Uzi maalum kwa madereva na abiria wa bodaboda (mikasa, matukio, changamoto na ngekewa)

Doctor Ngariba

JF-Expert Member
Jan 28, 2020
480
765
Habari ya weekend JF members,

Mimi mzima wa afya na mwenye changamoto ya kiafya nampa pole na kumuombea apone arejee katika majukumu ya kulijenga taifa mama Tanzania.Pole zangu pia ziwaendee kwa walioguswa kwa namna moja ama nyingine kwa hukumu ya nyundo (30 yrs behind the bars) iliyopitishwa juzi kwa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai ndugu SAYABA (rejea mahakamani kule).

Mabwana wakubwa tujifunze kupitia huyu kijana Sabaya ''Madaraka ni kama nguo hutoyavaa milele, aidha utavua au utavuliwa'' na situation moja kati ya hizo mbili ikitokea ndipo unabaki huna power ya kureact kama ulivokuwa kabla.Tutende wema nyakati zote,tuishi na watu vizuri ili tupate kuchangamana nao vema pindi tuanapotoka kwenye madaraka.

Wakuu naomba niende moja kwa moja kwenye mada hapo juu. Nimepata msukumo wa kutaka kushare na wenzangu hapa jukwaani kuhusu mada tajwa kutokana na mchango wa usafiri wa boda boda katika kuleta kipato cha mtu mmoja mmoja na hatimae taifa kwa ujumla kutokana na unafuu na uharaka wa usafiri husika.

Kadhaika usafiri huu umeleta majanga mbalimbali kwa jamii ikiwa pamoja na vifo,ulemavu wa kudumu na hata kuhusika katika shuhuli za ujambazi,wizi, ukahaba na utekaji nyara.Lakini pia usafiri huu umeleta urafiki na hata wengine kupata MAZALI YA MENTALI mwanawane (Big up kwa wote mliotusua kupitia boda boda).

Hivyo naamini kupitia uzi huu tutajifunza mengi kupitia shuhuda mbalimbali kutoka kwa madereva na watumiaji wa usafiri huu wa boda boda.Naomba watu wajimwage ili TUFAIDI VIZUURI.

Kwa upande wangu nitatoa kisa kilichompata rafiki yangu ambae ni dereva boda boda alikuwa anapaki boda yake kijiwe flani hapa town (DASLAM). Kama kawaida siku ya tukio mshikaji alipaki kijiwe kusubiria abiria ili apate chochote kitu.Mungu si Athumani alikuja abiria na kumtaka rafiki yangu ampeleke maeneo ya Karakata.

Jamaa akawasha chuma na chombo ikaanza kutembea kuelekea eneo husika.Na wakati huo huo kuna boda nyingine ilifuata kwa nyuma yao ambayo nayo ilikuwa na watu wawili (dereva na abiria).

Vuta mafuta chuma ikavuka reli (kama unatoka upande wa airport kwenda karakata) wakasonga mbele ghafla yule abiria aliyepakiwa na rafiki yangu akampiga roba jamaa angu huku pikipiki inatembea na huku ile boda ya nyuma inakuja kwa nyuma yao.Jamaa alikomaa huku anaendesha lakini baadae akachemka wakaanguka chini jamaa angu fasta akachomoa ufunguo kwa kujua kwamba hakupakia abiria bali kapakia Sabaya jr.(mnisamehe bure huyu jamaa alionea sana watu).Yule abiria akaanza harakati za kumnyang'anya ufunguo rafiki yangu lakini alichemka.

Ile boda nyingine ilisimamishwa majamaa yakateremka kuja kuongeza nguvu lakini mshikaji bado akakomaa jamaa wakaona usituzingue wakaanza kumcharanga mapanga ya kichwa na mikononi mwishowe jamaa angu akajikuta amezindukia hospitali huku akiwa na majeraha sehemu kadhaa za mwili na pikipiki ishabebwa na wajuba.Pole sana rafiki yangu japo umesema hutoacha kazi yako ila namuomba Mwenyezimungu akuepushie majanga katika harakati za kupambania familia yako.

Jamani mambo ni mengi lakini naomba tutiririke hapa (matukio,mikasa,changamoto na ngekewa) yaliyokupata au kumpata mtu wako wa karibu na hata asiye wa karibu.

KARIBUNI
 
Kuna conductor alimtusi mwenzie kwamba jamaa hakuzaliwa Kwa njia ya kawaida Bali mama Yake alimnya, hao wezi unaweza ukasema nao hawakuzaliwa
 
Sema kwa mimi sijaelewa..
piki piki inaendeshwa ghafla ikaanguka jamaa akachomoa funguo🧐🧐🧐.. yaani wapo kwenye mwendo wakuibiana na kujiokoa. Akaanguka akachomoa funguo.. kachomoa kabisa… aaaaanh bwana…

Mimi nina visa viwili vyakuchekesha na kusikitisha. Ukinipa maelezo vzuri ntakwambia.
 
Back
Top Bottom