Pavu Abdallah: Iundwe Tume ya Kijaji kuchunguza Ukiukwaji Mkubwa wa Haki za Binadamu Nchini

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
HOTUBA YA MSEMAJI WA SEKTA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA NDG. PAVU ABDALLAH - 22.04.2022

Tupo katika kipindi ambacho Bunge linaendelea kujadili bajeti za wizara mbalimbali, tarehe 21 April 2022, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/23. ACT Wazalendo katika mwendelezo wake wa kuisimamia serikali, kupitia msemaji wa sekta ya Utumishi na Utawala Bora imefuatilia, imeisoma na kuichambua hotuba hiyo kwa lengo la kumulika na kutazama kwa kiasi gani inakidhi matarajio na matamanio ya wananchi katika kupata huduma na usimamizi wa rasilimali zao.

Kupitia uchambuzi huu tumeonyesha maoni yetu kwenye maeneo tisa (9) yenye mtazamo mbadala wa ACT Wazalendo kuhusu hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, ambayo tunaona ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu na wananchi walio wengi.

1. Mishahara ya Watumishi wa Umma haijapandishwa tangu 2014.

Pamoja na kupanda kwa gharama za maisha, Serikali haijapandisha mishahara ya Watumishi wa Umma kwa miaka 7 iliyopita. Bado watumishi wa umma wameendelea kuishi kwa mishahara midogo sana isiyoendana na uhalisia wa kumudu mahitaji yao. Ongezeko la mishahara ya Wafanyakazi ni takwa la Kisheria, si la Utashi wala Hisani ya Kiongozi mmoja katika Nchi.

Kauli za huko nyuma za serikali zinaonyesha hadaa ya serikali juu ya jambo hili. Awali, serikali iliahidi kuongeza mishahara baada ya kukamilisha uhakiki wa wafanyakazi (ambao ungefanyika ndani ya miezi miwili), kisha pia Serikali ingeendelea kulipa malimbikizo ya madeni wafanyakazi, na kuajiri wafanyakazi wapya lakini haikufanya hivyo.

Kisingizio cha pili, ni kwamba serikali inatumia fedha nyingi kwenye miradi ya ujenzi miundombinu kwahiyo haiwezi kupandisha mishahara. Visingizio hivi inaonyesha kwa kiasi gani serikali hawajali na kiwaheshimu wafanyakazi wa nchi hii.

Ilani ya ACT Wazalendo ya 2020 inakusudia kuthamini Watumishi wa Umma na mchango walionao katika utoaji huduma kwa wananchi. ACT Wazalendo inaamini, Serikali inatakiwa kuheshimu ustawi na maslahi ya Watumishi wa Umma ili waweze kuishi maisha ya raha na furaha. Hili linawezekana tuu endapo Watumishi wa Umma watalipwa mishahara inayowawezesha kumudu gharama za maisha.

ACT Wazalendo inaitaka Serikali kupambanua mikakati, sera zake kwa kujali maslahi ya Watumishi wa Umma. Pia tunato wito kwa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA) kuongoza madai yao ya kisheria kila uchao sio hadi wasubiri risala za Mei Mosi za kila mwaka.

2. Madai ya stahiki za Watumishi wa umma yamefikia bilioni 492.

Hotuba ya Waziri wa Utumishi na Utawala bora bado haijasema wazi ni namna gani Serikali itashughulikia stahiki za watumishi wa umma.
Malimbikizo ya mishahara, madeni na stahiki zilizotakiwa kulipwa kwa Watumishi wa Umma zimefikia shilingi bilioni 429.80 mwaka 2020/2021 kutoka shilingi bilioni 334.15 mwaka wa fedha 2019/2020. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 28%.

