Uzalendo ni nini?

Ni bahati mbaya sana kwamba hii mada haikupewa uzito unaostahili. Miaka zaidi ya 6 tangu ianzishwe, umuhimu na uzito wake kwa nchi yetu unajitokeza kwa nguvu mpya. Bado swali la msingi halijajibiwa ipasavyo - UZALENDO NI NINI?
Kwa tafsiri ya sasa ni kuwa uzalendo ni ile hali ya dagaa walioko baharini kusifia kila kitu anachofanya papa
 
Kwa Bahati Mbaya Mtu Ukiwa CCM Ndio Unaonekana MZALENDO.
Uzalendo Sio Kuvaa Skafu Ya Bendera Ya Taifa.
Uzalendo Sio Kuisifia Serikali Pale Inapotimiza Wajibu Wake.
Uzalendo Sio Kwenda JKT.
Uzalendo Sio Kuimba Nyimbo Za Kusifu.
UZALENDO NI HISIA Za Mtu ZIZOKUJA KWA WAKATI FULANI. NA WALA UZALENDO HAUFUNDISHWI HAKUNA SHULE INAYOFUNDISHA UZALENDO DUNIANI.
Definetly you are a very rude oligarch, desperate to cling on thin air of your last breath of tormenting the poor people.
 
Wadau,
Naomba kuuliza swali hili la kizushi kwa sababu hivi sasa kumezuka mtindo wa kuwashutumu watu wanaofichua maovu kuwa hawana uzalendo.

Kwa mfano, Lissu alipoulizia kuhusu ahadi ya ndege tuliyoahidiwa na Mh Igwe kuwa ingefika July lakini mpaka Agosti haikufika na kuhusu kushikiliwa kutokana na deni lililotokana na uvunjwaji wa mkataba - akaambiwa hana uzalendo na kutiwa nguvuni

Lissu huyohuyo alitahadharisha mambo kadhaa kuhusu suala la mchanga wa Accasia akaitwa mropokaji, hana uzalendo, leo tunadaiwa mapesa kibao.

Kampuni ya uwakili ya IMMMA Advocates inasadikiwa kuwapa msaada wa kisheria Accasia na inadaiwa kuwa Lissu pia ni miongoni mwa mawakili mahiri waliopewa dili hilo la kuitetea Accasi dhidi ya sirikali sikivu- napo wanaitwa wasaliti, eti kwanini wanawasaidia wezi.

Hapo sasa naomba msaada kuhusu maana halisi ya neno uzalendo, lakini pia mnisaidie kati ya Lissu na wanaomuita msaliti nani mwenye uzalendo?

Hivi nafasi ya kubadili vifungu vya sheria za mikataba ya madini iliyopelekwa bungeni na wenye uzalendo kuongeza 2% na kufikia 6% ya mrabaha na kutaka umma uwapongeze wazalendo hao kwa kazi kubwa ya kututoa kwenye 4% hadi 6% hao na Lissu nani mzalendo?
 
Watu mnajichanganya IMMMA advocates Lau Masha alishatoka siku nyingi sana! ..

itakayo fuatia kulipuliwa ni REX attorneys ...

Najua niko nje ya mada! Alexander Litvnienko najua nachofanya!
 
Embu turudi katika lugha yetu tutaangalia maneno mengi na maana zake lakini leo tutaanza na 'Uzalendo'. Binafsi najua maana moja naamini wapo wasiojua lugha kama mimi nao wanajua maana hiyo hiyo.

Nachojua ni kwamba 'Uzalendo' ni hali ya kuipenda nchi yako. Ukianza kuichambua maana hiyo utapata mambo mengi sana katika ndani yake ambayo yanaweza kukufanya uelewe zaidi juu ya uzalendo, tabia zake na kupata kumjua 'Mzalendo'. Nitaenda kusoma zaidi baada ya kupata mawili matatu kutoka humu.

Je wewe wafahamje kuhusu 'uzalendo'?, Mzalendo ni nani? Je neno 'uzalendo' linatumika katika level gani ya nchi au hata katika familia? Tabia za uzalendo ni zipi?

Twende pamoja tujifunze lugha yetu vizuri. Mifano na quotations mbali mbali zinasaidia sana kuelewa.
 
Ngoja nijaribu kujibu nijuavyo japo mimi sio mwanasiasa..

