Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,619
- 46,258
Binadamu yoyote tofauti na wanyama ili aweze kukua vizuri, apate maendeleo na astawi anahitaji msaada, uangalizi na muongozo wa muda mrefu wa wazazi, familia, ndugu, marafiki, majirani na Serikali.
Anahitaji apatiwe chakula bora, mavazi bora, makazi, na elimu bora tangu akiwa mdogo hadi angalau miaka 18. Akimaliza masomo yake anahitaji apewe mazingira mazuri/awezeshwe kujipatia kipato kupitia kazi za hadhi nzuri "decent jobs". Wenye jukumu hili ni Familia yake na Serikali. Wanaposhindwa kutimiza jukumu hilo ndipo tunaona taifa likizalisha vijana lukuki ambao ni wamachinga, wauza pipi na maji barabarani, bodaboda na mama ntilie wanaopikia kuni katikati ya majiji.
Lawama nyingi zinaelekezwa serikalini kunapoteka matatizo yanayohusu kufuata utaratibu kwa makundi haya lakini ni vyema tujikite katika chanzo cha tatizo ambacho ni 1.sera za kiuchumi zilizoshindwa kufungua sekta za uchumi mkubwa wa viwanda, kilimo na huduma 2.
Kupuuza uzazi wa mpango kwa raia wengi. Ni lazima sote tukubali zama za kuzaa rundo la watoto ambao hujui hatma yao watakapofikisha miaka 20 zimepitwa na wakati. Hizi na zama za kuwa na watoto ukiwa na mpango kichwani wa jinsi gani watoto hao hawataishia kuwa makabwela wanaotanga tanga.