Taarifa ya CAG imegunduwa Jumla ya Sh. Billion 492 ni malimbikizo ya mishahara na stahiki nyingine walizotakiwa kulipiwa baadhi ya Watumishi wa umma. Kwa mujibu wa kanuni Na. 23 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma ya mwaka 2009, madai ya Watumishi yanatakiwa yalipwe mara tu yanapotokea. Hata hivyo, CAG ameonyesha kuwa madai yanayotokana na watumishi kutolipwa kwa wakati, malimbikizo ya mishahara ya waajiriwa wapya, waliopandishwa madaraja, makato na posho za watumishi yamefikia shilingi bilioni 429.

Hii inadhihirisha sababu za kuporomoka kwa ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi za Serikali kwa sababu ari ya watumisi wa umma imeshuka,
ACT Wazalendo tunaitaka Serikali iwalipe Watumishi wote malimbikizo ya madai yao mara moja ili kuwawezesha kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimeendelea kupanda miaka ya hivi karibuni.

ACT Wazalendo inawasihi Watumishi wa Umma kushikamana kupitia vyama vyao vya wafanyakazi kuidai Serikali stahiki zao bila woga kwa sababu ni haki yao ya msingi. ACT Wazalendo inaahidi kuwa na Watumishi wa Umma bega kwa bega katika mapambano yao hadi haki zao zitakapopatikana.

Pia, ACT Wazalendo inapendekeza kuwa malimbikizo ya madai ya Wafanyakazi wa Umma yatambuliwe katika takwimu za deni la taifa na Serikali itazame uwezekano wa kuweka sokoni Bondi maalumu kwa ajili ya kupata Fedha za kulipa malimbikizo yote kwa mkupuo na kuweka mfumo ambao utahakikisha kuwa hakuna madeni mapya yanayozalishwa siku za usoni.

3. Taasisi za Serikali kushindwa kuwasilisha makato ya kisheria ya watumishi wa umma kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Afya na Jamii.

Taarifa ya CAG ilibaini taasisi za Serikali zimekuwa zikichelewesha na nyingine haziwasilishi makato ya kisheria ambazo ni stahiki za Watumishi wa Umma kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii,
Bima za Afya, Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA).

Ukaguzi wa CAG umezitaja taasisi 15 ambazo hazikuwasilisha makato yenye thamani ya Sh. Milioni 391.68 ya mishahara kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Pia, taasisi 6 za Serikali zinatakiwa kulipa adhabu ya sh. Milioni 491.51 kwa kushindwa kuwasilisha makato hayo kwa wakati.
Serikali na taasisi zake zinaposhindwa kuwasilisha makato ya kila mwezi ya watumishi husababisha watumishi husika wasipate faida zinazotokana na kujuinga na mifuko ya jamii na afya. Ushahidi huu pia unaonyesha kuwa hakuna utaratibu mzuri ikiwemo ufuatiliaji kuhakikisha uwasilishaji wa makato ya watumishi kwa wakati. Kwa ujumla wake ni kutowajibika kwa wasimamizi wa masuala ya Utumishi. Utaratibu tuliojiwekea ni Taasisi kuwasilisha makato kila mwezi, na kushindwa kuwasilisha makato hayo kwa wakati kutapelekea adhabu kwa Taasisi husika. Serikali ndio muweka taratibu na sasa inaongoza kuvunja taratibu.

ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kupitia Wizara ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuhakikisha makato ya kisheria wa wafanyakazi yanafanywa kwa wakati na makosa haya yasijirudie.

4. Serikali ifanye mabadiliko kwenye Idara ya Usalama wa taifa ili iendane na wakati na kuiondoa kwenye milengo ya siasa.

ACT Wazalendo inaona umuhimu mkubwa wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa taasisi inayojiendesha bila kuegamia maslahi ya kundi lolote nchini na kutanguliza maslahi ya taifa, usalama wa raia na mali zake. Yapo maslahi makubwa kwa Taifa kama kusaidia mamlaka za Serikali kuepuka mikataba yenye hasara, wawekezaji wadanganyifu, matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu, hali ya usalama wa chakula nchini, mbinu na jinsi ya kukabiliana na milipuko ya magonjwa kama UVIKO-19 n.k
Badala yake, miaka ya karibuni, Idara ya Usalama wa Taifa imeonekana kama chombo kinachosaidia kulinda maslahi ya chama tawala kuendelea kubaki madarakani na kuegemea kulinda maslahi ya makundi machache.

