SoC03 Afya, uzazi wa mpango

Stories of Change - 2023 Competition

WINER777

New Member
Jul 31, 2023
1
0
Mwandishi MZT company limited, kazi za jamii.
Yanachochea mabadiliko katika utawala bora.

UZAZI WA MPANGO NI NINI?

Uzazi wa mpango ni uamuzi wa hiari unaofanywa na mtu binafsi, mwenzi au wote wawili, ili kuamua ni lini watapata watoto, baada ya muda gani na kuufuata.

Huu ni uzazi unaofutata misingi, taratibu nzuri za uzazi kwa mama aliyefikia umri wa kuzaa.

AINA ZA UZAZI WA MPANGO:

  • Kiasili
  • Uzazi wa mpango kwa njia asilia maana yake ni mbinu zile za kuzuia mimba isipatikane katika tendo la ndoa ambazo zinafuata maumbile tu.

  • Njia asilia za kupanga uzazi ni mbinu ambazo hazihusishi vifaa wala kemikali, bali zinategemea ufahamu wa uwezo wa mwanamke kupata au kutopata mimba wakati wa kufanya tendo la ndoa.
1pfpey9r.png
  • Kisasa
  • Njia asilia za kupanga uzazi ni mbinu ambazo zinahusisha vifaa vya kemikali, na ufahamu wa uwezo wa mwanamke kupata au kutopata mimba wakati wa kufanya tendo la ndoa, mfano njia ya mpira, vidonge

UZAZI TZ.jpg

Uzazi salama ni uzazi unaofuata kanuni za afya na usiokuwa na madhara baina ya pande zote mbili
Uzazi usio salama ni ule usiofuta taratibu zote za kiafya na usalama wa uzazi

DINI NA MPANGO WA UZAZI WA MPANGO.

Dini zote hukataza uzazi usio na mpangilio kwani hukataza kabisa zinaa, na huruhusu tendo la ndoa kwa wanandoa.

Uzazi wenye mpango na uzuri wake unachochea maendeleo ya :-

  • Kisiasa - Siasa safi na utawala bora
  • Kiuchumi - Uchumi imara ulioshamiri fursa kwa watu wote
  • Kijamii – Huchochea jamii yenye ustawi na siha njema
  • Kiutamaduni – hudumisha na kusitawisha utamaduni na kuepusha vifo na magonjwa mbalimbali, mfano ya kusononeka kama kulazimishwa kuoa au kuolewa na mtu usiyemtaka, hali itakayopelekea migogoro ya kifamilia na malezi mabovu kwa Watoto.

Uzazi wa mpango usio wa mpangilio husababisha:-
  • Idadi isiyo maalumu, takwimu zitakazokinzana, na mpango mkakati wa Taifa hali inayopelekea kushindwa kufikia lengo kwa mlipuko usiotarajiwa wa uzazi
  • Kutoendelea, maendeleo hafifu yasiyo na uhusiano kabisa na dhamira nini maana ya maendeleo kushindwa kufikia malengo
  • Kutoendana na misimamo, mahitaji ya ulimwengu na wahisani mbalimbali ndani na nje nchi

TOTO.jpg
TOMBO.jpg

  • Vifo, maradhi mbalimbali yatokanayo na kutopangilia wakati sahihi wa kutaka kuzaa mfano:- Kifafa, Festula
  • Kifafa Festula
  • Mimba za utotoni na ibuko kubwa la watoto wa mtaani, Watoto kuzaa Watoto kwani wanaume wengi wanapowapa ujauzito Watoto hawa huishia kukimbia
  • Serikari, Taifa linayumba, hapa wanaposhindwa kusimamia na kusaidia idadi kubwa ya watoto wa mtaani, mayatima na kutengeneza magenge ya uharifu mfano panya road
Nini kifanyike
  • Elimu ya uzazi wa mpango ihimizwe na ifanyike kuanzia nyumba za ibada, serikali za mtaa, tena kwa dhati bila mzaha wowote
  • Kusisitiza utawala bora, utakaokuwa huru na wa haki, utakaosikiliza mawazo haswa ya wananchi tena wa hali ya chini ndo wanafahamu vyema yanayowakuta na kuwasibu hususani hali ngumu ya maisha, ukosefu wa ajira na kupelekea msongo wa mawazo na wengine kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa kutokana na afya za akili kutokuwa sawa, unyonge uliopitiliza na masikini wengi mawazo na misongo yao humalizikia katika ngono, zinaa na kusababisha watoto wengi wasio rasmi kwa wakati wake, mara chache wazazi wa watoto haswa wa kike huwauw
  • a kwa kuwatupa chooni, ama kuwatelekeza na kuibuka kwa idadi kubwa ya watoto wa mtaani na mazio ya uhalifu mfano panya rodi, makahaba na watumia madawa
panya rodi makahaba watumia madawa

