engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,440
Wana jamvi,
Haya tunahitaji maoni yenu jinsi ya kuweza kutoa elimu ya uzalendo kwa mafisadi na wananchi kwa ujumla
Kwanza naomba mtambue nini maana ya uzalendo:
UZALENDO ni ile hali ya mtu kuipenda na kuithamini nchi yake na kuweka maslahi ya taifa lake mbele. Uzalendo ni neno dogo lakini maana inayobebwa na neno UZALENDO ni kubwa.
Elimu ya uzalendo ni elimu ambayo imekosekana kwenye jamii yetu. Hili linatokana na watu kutofundishwa kuipenda nchi yao. Upungufu huo ndio ambao hupelekea watu mbalimbali katika jamii kutenda mambo ambayo hushangaza watu na kuacha wengi katika mfadhaiko wa kujiuliza kama huyu mtu anaipenda nchi yake ama la.
Vitendo kama vya utoaji rushwa, upokeaji rushwa, upoteaji wa tamaduni (kutothamini kabila lako na chanzo chake), kutojiamini kama Mtanzania kwamba wewe ni bora kama wengine, wivu wa maendeleo uliyojikita kwa Mtanzania mwenzako na sio kwa mtu wa taifa lingine, kutothamini cha kwako na kutukuza cha mwenzako (Bidhaa za Tanzania, lugha ya Kiswahili, timu za mpira wa Ulaya) na kutojua ya kwamba utunzaji wa maslahi ya taifa lako ni jukumu lako na langu pia na sio la serikali pekee..
NAWASILISHA
MAPINDUZIIII DAIMAAAAAA