Pia, pamekuwa na matukio yanayoashiria uporomokaji wa hali ya usalama nchini kwa kuendelea kuwepo kwa vitendo vya kutishwa raia na wageni nchini hadi baadhi ya raia wa Tanzania kulazimika kuomba makazi ‘asylum’ kwenye nchi jirani na za mbali, uwepo wa kesi za kubambikizwa kwa raia, Serikali kupitisha sera zinazopelekea kukandamizwa kwa haki za wanawake na Watoto wa kike walioko mashuleni. Pia, pamekuwa na matukio ya kupotea kwa raia hasa wanachama wa vyama vya upinzani, wanaharakati na wanahabari, kushamiri kwa matukio ya kutapeliwa kwa wananchi hasa kwa njia za mitandao. Idara ya Usalama wa Taifa haijaweka taarifa ya wazi kwa watanzania, kuwagundua na kuwajibisha wanaosabibisha vitendo hivi vinavyoleta mashaka kwenye hali ya usalama nchini na wameshindwa kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao.

Matukio haya yamepelekea Tanzania kushuka nafasi katika orodha ya nchi salama duniani kwenye miaka ya hivi karibuni. Hii imepelekea hata watalii, wadau wa maendeleo, wawekezaji na wageni kutoka nchi nyingine kuwa na mashaka na usalama wao wanapokuwa nchini.

ACT Wazalendo inaitaka Serikali kutathmini upya inavyoitumia idara ya Usalama wa Taifa ili iweze kuwa ni chombo kinachotumia weledi wake kuliepusha Taifa na hasara za kiuchumi na vitendo vinavyoweza kupelekea kulitia doa Taifa letu kwenye wigo wa haki za binadamu.

5. Upungufu wa wafanyakazi katika taasisi za umma, uwepo wa watumishi wasiyo na leseni za kitaaluma umeendelea kuathiri utendaji na kushindwa kufikia malengo ya utoaji huduma kwa Wananchi.

Taarifa ya CAG imeonyesha upungufu mkubwa wa Watumishi wa Umma unasababishwa na mamlaka kutotoa vibali vya ajira kuruhusu taasisi kupata watumishi wa kutosha. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeshindwa kushughulikia swala la uhaba wa watumishi kwenye taasisi za serikali na matokeo yake ni kushindwa kutoa huduma.

CAG amebainisha, kuna upungufu wa watumishi 33,145 katika taasisi za Serikali kuu, upungufu mkubwa wa walimu, wataalamu wa afya kwenye taasisi za umma nchini. Katika Shule za Msingi, idadi ya Walimu wanaohitajika ni 40,458 na waliopo hivi sasa ni 23,8881 tu. Shule za Serikali zina upungufu wa waalimu 16,571 sawa na 40% na matokeo yake yamekuwa mzigo mkubwa wa majukumu kuwekwa kwa Walimu wachache.

Pia, ukaguzi wa CAG ulibaini uendeshaji duni wa hospitali za Rufaa za Mikoa (RRH) kutokana na ukosefu wa wataalam wa kutosha wa matibabu, dawa na vifaa tiba. Jumla ya wagonjwa 13,583 walipewa rufaa kwenda hospitali nyingine kutokana na upungufu mkubwa wa Waganga wa kutosha. Pamoja na haya kuna watumishi wa umma wasio na leseni za taaluma, kwa mujibu wa taarifa ya CAG, Wataalamu wa Afya 320 kutoka hospitali tano za rufaa wanaofanya kazi zao bila ya kuwa na leseni ya kitaaluma.

