Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Paschal Katambi akiwatunuku zawadi Wakaguzi na Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Idara ya Uhamiaji waliofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi leo Machi 16, 2026 amesema kuwa ni wajibu kwa Jamii ya watanzania na Afrika na Dunia nzima kusimamia mmomonyoko wa Maadili kwani ndiyo chanzo cha rushwa, wizi, uvunjaji wa sheria, uwepo wa jinai na machafuko yote yanayotokea akisisitiza kuwa uzalendo na utaifa unaanzia katika ngazi ya familia.