Uwazi ni kanuni ya msingi kwa Waandishi wa Habari wakitarajiwa kutoa Taarifa kwa Umma ili Wananchi waweze kufanya maamuzi sahihi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Waandishi wa habari mara nyingi huandika matukio ya kisiasa na matendo ya wanasiasa, na wanasiasa hutegemea utangazaji wa vyombo vya habari kuwasiliana na umma. Hata hivyo, kudumisha tofauti ya wazi ya majukumu ya waandishi wa habari ni muhimu kwa utendaji wa demokrasia yenye afya, ambapo wananchi wanapata habari zisizo na upendeleo ili kufanya maamuzi sahihi kuhusu serikali na viongozi wao.

Uwazi ni kanuni ya msingi kwa Waandishi wa Habari wakitarajiwa kutoa Taarifa kwa Umma ili Wananchi waweze kufanya maamuzi sahihi. Wajibu wa Msingi wa Tasnia ya Habari ni kuhabarisha Umma na kuwawajibisha walio Madarakani kwa kutoa taarifa sahihi na zisizo na upendeleo

Wanahabari wanapaswa kuepuka Migongano ya Kimaslahi, Kujiepusha na misimamo ya Kisiasa, na kuripoti Taarifa bila kupendelea kikundi au itikadi yoyote

Wanabeba jukumu la kuwawajibisha Viongozi walio Madarakani kwa kuchunguza na kuripoti Vitendo vyao, Sera na Shughuli za Serikali. Pia, kuhoji Mamlaka, kufichua Ufisadi, na kuchochea Uwajibikaji Serikalini.
 
Back
Top Bottom