Serikali inayowajali wananchi wake lazima ihakikishe inawekeza kwenye raslimali watu watakaotoa huduma bora kwa Wananchi. Pia, taasisi za Serikali ilitakiwa kubaini mapema, kuwa na nyenzo za kuzuia uwepo wa watumishi kwenye vituo vya afya bila leseni za kitaaluma. Hii imeendelea kuweka maisha ya Watanzania hatarini kwa kukosa huduma za afya stahiki.

ACT Wazalendo inaitaka Wizara ya kutoa vibali vya ajira kwa taasisi zinazohitaji wataalamu lakini pia kuhakikisha wataalamu wanaopatikana wana vigezo vya taaluma zao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

6. Wizi wa fedha za Umma na Baadhi ya watumishi wasio waaminifu umeendelea kusababishia taifa hasara kubwa.

Serikali imeshindwa kuimarisha mifumo ya udhibiti wa mapato ya ndani na hivyo kusababisha uwepo wa mianya ya watumishi wa umma kufanya udanganyifu na kuiba pesa za umma.

Taarifa ya CAG imeainisha watumishi wa umma wakiwemo maafisa wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa ubadhilifu wa fedha za umma, udanyanyifu na wizi wa fedha za umma. Hii ni katika taasisi mbalimbali kama Benki Kuu, Idara ya uhamiaji, balozi za Tanzania, taasisi za Elimu, Halmashauri kadhaa nchini.
CAG ameeleza Mapato ya Tsh. 19.72 ya halmashauri yalikusanywa na Mawakala pamoja na watumishi 19 Hatimaye 4.64 Bilion hazikupelekwa Bank.

Taarifa ya CAG imeibua ubadhilifu uliofanywa na watumishi wa balozi kadhaa zikiwemo ubalozi wa Tanzania – Addis Ababa, Ethiopia ambako palikuwa na ufujaji wa ada za VISA, ACT Wazalendo inaitaka Serikali kutunga sera za usimamizi kwenye taasisi zote za Serikali na kufanya tathmini za mara kwa mara kuepuka hatari za ubadhilifu.
Pia, ACT Wazalendo inaitaka Serikali kuhakikisha inazisimamia taasisi zake kufanya kwa uaminifu tathmini ya ufanisi na utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa mfumo uliopo wa OPRAS ili watumishi wanaogundulika kukosa uadilifu na uaminifu kuchukuliwa hatua za kinidhamu mapema.

7. Kudorora kwa dhana ya utawala bora katika utumishi wa Umma
Sekta ya utumishi wa umma ni sekta inayotoa huduma katika jamii. Hivyo basi wale wanaotoa huduma hiyo wanaposhindwa kutoa huduma hiyo kwa viwango stahiki maana yake ni kwamba Serikali imeshindwa kukidhi matakwa na matarajio ya wananchi ambao ndio wateja wake. Yapo malalamiko ya wananchi juu ya utendaji wa watumishi wa umma usiozingatia msingi ya utawala bora.
Dhana ya utawala bora kuwa ni matumizi sahihi ya mamlaka ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika kusimamia masuala ya nchi kwenye ngazi zote ambayo uambatana na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu.

Ili kutekeleza utawala bora lazima mambo kadhaa yazingatiwe ikiwemu; matumizi ya kiutu ya dola na vyombo vya mabavu, matumizi mazuri ya rasilimali kwa faida za wananchi, matumizi mazuri ya madaraka na kutambua na kuheshimu madaraka na mipaka ya uongozi, katiba na sheria.

ACT Wazalendo tunaitaka serikali kufanya mabadiliko ya mfumo na utendaji wa Tume ya Maadili ya Umma ili kuipa nguvu na nyenzo za kusimamia kikamilifu maadili ya utumishi wa umma, kwa kuweka utaratibu wa kisheria utakaoelekeza uteuzi wa viongozi wa Tume hii kufanywa na Tume ya kijaji, chini ya Jaji Mkuu na kufanyiwa usaili na kuthibitishwa na Bunge ili kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi.

