Uzi Maalum Wa Kujadili Shule Mbali Mbali

Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
18,143
34,180
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza na kwa kuzingatia JF ni uwanja mpana unaojumlisha wazazi, wamiliki wa shule, maofisa wa elimu wenye wadhifa tofauti na pia kwa vile waalimu wamo humu basi tukutane kujadili uwanja mzima wa Shule za Nursery, Primary na Secondary Tanzania.

Tutakosoa mifumo mbali mbali ya elimu, ada ambazo wazazi wanahisi ni uonevu kwa vile hazikuwepo mwanzoni.... kudorora kwa elimu ama performance ya shule.... nidhamu za wanafunzi na hata waalimu wao... na kadhalika.

Karibuni wana JF....

Cc Mshana Jr Madame S Khantwe snowhite Mentor Asprin Daby cute b Relief Mirzska farkhina Dreka BAK Watu8 Castr Nyani Ngabu BAFA
chaliifrancisco espy Hornet Zamazamani
Rebeca 83 Lizzy afrodenzi Sky Eclat
 
Hii mada kwakua haiko specified ni pana mno.

Ingewekwa kwenye kujadili eneo moja, takwimu zaidi na taarifa zaidi zingetolewa.
 
Nitaijadili Shree Hindu Mandal Nursery School iliyopo Upanga Dar es salaam. Naikubali kwamba ni shule nzuri na wana system nzuri kuanzia elimu yake, na napenda sana wanavyowajali wanafunzi na kuwalinda.

Watoto wanareport 7.30 a.m na wanaondoka shule 12.00 pm. Wakiwa shuleni kila darasa lina waalimu wawili na caretaker mmoja. Hawa waalimu mmoja ni Mswahili (African) mwingine ni Muhindi.

Caretaker ni binti ambae kazi yake ni kama househelp wa nyumbani. Kuwaangalia watoto. Kuwasindikiza washroom, kuwanawisha mikono na sabuni akitoka washroom na wakati wa kula snacks wanazobeba kutoka nyumbani saa nje asubuhi. Wakimaliza anawasafisha pia. Na kuwasindikiza kwenda kupanda school bus ikifika saa sita.

Wakati wa swimming classes, wanafunzi wana swimming instructor ambae anashirikiana na caretaker wa darasani kuwabadilisha watoto nguo na wana pre shower kabla ya kuingia swimming pool na baadae kuwabadili nguo.

Wakati wa kuondoka shule mtoto huwa anakabidhiwa only kwa mzazi ama mlezi ambae wana picha yake ama kwa school bus na hizi school bus tumechaguliwa na shule so wanawafahamu vizuri. Watoto wanaletwa mpaka nyumbani na kukabidhiwa kwa mzazi ama mlezi anaefahamika.etc etc

Mtoto akienda na alama yeyote shule mzazi inabidi ujieleze mtoto kaumiaje na alama kaipataje. If its violence my friend you will get it.😀😀

Kiukweli sina complaints whatsoever kuhusu Shree Hindu Mandal Nursery School Upanga. Bravo.
 
"Na hizi school bus TUMECHAGULIWA na shule"
 
Sorry, nilichomaanisha ni kwamba haya magari ya shule wamiliki na madereva wao wanajulikana na shule.

Sijui kama hapo mpana ufasaha nakaribisha kusahihishwa.

Usijali nilielewa, ila nilikua najaribu kuchokoza mada km jamaa wa hard talk
 
mimi bado nalia,lugha ya kiingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia vidudu mpaka chuoni,

kisha,Serikali ijenge state nursery schools,sasa hivi nursery nyingi ni private na kwa watu wachache wanaoafford hizo fees...serikali inaweza kutoa cheap nursery kila m toto apate better start..
 
Mimi sisomeshi sina uchambuzi wa moja kwa moja. Ila nitaongelea elimu kwa ujumla wake.

Tanzania elimu yetu haiko sawa.

Tangu tupate Uhuru hatujawahi kua na sera ya elimu ambayo ilidumu, kuanzia Nyerere na UPE mpaka sasa Magufuli na Elimu Bure.
Ukifuatilia kila Rais alikuja na lake ilipokuja swala la elimu, kuanzia mitaala, vitabu vya kiada, walimu wa kufundisha, sasa hivi hadi muda wa kufunga na kufungua shule Rais anadictate.

Surprisingly hakuna sera ambayo iliridhisha kiasi atakayefuatia aone ngoja niendelee na hii. Kila anayekuja anafanya majaribio yake.

Watu wanaojipendekeza, waoga, wanaokaa kusubiri elimu iwakomboe ni matokeo ya hayo majaribio. Ni matokeo ya mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika lakini anafaulu kwenda kidato cha kwanza.

