Uyui, Tabora: Msafara wa Viongozi wa CHADEMA, wapata ajali wakiwa wanaelekea Kigoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Msafara wa Viongozi uliokuwa ukielekea Kigoma kwaajili ya maandalizi ya uzinduzi wa Oparesheni mpya ya Chama umepata ajali saa nane usiku wa kuamkia leo Aprili 27, 2023.

Ajali hiyo imetokea wilaya ya Uyui Tabora, Kata ya Kigwa, Waliopata ajali Yohana Kaunya Kaimu Katibu Mkuu Bavicha, Nuru Ndosi Naibu Katibu Mkuu Bawacha - Bara, David Chiduo, Josephat magambo na Daniel Marwa - Dereva.

Hakuna aliyefariki, wote wanapatiwa matibabu katika Zahanati Kigwa B,
Wilaya ya uyui.
IMG-20230427-WA0000.jpg
IMG-20230427-WA0001.jpg
IMG-20230427-WA0002.jpg
 
Msafara wa Viongozi uliokuwa ukielekea Kigoma kwaajili ya maandalizi ya uzinduzi wa Oparesheni mpya ya Chama umepata ajali saa nane usiku wa kuamkia leo Aprili 27, 2023.

Ajali hiyo imetokea wilaya ya Uyui Tabora, Kata ya Kigwa, Waliopata ajali Mhe. Yohana Kaunya Kaimu Katibu Mkuu Bavicha, Mhe. Nuru Ndosi Naibu Katibu Mkuu Bawacha - Bara, David Chiduo, Josephat magambo na Daniel Marwa - Dereva.

Hakuna aliyefariki, wote wanapatiwa matibabu katika Zahanati Kigwa B,
Wilaya ya uyui.
View attachment 2601073View attachment 2601074View attachment 2601075
Mungu asante kwa kuwapigania makamanda.. Mungu ibariki CHADEMA
 
Mungu asante kwa kuwapigania makamanda.. Mungu ibariki CHADEMA

Nawataka CHADEMA kumuomba radhi Makonda, wakikaidi watakutana na hasira ya Mungu
 
Poleni sana mliopatwa na ajali.

Kumbukeni kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa vifo vinavyotokana na ajali barabarani, licha ya ukweli kwamba ni nchi yenye magari machache. Umakini wa hali ya juu unahitajika sana unapokuwa barabarani.
 
Back
Top Bottom