8. TAKUKURU kuwa na kazi za kuzuia rushwa kuliko kungoja kupambana na makosa yatokanayo na rushwa.

TAKUKURU imeendelea kuwa chombo kinachopambana na matokeo ya rushwa badala ya kuwekeza kwenye kuishauri Serikali mbinu za kubaini, kuviharibu vyanzo vya rushwa nchini.

Mapendekezo ya hotuba ya Wizara bado yameendelea kuwa na mipango ileile ya miaka yote ambayo haijafanikiwa kuondoa vitendo vya rushwa katika taasisi binafsi na za umma.

Hotuba ya Waziri imeonyesha TAKUKURU ilibaini miradi 81 kuwa na mapungufu katika utekelezaji wake kufikia thamani ya shilingi bilioni 43 na bado hatua za kisheria hazijachukuliwa kwa wahusika.
TAKUKURU inatakiwa kujitathmini na kurekebisha utendaji wake.

ACT Wazalendo inaitaka Serikali kuimarisha mifumo, dira na utendaji wa TAKUKURU ili kiwe chombo cha kisasa kinachokuja na mbinu za kuishauri Serikali kuondoa vyanzo na motisha za vitendo vya rushwa na kuondoa kabisa mianya ya rushwa. Gharama za kupambana na matokeo ya rushwa ni kubwa ikilinganishwa na kama TAKUKURU ikijenga mifumo yake kuzuia vitendo hivi.

9. ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuunda Tume ya Majaji ya kuchunguza matendo ya mauaji, utekwaji, ubambikiwaji wa Kesi nchini.

Kutokana na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza ndani ya nchi yetu ni wazi kuwa kuna malalamiko, vinyongo na kupoteza matumaini kwa wananchi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuliunganisha taifa. Masuala ambayo tume ya uchunguzi ya majaji inapaswa kuifanyia kazi ni kupotea kwa baadhi ya wananchi na wengine kuuwawa kikatili, kuchunguza kesi zote zinazotokana na uchaguzi na siasa kwa ujumla wake,matukio ya utekwaji wa raia, kuuwawa kwa wananchi wakiwa kwenye mikono ya vyombo vya dola.
Kama ambavyo kwenye Ilani ya ACT Wazalendo ya mwaka 2020 inavyosema kuwa “Ili kuboresha taasisi za ulinzi na usimamizi wa sheria Serikali ya ACT WazalendoiI itaboresha muundo na utendaji wa vyombo vya dola ili kuviwezesha kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa kisiasa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria na Katiba.”

Mwisho, hotuba ya bajeti ya Wizara ya Menejimeti, utumishi wa Umma na utawala bora ilipaswa kuwa nyenzo muhimu katika kumulika uwajibikaji wa serikali kwa kuimarisha vyombo vya kuisimamia serikali kama vile Ofisi ya Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa hesbabu za Serikali, Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuimarisha uhuru. Pia kuimarisha taasisi za usimamizi na ulinzi wa sheria kama vile, Usalama wa taifa, tume ya maadili ya utumishi wa umma. Lakini hotuba ya Waziri wa Utumishi na Utawala Bora yenyewe imeshindwa kujimulika na kuona uhalisia wa kuporomoka kwa hali ya misingi yake nchini.

Imeandaliwa na:
Ndugu. Pavu Abdalla
pabdallah@actwazalendo.or.tz
Msemaji wa Sekta ya Utumishi na Utawala Bora - ACT Wazalendo.

IMG-20220422-WA0017.jpg
 
Naunga mkono hoja ILA kabla ya kuunda jopo la kijaji kuchunguza hayo,majaji wote wajiuzuru na waombe kuwa majaji na wafanyiwe interview na kamati maalum, binafsi judge ninayempa heshima ni aliyekua Judge mkuu wakati nchi Ina heshima na adabu, CJ Francis Nyalali (rip)waliobaki wote ni upotolo tu.
 
Daaah hawa jamaa 🤔 yaan Kwel wamedhamiria kbs kufuta legacy yote? Hata kutuachia angalau machache?
 
Chama cha AYATOLLAH ZITTO ZUBERI KABWE
 
Back
Top Bottom