Mzalendo ni yule mtu ambaye yupo tayari kujitoa kwa nchi yake, kutetea maslahi ya watu wote na sio binafsi... Uzalendo unatumika level zote za nchi kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu na hata kwenye familia...

Tabia za mzalendo
-Anapenda nchi yake

- Msema kweli
- Anatetea maslahi ya umma sio binafsi
-Ana nidhamu
-Anasimamia kile anachokiona ni sahihi
-Hayumbishwi na misimamo hasi (Ana msimamo)
-Sio Muoga
-Anajitoa kwa kazi mbalimbali za kijamii
-Ni mtu wa watu
 
Natumai wote mu wazima.

Ili swali limekuwa likinisumbua kwa hivi karibuni,na hii nikutokana na maelezo tofauti toka kwa watu tofauti kuhusiana na Uzalendo/Mzalendo.

Recently tumepata reference mpya juu ya Uzalendo au Mzalendo. Kwasasa Mzalendo mkuu ni kiongozi wa juu kabisa wa serikali yetu,na kila anayemsupport naye uhesabika kama mzalendo.

Tukibase katika nchi yetu pendwa Tanzania, je mzalendo ni mtu wa aina gani? Na uzalendo hasa ni nini?

Vipi mtazamo wako wewe mdau kuhusiana na uzalendo?

Je,kuwa against kimtazamo na mambo yanayohusu nchi baina yako na viongozi wa nchi inakufanya usiwe mzalendo?? Au kuunga mkono 100% juhudi za serikali ni moja ya dalili za uzalendo??

My point is "Uzalendo ni nini na Mzalendo ni nani?"

[HASHTAG]#Analyse[/HASHTAG]
 
Ngoja nijaribu kujibu nijuavyo japo mimi sio mwanasiasa..

Mzalendo ni yule mtu ambaye yupo tayari kujitoa kwa nchi yake, kutetea maslahi ya watu wote na sio binafsi... Uzalendo unatumika level zote za nchi kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu na hata kwenye familia...

Tabia za mzalendo
-Anapenda nchi yake

- Msema kweli
- Anatetea maslahi ya umma sio binafsi
-Ana nidhamu
-Anasimamia kile anachokiona ni sahihi
-Hayumbishwi na misimamo hasi (Ana msimamo)
-Sio Muoga
-Anajitoa kwa kazi mbalimbali za kijamii
-Ni mtu wa watu
-Hukubali mapungufu yake na yu tayari kukosolewa
 
UZALENDO ni ile hali ya mtu kuipenda na kuithamini nchi yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele. Uzalendo ni neno dogo lakini maana inayobebwa na neno UZALENDO ni kubwa.

Elimu ya uzalendo ni elimu ambayo imekosekana kwenye jamii yetu. Hili linatokana na watu kutofundishwa kuipenda nchi yao. Upungufu huo ndio ambao hupelekea watu mbalimbali katika jamii kutenda mambo ambayo hushangaza watu na kuacha wengi katika mfadhaiko wa kujiuliza kama huyu mtu anaipenda nchi yake ama la.

Vitendo kama vya utoaji rushwa, upokeaji rushwa, upoteaji wa tamaduni (kutothamini kabila lako na chanzo chake), kutojiamini kama Mtanzania kwamba wewe ni bora kama wengine, wivu wa maendeleo uliyojikita kwa Mtanzania mwenzako na sio kwa mtu wa taifa lingine, kutothamini cha kwako na kutukuza cha mwenzako (Bidhaa za Tanzania, lugha ya Kiswahili, timu za mpira wa Ulaya) na kutojua ya kwamba utunzaji wa maslahi ya taifa lako ni jukumu lako na langu pia na sio la serikali pekee..
 
Kiufupi tu Uzalendo ni hali ya mtu kuwa na uchungu na nchi yake yaani kutokukubaliana kutoka moyoni na jambo lolote ambalo siyo sahihi linofanywa dhidi ya nchi yako na uwe tayari kukabiliana nalo kwa namna yoyote ile.
 
kuenenda ktk misingi ya haki,kufuata sheria,kusaidia,kuwa na upendo bila kunyanyapaa kikabila,kikanda n.k
 
Wadau nisaidieni uzalendo ni nini maana wamshabikiao jpm wanasema ni uzalendo waoneshao uozo wanaonekana si wazalendo je uzalendo ni nini?
 
Back
Top Bottom