SoC03 Uwajibikaji mbovu wa watoa huduma kwa wateja

Stories of Change - 2023 Competition

Ibudigital

JF-Expert Member
May 11, 2020
323
653
Heshima kwenu wakuu.

Leo nimeona tuzungumzie kuhusu baadhi ya watoa huduma kwa wateja kutoka kwenye makampuni/biashara mbali mbali wanavyosababisha kero kubwa kwa wateja wao kutokana na uwajibikaji wao mbovu kabisa! Niliwahi kusikia malalmiko mengi sana kutoka kwa watu tofauti kuhusu kupewa majibu mabovu na baadhi ya watoa huduma pale wanapoenda kufuata huduma fulani. Mwanzo nilijua sio kweli, lakini hili janga lilipokuja kunipata na mimi ndipo nilipoamini kile nilichokisikia mwanzo.

Sijui ni kwanini, lakini kuna wakati unaweza kwenda kwenye kampuni fulani au hata duka tu la kawaida kwaajili ya kupata huduma, unaweza kupokelewa vizuri lakini ghafla majibu ya mtoaji huduma yakaanza kubadilika na kuwa ya kero kulingana na huduma/bidhaa unayohitaji. Hii inashangaza sana kwasababu wakati mwingine utakuta unalipia kiasi kikubwa ili kupata huduma unayohitaji, lakini bado unapewa majibu ya kuudhi sana au kuangaliwa kwa jicho baya kama vile unafukuzwa mahali hapo. Katika uchunguzi wangu niliofanya niligundua baadhi ya vitu vinavyosababisha baadhi ya watoa huduma kujibu majibu ya maudhi kwa wateja wao, ila inasikitisha kwasababu ni sababu za kijinga sana na zisizo na maana;

  1. Ukiuliza maswali mengi wakati wa kuhitaji huduma/bidhaa.
  2. Ukinunua bidhaa/huduma ya gharama ndogo.
  3. Ukionekana ni mtu wa kuchagua sana.
  4. Ukionekana huna usafiri (inaumiza sana).
  5. Wakijua una umri mdogo.

1.) Ukiuliza maswali mengi wakati wa kuhitaji huduma/bidhaa.

Mimi sijui ni kwanini hiki kitu kinawaudhi watoa huduma na kuwafanya wakujibu ovyo! Kwasababu haiwezekani uende kupata huduma fulani au kununua bidhaa pasipo kuuliza maswali. Chaajabu ni kwamba unaweza kuulizwa maswali yasiyozidi tano lakini ukaanza kununiwa na kujibiwa kero hadi ukawaza labda hawataki upate huduma/bidhaa zao.

2.) Ukinunua bidhaa/huduma ya gharama ndogo.

Sababu hii inachekesha mno na kusikitisha pia! Nakumbuka siku moja tulipoenda kununua bidhaa za dukani (duka la urembo wa kina dada) kariakoo mimi na mama yangu kipenzi kwasababu yeye ndio anafahamu vitu hivyo vingi. Tulipofika hapo dukani tulipokelewa na mama mmoja mwenye asili ya kiarabu, mama yangu akaanza kuulizia vitu tofauti kutokana na orodha tuliyokuwa tumeandika kwenye karatasi. Aliulizia bidhaa moja moja akiomba atajiwe na bei, ila sitasahau jinsi yule mama alivyomtizama mama yangu kwa jicho la hasira na kumuita kijana wake akamuambia "ebu sikiliza huyu mama!" Aise! Mama yangu ni mvumilivu sana. Yule kijana kidogo alikuwa mstaarabu akajibu vyema, baada ya kujiridhisha na kukubaliana kwa bei nzuri ya jumla (hilo duka ni la jumla tu) mama yangu aliagiza vitu vya milioni moja na laki tatu (Tsh 1,300,000). Huwezi amini yule mama wa kiarabu alivyosikia oda yetu alirudi kwa mama na kumkaribsha upya! Tena alimkaribisha na hadi wakabadilishana namba za simu ili mzigo wa dukani ukiisha mama ampigie simu chapu. Sasa si ujinga huu? Inamaana mtu ukienda kununua hereni za elfu kumi (Tsh 10,000) utajibiwa vibaya sio? Haya ni maudhi makubwa mno na inapaswa tuheshimu kila mtu, kama hawathamini wateja wadogo basi wasiuze bidhaa za Tsh 100/200.

3.) Ukionekana ni mtu wa kuchagua sana.