Kuna mwaka niliona kitabu cha kiada cha shule ya msingi inaonyesha sehemu za mwili na kazi zake. Kile kitabu kilionyesha kichwa halafu kazi yake ilikua ni kubeba mizigo.

Huyu mtoto tunataka aweje?
 
mimi bado nalia,lugha ya kiingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia vidudu mpaka chuoni,

kisha,Serikali ijenge state nursery schools,sasa hivi nursery nyingi ni private na kwa watu wachache wanaoafford hizo fees...serikali inaweza kutoa cheap nursery kila m toto apate better start..
Kuna nchi nyingi kiingereza siyo lugha ya kufundishia.

Hakuna nchi ambayo inaendelea kiuchumi halafu hapohapo inazikataa tamaduni zake, HAKUNA.

Tamaduni inatia ndani lugha.

Kama leo tukishakataa kiswahili kesho kutwa tutakataa nini?

Wachina, Wajapan, Wadenish n.k hakuna aliyeikataa lugha yake na kumfundisha mtoto kwa lugha ngeni. Leo hii ukiomba scholarship China cha Kwanza wanataka ujifunze kichina ndiyo udahiliwe.
 
mnhhh.hata hizo nchi nyingi sasa hivi wanatafuta walimu wa English,

watoto wakifundishwa kwa kingereza madarasa yote,nursery,primary,secondary na chuoni sidhani kama itakua tatizo…..

kisha kwenye ajira mtu kama kasomea vitu kwa Kiswahili,inam limit huyu mtu afanye kazi katika nchi zinazoongea Kiswahili tu...au makampuni ya Kiswahili tu...ila kwa Kingereza inapanua wigo,unaweza uka explore hata kazi nje ya nchi...as English ni standard language...

Mambo ya culture yaache Adrian,hata tufundishwe ki china,kiswahili hakiwezi kufutika...
 
V
mimi bado nalia,lugha ya kiingereza kiwe lugha ya kufundishia kuanzia vidudu mpaka chuoni,

kisha,Serikali ijenge state nursery schools,sasa hivi nursery nyingi ni private na kwa watu wachache wanaoafford hizo fees...serikali inaweza kutoa cheap nursery kila m toto apate better start..
Very true.

Hii vita against English we cannot win.
 
Hivi kwanza ilikuwaje sijaona hii tag?

Mimi naongelea kwenye suala nzima la Hostel au mabweni shuleni. (Shule za secondary)
Kuna shule ambazo zipo mbali sana na mjini (I mean kijijini) na zina pokea wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali za jiji, lakini zile shule hazina makazi maalum ya kuwatunza wale wanafunzi.

Mwishowe wanafunzi wanalazimika kuishi "maghetoni" ili waweze kuwa karibu na shule. Huko wanapoishi nje ya shule si salama kidogo hususani kwa watoto wa kike.

Vile vile watoto wanaomaliza la saba siku hizi ni wadogo sana kimwili na kiumri tofauti na miaka niliyosoma Mimi/wengi wetu katika hii forum. Hata akili zao ni ndogo sana ni vigumu wakaweza kumiliki "ghetto" na kupika na kuweza kuhudhuria shule.

Mimi nilisoma shule ya namna hii na mpaka namaliza pale form 4 mwaka 2010 bado hapakuwa na makazi muhimu ya kuweza kuwa accommodate watoto.

Nashindwa kuitaja hiyo shule maana pengine wameshatatua hilo tatizo lakini naamini bado kuna shule ambazo bado zina hizi changamoto.

Suala lingine ni fimbo jamani, walimu hawaangalii pa kuchapa watoto. Mdogo wangu alirudi nyumbani mgongo umevimba ni fimbo za mgongo walichapwa. Sindani kama ni sehemu sahihi.

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
 
mnhhh.hata hizo nchi nyingi sasa hivi wanatafuta walimu wa English,

watoto wakifundishwa kwa kingereza madarasa yote,nursery,primary,secondary na chuoni sidhani kama itakua tatizo…..

kisha kwenye ajira mtu kama kasomea vitu kwa Kiswahili,inam limit huyu mtu afanye kazi katika nchi zinazoongea Kiswahili tu...au makampuni ya Kiswahili tu...ila kwa Kingereza inapanua wigo,unaweza uka explore hata kazi nje ya nchi...as English ni standard language...

Mambo ya culture yaache Adrian,hata tufundishwe ki china,kiswahili hakiwezi kufutika...

Ni kweli ila walimu wanatafutwa ili watu wafundishwe kukijua kiingereza kama lugha na siyo sehemu yao ya maisha.

Kama ujuzi wa mtu una soko lugha siyo kikwazo hata kidogo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom