Uwekezaji wa majengo haulipi

Uwekezaji wa majengo haulipi

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,104
Reaction score
55,512
Kuwekeza kwenye majengo ni sawa na fedha zako kuzifukia sehemu, na kuanza kuila kidogo kidogo mpaka iishe.

Na kula huko unakuwa hauli faida zaidi ya kula mtaji (fedha ulioiwekeza). Wengi ukimbilia kujenga nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k huku wakijipa matumaini majengo hayo yatawalipa na kupata faida zaidi na zaidi.

Kwa ujumla majengo hayo uwapa hasara, vinginevyo mmiliki hatonufaika zaidi ya kizazi chake kijacho ambacho ndio kitakuwa kinakula faida baada ya miaka kadhaa kupita.

Ukitaka kuamini hili, tembelea nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k zipe miaka mitano alafu ukazitembelee tena, utazikuta zimechoka na kama hakutokuwa na hela ya ziada ya ukarabati, ndio hivyo biashara inakuwa imekufa.​
 
Ila nijuavyo ardhi haishuki thamani
Kwenye majengo jenga simple stractues kuepuka uwekezaji mkubwa huku fashion zikikimbia mno
Uko sahihi, tembelea hapo mjini zile hoteli zote zilizokuwa tishio miaka mitano iliyopita, ukizikagua ndani na nje utagundua uchakavu, kwa sababu fedha za kurudisha upya wa majengo hayo ni kubwa.​
 
Uko sahihi, tembelea hapo mjini zile hoteli zote zilizokuwa tishio miaka mitano iliyopita, ukizikagua ndani na nje utagundua uchakavu, kwa sababu fedha za kurudisha upya wa majengo hayo ni makubwa.​
Watanzania biashara au uwekezaji wetu huwa tunafikiria kwa muda mfupi, na muda wote tunataka super profit tena kwa muda mfupi iwezekanavyo. Ndiyo maana unakuta dalali anataka akiuza nyumba, ile faida anayopata akajenge nyumba yake. Ndiyo, najua shilingi yetu huteremka thamani sana, lakini duniani kote ukiwekeza kwenye nyumba huwezi kutegemea fedha ulizojengea zirudi kwa muda mfupi. Chukulia hivi. Nyumba haishuki thamani, na ile kodi unayochukuwa kila mwezi ndiyo faida yako. Yaani kama unachukuwa milioni mbili, basi hiyo ndiyo faida yako, na mtaji wako unabaki kama ulivyo. **nyumba ikijengwa kitaalam na eneo zuri inachukuwa muda kufanyiwa marekebisho makubwa. Kutoka kwenye kodi weka asilimia ndogo kila mwezi ambayo itafanya ukarabati wakati ukifika. Ila ukijenga kibongo-bongo miaka 10 tu unakuta nyumba inadai kubomolewa ijengwe nyingine.
 
Napingana na wewe mkuu, uwekezaji wa ardhi ndo kila kitu, hizi biashara za kufungua sijui duka, au kununua magari ya usafiri kuna mda unaweza kuwa maskini ndani ya lisaa limoja.

Uwekezaji wa kwenye ardhi utakula mda mrefu hata kama huna nguvu za kufanya kazi, upo na ulemavu na mengineyo. kuhusu ukarabati hilo ni jambo la kawaida
 
Ile kodi unayoipata pale sio faida, unatakiwa utoe gharama zote za uendeshaji ndipo ujilipe kama faida. Ni sawa na umenunu basi kwa milioni 300 na ukaliweka barabarani, ile nauli ya abiria sio faida. Faida itapatikana baada ya kutoa fedha uliyowekeza.
 
Napingana na wewe mkuu, uwekezaji wa ardhi ndo kila kitu, hizi biashara za kufungua sijui duka, au kununua magari ya usafiri kuna mda unaweza kuwa maskini ndani ya lisaa limoja.

Uwekezaji wa kwenye ardhi utakula mda mrefu hata kama huna nguvu za kufanya kazi, upo na ulemavu na mengineyo. kuhusu ukarabati hilo ni jambo la kawaida
Ni kweli ardhi ndio kila kitu, ila unachokiweka juu ya ardhi sio kila kitu.
 
Kuwekeza kwenye majengo ni sawa na fedha zako kuzifukia sehemu, na kuanza kuila kidogo kidogo mpaka iishe. Na kula huko unakuwa hauli faida zaidi ya kula mtaji (fedha ulioiwekeza). Wengi ukimbilia kujenga nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k huku wakijipa matumaini majengo hayo yatawalipa na kupata faida zaidi na zaidi. kwa ujumla majengo hayo uwapa hasara, vinginevyo mmiliki hatonufaika zaidi ya kizazi chake kijacho ambacho ndio kitakuwa kinakula faida baada ya miaka kadhaa kupita. Ukitaka kuamini hili, tembelea nyumba za kupanga, 'apartment', hoteli, nyumba za kulala wageni n.k zipe miaka mitano alafu ukazitembelee tena, utazikuta zimechoka na kama hakutokuwa na hela ya ziada ya ukarabati, ndio hivyo biashara inakuwa imekufa.​
CC RRONDO Extrovert mrangi

adriz de mbusii
 
Mzee wangu ange kusikiliza wewe, leo hii intelli ningekuwa muokota makopo.

Mtu mpaka ana Jenga lodge, nyumba za kupangisha, jua amesha piga hatua na uwekezaji huo sio wa mwaka 1 au miwili ni mbeleni huko.

miji inakua na kubadilika, kuna maeneo ukitega itakulinda wewe au kizazi chako.
Screenshot_20260302_140641_Chrome.jpg
 
Mzee wangu ange kusikiliza wewe, leo hii intelli ningekuwa muokota makopo.

Mtu mpaka ana Jenga lodge, nyumba za kupangisha, jua amesha piga hatua na uwekezaji huo sio wa mwaka 1 au miwili ni mbeleni huko.

miji inakua na kubadilika, kuna maeneo ukitega itakulinda wewe au kizazi chako.
Kwa kizazi kijacho hakuna shida, ila wewe uliyewekeza ni sawa na umepoteza.
 
Back
Top Bottom