Uwekezaji wa majengo haulipi

Kwa kizazi kijacho hakuna shida, ila wewe uliyewekeza ni sawa na umepoteza.
Sahihi na watu wanaamini zile laki tatu tayu
Mfano nina milioni 200, itanichukua miaka mingapi kuipata hiyo milioni 200 niliyoiwekeza?
nyumba hiyo kwa mwezi unachukua 1Milioni, kwa mwaka unapata 12milioni.

Itakuchukua miaka 20 mzee, na hapo tumezingatia kila mwezi una wateja na uhalisia hauko hivyo unaweza kukata miezi hata sita unatafuta wateja au miezi mitatu.
 
Umefafanua vizuri mkuu
 
Uwekezaji ni jambo la muda mrefu, ni sawa hata usipofaidika wewe wafaidike kizazi chako. Si kama maghorofa ya kariakoo tu
 
Haujui chochote kuhusu uwekezaji wa majengo. Acha kupotosha watu. Kajifunze
 
Inaonekana mtoa mada hana uzoefu kwenye huo uwekezaji wa real estate

Biashara ya lodge & hotel ni uwekezaji unaolipa (speaking from my own experience), nimewekeza kiasi huko

Niliwekeza shilingi 170M hivi awali, lakini baada ya miezi 14 hivi hela yangu ilirudi kupitia hiyo hiyo biashara ya lodge

Miaka miwili mbele, nikajenga lodge ya pili kupitia lodge ya awali

Ukipata location nzuri, biashara ya lodge haiwezi kukutupa

Jambo la kuzingatia, ni kufanya maintenances za mara kwa mara, shower ikiharibika, unatakiwa ukai-replace, sijui TV hainoeshi unatakiwa ukairekebishe ili wateja wasije wakaanza kukulalamikia

Niliwahi kupata wazo la mkumbo la kwenda kuziweka hizo hela kwenye hisa/bond n.k lakini nimegundua kupitia biashara hii ya real estate unapata return nzuri kuliko kwenda kuziweka hela huko..

Ukiwa na shida ya milioni 50 ama 70 unakwenda kukopeshwa na benki bila shida yeyote huku ukipata nafasi ya kupanua wigo wa biashara yako
 
Sawa mkuu
 
Mfano nina milioni 200, itanichukua miaka mingapi kuipata hiyo milioni 200 niliyoiwekeza?
hiyo nyumba tayari ni mtaji kama ulitumia million 200, basi miaka 5 mbele ukitaka kuiuza utakuta imeshafika 250 au 300. kwasababu ardhi pia inapanda thamani

sasa wewe unavyosema ukusanye tena kodi hadi zifike 200 unakosea namna ya kufikiri
 
hiyo nyumba tayari ni mtaji kama ulitumia million 200, basi miaka 5 mbele ukitaka kuiuza utakuta imeshafika 250 au 300. kwasababu ardhi pia inapanda thamani

sasa wewe unavyosema ukusanye tena kodi hadi zifike 200 unakosea namna ya kufikiri
Nyumba haipandi thamani
 
Baada ya miaka 5 uje utupe mrejesho wa hayo majengo
 
Kwa nini hoteli nyingi zinachakaa wakati zinaingiza fedha?
 
Leta elimu yako ukiwa na mchanganuo wa miaka 5
Ungekuwa na nia ya kuelewa ungejifunza kwanza kabla uya kuja kuandika hapa. Hata hivyo nitakupa dondoo chache.

1. Kwanza maintenance ya nyumba inafanyika baada ya miaka 15 au zaidi. Siyo kila baada ya miaka 5. Nyumba iliyojengwa vyema miaka. 10 bado mpya kabisa. Kwenye hotel unaweza badilisha furnitures baada ya miaka 6 to 7. Lakini rangi na fittings baada ya miaka 15. Cha msingi utumie mafundi wazuri na materials zenye ubora.

2. Nyumba ni uwekezaji wa muda mrefu. Hapa tunaongelea rerurn on investment (ROI) ya miaka 8 - 15 kutegemea na matumizi ya nyumba. Hotel/Lodge zinarudisha fesha haraka zaidi.

3. Ukijenga nyumba ya kupangisha ukiwa na miaka 40, ROI ya 10 years.. Ukabahatika kuishi miaka 60, 70 tayari unakula matunda ya uwekezaji wako.
4. Nyumba inaongezeka thamani ni kweli ingawa mimi binafsi hili huwa siliweki maanani, na siyo kipambele changu.

Sasa ngoja nikupe mfano
Mfano: Nunua kiwanja 30-50m. Tufanye 50m Weka. Nyumba 3, 2 za 2-bedroom na 2 za 1 bedroom na sebule, jiko choo. Fanya simple but quality., finishing nzuri. Hizi nyumba zitagharimu kiasi cha 80m. Kwa hiyo jumla ya uwekezaji wako ni 130m. Za 2 bedroom utapanganisha kwa 250,000 na bedroom utapangisha kwa 200,000. Makusanyo kwa mwezi 900,000. Jumla ya makusanyo baada ya miaka 10 ni. Kama 108m. Ni. Kwelihaijarudisha fedha. Lakini wenzako wanacholifanya hizo fedha za kodi kidogo kidogo wanaenda ku zi invest kwenye UTT na sehemu zingine za uwekezaji. So piga hesabu kama unawekeza 900000 kila mwezi kwa miaka 10.

tena utamu wa bongo nimkwamba unapokea pesa ya miezi 6 au 3 hivyo unawekeza fedha ambayo ungeioata miezi 6 ijayo ila wewe umpeipata leo na ku invest leo.

Kaa na maujinga yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…