Uvutaji sigara kwenye maeneo ya wazi umepigwa marufuku katika mji wa Milan nchini Italia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Uvutaji sigara kwenye maeneo ya wazi umepigwa marufuku katika mji wa Milan nchini Italia.

Kulingana na uamuzi wa Manispaa ya Milan, uvutaji sigara hautaruhusiwa katika maeneo ya wazi, bustani za umma, viwanja vya michezo, makaburi na vituo vya mabasi endapo kutakuwa watu wengine waliosimama ndani ya masafa ya mita 10.

Wavutaji sigara watakaovunja marufuku hayo watatozwa faini ya fedha hadi euro 240.

Mji wa Milan ambao ni moja ya miji iliyo na uchafuzi mkubwa wa hewa nchini Italia na Ulaya, ulichukuwa uamuzi huu wa marufuku ili kupunguza uchafuzi wa mazingira na kulinda afya ya umma.

Lengo la umauzi huo pia ni kupanua wigo wa marufuku ya kuvuta sigara katika miaka ijayo, na kupiga marufuku kikamilifu uvutaji sigara katika mji huo ifikiapo mwaka 2025.

Ndani ya mwaka ujao, kumepangwa kuchukuliwa hatua za kuweka marufuku ya fataki na uchomaji nyama nje pia.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni, miji ya Milan, Torino na Napoli nchini Italia ni kati ya miji iliyo na kiwango kikubwa cha chembe za PM10 (zinazosababisha uchafuzi wa hewa na kuharibu mapafu) katika Jumuiya ya Ulaya.
 
Hatari sana, huku kwetu naona viwango vya uvutaji wa sigara sio vikubwa sana.
 
Ukifika Iringa mjini,ingia hotelini washa sigara uvute ,subiri kitakachofuata.Najua mhusika utakasirika sana na kupiga kelele sana,lakini pale Iringa watu wengi watakushangaa sana maana ustaarabu wa kutovuta sigara hadharani ni wa siku nyingi sana.
 
Back
Top Bottom