mazingira na uhalisia wa maisha ya elimu inayotolewa kwa wanafunzi hao, haiwezekani mwanafunzi asiye na walimu wa kutosha, asiye na vitabu unampima sawa na mwanafunzi wa Marian, Mzumbe, St thomas feza n.k. Maon; mitihani itofautishwe kati ya shule za kata na shule zingize ili kuweza kuacess kile mwanafunzi amejifunza.

Hapana mkuu,shule ambazo walimu hamna wa kutosha wala vitabu wala maabara ZIBORESHWE ili ziwe na hizo facilities....na sio kutungiwa mtihani yao....mkianza kubagua huku secondary,mjue na kwenye soko la ajira mtabaguliwa,wale wa Marian,Feza erc ndio watakaopewa kazi,wenzangu na mie wa shule za kata kazi hamna...So kipimo cha kufanya mtihani mmoja kwa wote bado kitaendelea kuwa ni kipimo sahihi...
 
Hivi kwanza ilikuwaje sijaona hii tag?

Mimi naongelea kwenye suala nzima la Hostel au mabweni shuleni. (Shule za secondary)
Kuna shule ambazo zipo mbali sana na mjini (I mean kijijini) na zina pokea wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali za jiji, lakini zile shule hazina makazi maalum ya kuwatunza wale wanafunzi.

Mwishowe wanafunzi wanalazimika kuishi "maghetoni" ili waweze kuwa karibu na shule. Huko wanapoishi nje ya shule si salama kidogo hususani kwa watoto wa kike.

Vile vile watoto wanaomaliza la saba siku hizi ni wadogo sana kimwili na kiumri tofauti na miaka niliyosoma Mimi/wengi wetu katika hii forum. Hata akili zao ni ndogo sana ni vigumu wakaweza kumiliki "ghetto" na kupika na kuweza kuhudhuria shule.

Mimi nilisoma shule ya namna hii na mpaka namaliza pale form 4 mwaka 2010 bado hapakuwa na makazi muhimu ya kuweza kuwa accommodate watoto.

Nashindwa kuitaja hiyo shule maana pengine wameshatatua hilo tatizo lakini naamini bado kuna shule ambazo bado zina hizi changamoto.

Suala lingine ni fimbo jamani, walimu hawaangalii pa kuchapa watoto. Mdogo wangu alirudi nyumbani mgongo umevimba ni fimbo za mgongo walichapwa. Sindani kama ni sehemu sahihi.

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
8 niños?? Form 4, 2010? Smh 😂😂
 
Wazazi wenye uwezo wamebaki na option ya kupeleka watoto private schools.

Government schools ni disgrace.

Dar es salaam, jiji ambalo lingetegemewa kuwa mfano lina shule za msingi ambazo chumba kimoja cha darasa kinakuwa na watoto 200, huko kwingine itakuwaje!
 
Hahahahaha, huko huko ila siyo mirongo.
Ina jina la aliyekuwa kiongozi fulan hivi wa ccm, kipindi Fulani aliomba mapumziko.
Hiyo ya kudandia asoma kaka yangu.
Hivi mpaka Leo hamna magari ya kwenda Kule?

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
Pale kwa Morombo kuna vifodi vinaendaga siku hizi si kuna na chuo cha mambo ya kilimo na ufugaji (nadhani) kipo maeneo hayo hayo so sio challenge kama enzi zetu maana ningekuwa mimi saizi ningekuwa chokoraa maana huo usafiri wake mpaka utoboe skonga saa 5 hapo uwaze kurudi ni shida tupu
 
Wazazi wenye uwezo wamebaki na option ya kupeleka watoto private schools.

Government schools ni disgrace.

Dar es salaam, jiji ambalo lingetegemewa kuwa mfano lina shule za msingi ambazo chumba kimoja cha darasa kinakuwa na watoto 200, huko kwingine itakuwaje!
Fanya siku upate Mtaa wa Kibasila Upanga mida ya Saa 9 home watoto wanavyocheza barabarani na magari yanapita kama kawaida.

Where I schooled huwezi kuta mambo kama hayo. Mpita njia ana haki ya ku note registration bamba yako kwenye uniform na kukushtaki shule then utakipata pata.

Dar es Salaam kutwa wanafunzi kuzurura mpaka unabaki unajiuliza wanatumia system gani? Inabidi 8 to 5 kusiwe na wanafunzi wa upper primary barabarani.
 
Pale kwa Morombo kuna vifodi vinaendaga siku hizi si kuna na chuo cha mambo ya kilimo na ufugaji (nadhani) kipo maeneo hayo hayo so sio challenge kama enzi zetu maana ningekuwa mimi saizi ningekuwa chokoraa maana huo usafiri wake mpaka utoboe skonga saa 5 hapo uwaze kurudi ni shida tupu
Bora hata watoto wetu wasome kwa raha. Kwa sababu maasi na madhambi na ma sins yaliyokuwa yanafanyika kwenye yale mafuso daah.
Mtoto akifika form 2 ni mjamzito (kama ni wakike)

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
 
Bora hata watoto wetu wasome kwa raha. Kwa sababu maasi na madhambi na ma sins yaliyokuwa yanafanyika kwenye yale mafuso daah.
Mtoto akifika form 2 ni mjamzito (kama ni wakike)

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
Wewe uli survive vipi au uliogopa fimbo za mama nyumbani? 😂😂🏃🏃
 
Back
Top Bottom