Simulizi: Madhila Wanayopitia Madereva wa Malori Boda ya Tunduma. Mamlaka Ziko Wapi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,863
Kwa nini mnawacheleaesha kiasi hiki? Tatizo ni nini Hadi Hali inakuwa mbaya kiasi hiki? Urasimu utaisha lini?

Serikali wasaidieni Madereva hapo Mpakani Tunduma,Wiki 2 unakaa kusubiria documents? Seriously?

Waziri wa Fedha , Waziri wa Biashara,Wizara Ya Mambo ya ndani na taasisi husika inaman hamuyaoni haya?

----
"Boda ya Tunduma (Songwe) na Nakonde (Zambia) kuna changamoto kubwa sana sioni sababu ya kuwaweka madereva siku nyingi. Unatoka Dar es Salaam umekabidhiwa mzigo na documents kwa wakati anapewa siku Saba za kufika boda. Unafika boda unakabidhi documents lakini cha kushangaza dereva anakaa kusubiri document mpaka wiki Mbili. Ukiuliza unaambiwa documents bado!.

"Unakaa pale unatumia pesa, unalala gesti, unakula. Kuna sababu zipi za kukaa wiki Tatu? Inanifikirisha inawezekana zile biashara za gesti na chakula pale boda ni za watu? Nashauri Waziri mwenye dhamana aende akafuatilie hizi boda kuna nini? Mbona Malawi hakuna huo utaratibu?? Juma Nyambwilo, Dereva wa Malori


View: https://www.instagram.com/p/CzAppT5iC1G/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Back
Top Bottom