PANYA 3.jpg

picha kutoka mtandaoni

Mfano mchache wa haya makundi, ukiangalia kwa undani ni tatizo litokanalo na familia walizotoka, koo, historia zao za vizazi na vizazi.

Ni ukweli usiopingika kilichotoka katika mfumo bora, huwa bora kwenye kila kitu, na kisicho bora na kikawa bora ni nadra sana kuwa bora ingawa wapo wapo, hawa ni wachache.
  • Kufuata technolojia na mahitaji ya ulimwengu, ni vyema kuwa na taratibu katika kuzaliana mfano ndoa.
  • Mfano wa taifa lisilofanikiwa kwa kuwa na idadi maalumu ya katika kuzaana
Screenshot_20230731-184330.jpg

Tanzania
  • Mfano wa taifa lililofanikiwa ingawa lina watu wengi
CHINA.jpg

China-picha kutoka mtandaoni

Kila mmoja kuwajibika kuishi kwa nidhamu, ukweli, na kuchapa kazi na kushambulia fursa popote, inapoonekana na kuacha maneno, unyonge na kuweka mikono shavuni, kwani nguvu za mwili na akili zinapotea, na hata hakuna atakaye kuonea huruma, wala kupoteza wakati wake kukuhurumi, kwa hiyo ni vyema kuishi katika kujitambua na kutambua wengine.
Na kuyatazama maisha katika jicho la tatu zaidi na kujifunza kupita wengine na kujiamini, kuwa huru, kufanya kwa pamoja kwa kushirikiana, na mataifa mengine kwenye mambo madogo madogo ambayo yana faida kubwa sana.

Mfano matumizi ya fursa za jumuiya ya Afrika mashariki, kama wasemavyo watu wamoja, lengo moja ni sawa na sahihi na lazima watu hususani wajasiriamali wadogo kutumia fursa za kibiashara, kijamii kitamaduni kujikwamua kwenye biashara mfano:

Karanga, mahindi mabichi, hiliki, karafuu, mchele, karanga, vitenge, viatu kupeleka nchini Uganda, Kenya,
vitu hivi navijua kwa uthibitisho kwakuwa nilishafanya utafiti na mradi kuelezea fursa zinazotokana na mtangamano wa jumuiya ya afrika mashariki, watu wamoja lengo moja.



Tazama baadhi ya fursa zinazopatikana Afrika mashariki

CHAMBANI.jpg
KATANI.jpg


picha kutoka mtandaoni


HITIMISHO
Jamani bila kuuma uma maneno tujiajiri tutumie vyema ardhi yetu ya Tanzania ili kuvuka umasikini, tupendane, tuwe watu wa kiasi, tuache dhuruma iliyopitiliza ardhini, na tupeane nafasi kwani kila mmoja anauwezo na lazima afanye jambo kwa ajili ya nchi yake.

Na wenye uwezo tayari wa kifedha, na wako tayari kuzungusha fedha zao kwa njia nzuri washirikiane na wataalamu mfano sekta ya afya, makampuni, taasisi kutatua matatizo yatokanayo na afya, mfano maswala ya afya uzazi wa mpango, ajira, siasa safi na uongozi bora pamoja na uchumi imara.

Asanteni na tumwogopeni Mungu kwa hatua zote anatuona
 
Back
Top Bottom