Hii nayo ni kero nyingine kwasababu huwezi kuweka bidhaa zaidi ya moja dukani kwako, au kuwa na huduma zaidi ya moja na ukakasirika pale ambapo mteja atachagua kimoja wapo. Kuna watoa huduma wanaanza kukujibu vibaya wakikuona unachagua bidhaa tofauti tofauti, yaani hao wanataka ufike pale utaje unachohitaji, upatiwe, ulipe, na uondoke! Hii haipo. Wameweka huduma tofauti na bidhaa tofauti kwahiyo mteja anao uhuru wa kuchagua nini anataka, wajirekebishe katika hili pia.

4.) Ukionekana huna usafiri (inaumiza sana).

Hii nayo ni kweli kabisa! Inaumiza sana ingawa ni ushamba wa hali ya juu na kupoteza wateja tu. Tabia hii asilimia kubwa wanayo walinzi wa makampuni mbali mbali. Unaweza kwenda sehemu fulani kuhitaji huduma/bidhaa ukiwa huna gari na mlinzi akakukataza kuingia ndani kwasababu tu umeenda kwa miguu! Sasa sijui walitaka uende na gari na uiingize hadi hapo mapokezi kabisa! Hii kitu imewahi kunipata kwenye ofisi fulani maeneo ya Mwenge, Dar Es Salaam nilipoenda kuwasilisha barua za mambo ya masoko, niliwasiliana na afisa masoko wa ofisi hiyo na akanipa mawasiliano ya katibu wake ili nikifika pale nimpatie hiyo barua. Aise, ilibaki kidogo nipigwe virungu na mlinzi aliyekuwa pale! Kila nikijaribu kuelezea kuwa nimewasiliana na katibu wa bosi wake hanielewi kabisa hadi ikabidi nimpigie simu huyo katibu akaongea na mlinzi wao ndio nikaruhusiwa kuingia. Chaajabu ni kwamba, muda wote huo walikuwa wakiingia wenye magari wanulizwa swali moja tu "Karibu, unaenda ofisi ipi?" wanataja ofisi na wanaingia bila tatizo lolote. Huu nao ni ujinga wa hali ya juu, wapo wengi wenye usafiri binafsi tena za mamilioni ila wakati mwingine wanaamua kutembea kwa miguu kwa sababu zao binafsi.

5.) Wakijua una umri mdogo.

Hapa ndo unaweza ukalia! Kuna watoa huduma wana dharau sana haki ya Mungu! Yaani unaweza kwenda kwenye ofisi ya mtu/kampuni/duka/nk na akakuona vizuri kabisa kisha akachukua simu yake na kuanza kumpigia mtu simu, tena akakuambia subiri kidogo na anaongea kwa kelele kabisa akiwa anacheka! Wakati mwingine unaweza kufika hapo akachukua chakula na kuanza kula, na hapo utamsubiri hadi amalize kula. Huu ujinga wanawafanyia vijana wadogo, anajua kabisa huyu kijana hawezi kuzungumza chochote. Ni dharau kubwa sana na inaweza kuwapotezea wateja.

Kwa leo tuishie hapo.

Haya mambo yapo jamani, labda hujawahi kukutana na hizi kero lakini ipo siku tu utakutana nazo. Kwasababu wakati mwingine hawa watoa huduma wanakujibu vibaya hata kwenye simu tu! Inaumiza sana kwasababu wanamjibu vibaya mtu ambae ndio wanamtegemea wamuuzie huduma/bidhaa zao ili maisha yasonge.

Huu ni uwajibikaji mbovu sana kwa hawa watoa huduma, wanajipotezea wateja wenyewe tena kwa asilimia 100% na kisha huko nje wanalalamika kuwa bisahara ni ngumu. Biashara haiwezi kuwa rahisi ikiwa wewe mwenyewe unakuwa mgumu kwa mteja wako, haijalishi mteja amekuja na muonekano gani kwenye biashara yako, hebu msikilize kwanza ni kitu gani kimemleta hapo.

Tujitahidi sana kuepuka kero hizi tunapokuwa na biashara zetu, kwasababu mteja anaangalia nidhamu ya mtoa hudumua pia, sio ubora wa bidhaa pekee. Unaweza kujiweka mahali paya na kujilaani tu mwenyewe kwa kulia kilasiku kukosa wateja, kumbe shida ni wewe mwenyewe.

Tuboreshe uwajibikaji wetu kwa wateja ili kuweza kufikia lengo katika biashara zetu/kampuni/nk. Asanteni wote kwa kusoma, nakaribisha maoni yenu.
 
Good
 
Back
Top Bottom