Uzalendo sio kuvaa nguo zilizoshonwa kwa vitenge vya bendera ya Taifa

De Fernandez

Member
Oct 13, 2023
22
26
Watu wengi tumekuwa katika fikra ya kwamba uzalendo ni kuwa tayari kuipigania nchi yako.

Huo ndio ukweli lakini uzalendo pia unaambatana na mapenzi ya dhati kwa taifa lako.

Mapenzi haya ndio watanzania wengi tunayakosa yaani hatuna uchungu na Taifa letu la Tanzania pamoja na rasilimali zake.

Uzalendo pia unaambatana na uwajibikaji wa kila mmoja wetu ili kuleta maendeleo katika taifa letu 🇹🇿. uwajibikaji wa kila mtu katika nafasi yake.

Kama alivyosema Mwl Julius Kambarage nyerere kuwa ili tueendelee ni lazima tupambane na maadui watu (ujinga,maradhi na umaskini).

Ni lazima kila kiongozi awe muwajibikaji pia aepuke Matumizi ya Rasilimali za Taifa kwa maslahi yake binafsi kwani ipo siku watakuja kuulizwa na Mwenyezi mungu na kulipwa kutokana na waliyoyatenda, pia watambue kwamba uongozi ni mtihani waliopewa na Mwenyezi mungu kuwapima uadilifu wao kwa hiyo wajitahidi kufaulu mtihani huu.

Kwani katika Qur'an imeandikwa kuwa mwenyezi mungu hawapendi mafisadi
"Na utafute, kwa aliyokupa Mwenyezi mungu, makazi ya akhera. wala usisahau fungu lako la Dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi mungu alivyokufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi mungu hawapendi mafisadi" Qur'an (28:77)
 
Back
Top Bottom