Hoteli za Morena na Huduma Mbovu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
Tuna kawaida mtu akiandika kitu cha kugusa mahala fulani utasikia umetumwa

Mimi naandika haya ambayo nimetendewa na nimeona hii ni fursa ya kuwasilisha dukuduku langu

Huenda nisifunguke sana lakini ITOSHE KUSEMA MORENA HOTELS hasa Morogoro MJIREKEBISHE SANA.

Huduma zenu ni mbovu sana na za KIBABE na si mimi tu nimetendewa, hapo nimeshuhudia watu wengi wakihama kwa HUDUMA MBOVU.

  1. Kubagua wateja
  2. Majibu ya kifedhuli na kihafidhina
  3. Huduma kuchelewa
  4. Kulisha watu vyakula vilivyooza
  5. Kudai pesa kila siku hata kwa mteja anayeendelea

Nasikitika kwa sababu hoteli bado mpya lakini huduma hazisadifu uendelevu wake........mtu unaenda kwa moyo kukaa hapo unafika mhudumu utadhani ndiye MTEJA NA WEWE MTEJA UNAGEUKA KAMA MHUDUMU.

Mlichonifanyia MUNGU ATAHUKUMU

1707007486268.png
 
Wanaoongoza kwa jeuri na maringo siku zote ni waaajiriwa....

Sio maofisini, Safarini, mahotelini..
Mhusika mwenyewe hana hizo mambo, nenda kwa mpokea mshahara sasa..

Background ndio inawatesa Sana waajiriwa wa namna hio.
 
Mimi naandika haya ambayo nimetendewa na nimeona hii ni fursa ya kuwasilisha dukuduku langu mojawapo
[*]Kudai pesa kila siku hata kwa mteja anayeendelea
Sasa kama Unaendelea si ulipe kabisa siku zote utakazokaa? Au uwe unalipia Kila siku.Ulitaka ukope kijanja halafu utokomee gizani pesa Yao wangepata wapi? Lipa kabisa ndio ulale siku husika
 
Wanaoongoza kwa jeuri na maringo siku zote ni waaajiriwa....

Sio maofisini, Safarini, mahotelini..
Mhusika mwenyewe hana hizo mambo, nenda kwa mpokea mshahara sasa.
Mhusika akishindwa kuwasimamia wafanyakazi basi yeye ndiye anapaswa kulaumiwa. Asijifiche kwenye kile kivuli ambacho watanzania tumezoewa kusikia.... ''rais anaangushwa na wasaidizi wake.. ''.
 
Tatizo la waajiriwa ni kulipwa mshahara badala ya kamisheni. Mtu angelipwa kamisheni, angeheshimu sana kazi. Mshahara unafanya watu wawe wavivu na wenye viburi.
Mkuu kuna mengine. Tanzania huduma kwa wateja ni majanga. Nenda popote. Hata mfanyakazi alipwe nini, ila tumeshajijengea utamaduni wa kudharau wateja. Nadhani hii ilianza kipindi cha ujamaa wakati vitu vilikuwa vimeadimika na huduma nyinge zikiwa zinatolewa na serikali na sekta zake. Bado hujaweka tatizo jingine la wizi na uvivu.
 
Aisee imekuaje tena, mahotelini ndo kunaongoza kua na customer care nzuri. Hata mtu aende kavaa hovyo ila ukaribisho wake mpaka yeye anajihisi tofauti.
Na mimi hapo hawanipati, cha kwanza kabisa nachoangalia kabla ya huduma ni hiyo customer care.
 
Hospitality industry imevamiwa na cheap labour na unprofessionals.
Ni ngumu sana kupata value for money kwenye hizi hotels zinamilikiwa na wabongo na kuajiri wafanyakazi wote wa Kibongo.
Ni shiidaa maisha ya dhiki ya wafanyakazi wanayaleta hadi kwenye hotels za watu.
Inakera sana.
 
Tatizo ni kuajiri watu wasiopitia mafunzo ili walipwe kiduchu kumaximize faida
Wabongo wanapenda ubahiri kwenye biashara wakiamini ndio kufanya maximization of profit.

Huwezi maximize profit ambayo haipo, ambayo unaikwepa na kuikataa kwa makusudi. Unakuta manager waiting room ya wateja anasema usiwashe AC umeme unaenda sana, akiamini amebana matumizi kumbe ndio anafukuza watu kwa experience mbovu wanayopata wakija.

Mtu anaajiri kilaza amlipe kidogo eti asitumie gharama nyingi, wakati in return huyo kilaza ataleta wateja wachache na hatokiwa na customer retention nzuri. Au mmiliki anagoma kabisa kutoa bonus na zawadi kwa wafanyakazi akiamini amebana matumizi kumbe amepunguza kujituma na ufanisi wa kazi wa watu wake.

Ujingaujinga tu
 
Mtanzania hata umpe mafunzo mpaka mbinguni, kwenye huduma kwa wateja ni sifuri.
Sio kweli mkuu,mtanzania ni hard worker ila tatizo hawa employers wengi ni mafedhuli, na wakati mwingine hawa ma HRs wetu ni vibaraka na roho mbaya, wakati DSM Sheraton Hotel wanaendesha ile hotel pale, kulikua na zaidi ya 260 staff's, ILA wote walikuwa level moja,GM alikua anakula kwenye staff canteen, hii ilileta kitu tofauti kwa staff's, ndio maana services pale ilikua top class, lakini sasa mafisadi yanapiga hela, kila baada ya miaka 5 eti kuna mwekezaji mpya!!!
 
Back
Top Bottom