Asili ilivyobadilisha ‘Mji wa Upepo wa Wuerhe’ na kuunda miamba yenye maumbo ya kustaajabisha

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
微信图片_20230731144217.jpg

Kadiri unavyotaka kuujua kwa undani zaidi mkoa wa Xinjiang Uygur, China, ndivyo mkoa huu unavyoendelea kukuacha mdomo wazi, na kama ulidhani kwamba unaujua vizuri, basi kuna mambo mengi ya kushangaza ambayo bado hujayaona. Huo ndio mtazamo wangu baada ya safari hii kutembelea kwenye maeneo ya kustaajabisha na kugundua mambo mengi mapya.

Leo tuliingia tena barabarani na kuwa na safari ndefu kiasi hadi kwenye ‘Mji wa Mashetani’ ama wengine huuita ‘Mji wa Upepo wa Wuerhe’. Eneo hili lililopo sehemu za chini ya Mto Jiamu kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi wa Bonde la Junggar wilayani Karamay mkoani Xinjiang, ni maarufu kwa kuwa na mandhari ya kipekee ya mmomonyoko unaotokana na upepo na maji. Chanzo cha jina hili la Mji wa Upepo wa Wuerhe kinatokana na kwamba sehemu hii ina upepo mkubwa ambao umeleta sura mpya ya eneo hili. Ingawa unaitwa mji, lakini kimsingi huu sio mji halisi.

Kwa mujibu wa wenyeji waliotupatia maelezo ya mji huu, wakati wa kipindi cha ‘Cretaceous’ karibu miaka milioni 100 iliyopita, mahali hapa palikuwa na ziwa kubwa lenye maji safi. Na kutokana na hali ya hewa yake ya joto na unyevunyevu, eneo hilo lilikuwa kama pepo kwa dinosauri. Kwa vile mahali hapa kunapatikana visukuku vingi vya dinosaur, vielelezo kadhaa vya dinosaur pia vimewekwa hapahapa, ambapo baadhi vikiwa vimesimama kwenye mwamba na vingine vikiwa vimelazwa.

Baada ya harakati nyingi za kujiunda kwa gamba gumu, likapatikana eneo hili la Gobi ambalo limeshehi miamba na vilima. Upepo katika mji wa mashetani unavuma kila siku. Katika siku za kale, hapakuwa na barabara inayounganisha eneo hilo na ulimwengu wa nje na hapakuwa na makazi katika eneo jirani. Hivyo upepo mkubwa au dhoruba za mchanga zilipoibuka, zilinguruma katikati ya mji zikitoa sauti kama mizimu huku mchanga na vumbi likitanda kwenye anga. Sauti hizi za kelele zilizidi kusogea karibu na watu na wakati mwingine zilikuwa kali ama wakati mwingine zilikuwa zikitoa kama mlio wa mbwa mwitu ambao ulifanya watu wasisimke mwili na vinyweleo kuwasimama.

Upepo huu uliochanganyika na mchanga uliumiza sana wakati ukipiga kwenye uso. Hivyo watu hawakuweza kufumbua macho huku mchanga wa manjano ukijaa mdomoni, masikioni na shingoni. Na upepo ulipoacha kuvuma watu walihisi kama wamenusurika kwenye makucha ya shetani. Ndio maana jina la mji wa shetani likapatikana.

Upepo huu mkali ulipeperusha mchanga na kuibua tabaka la mji wa mashetani, ambapo matokeo yake miamba mikubwa yenye maumbo mbalimbali ikajichonga. Baadhi ya miamba inafanana na majumba, mahekalu, mabanda na minara ya ukuta wa mji, huku mingine ikifanana na wanyama kama simba, farasi, kasa, na tai. Ukitembea katika mji huu wa mashetani utaona jinsi asili ilivyounda upya majengo mengi maarufu duniani.

Bahati nzuri nilipofika mahali hapa nilishuhudia kwa macho yangu miamba inayoonekana kama simba wapenzi wa baharini wakitazama mwezi huku wakiwa wamekaa ana kwa ana. Na hapa pia unaweza kuona umbo la tausi mzuri akitandaza mkia wake huku akiwa kama anasubiri kuwasili kwa watalii.

Wenyeji wanaamini kwamba kama ulikuwa unaandamwa na mikosi na mabalaa, ukitembelea katika mji huu basi unaweza kuiacha mikosi na mabalaa yote hukohuko. Katika mji huu wa mashetani ambao unafunguliwa kwa ajili ya watalii kujionea maajabu ya ulimwengu, mtu anaweza kupata hata usafiri wa ngamia. Pia kunakuwa na maonesho ya wapanda farasi na hata unaweza kuona mifupa ya dinosaur ambayo ni ya bandia.

Mkoani Xinjiang, kawaida jua huwa linachelewa sana kuzama wakati wa majira ya joto. Hivyo kabla ya kumaliza siku yetu katika mji huu wa mashetani, ilipofika saa tano za usiku muda ambao ndio jua linazama, tuliandaliwa maonesho ya dansi na ngoma za kienyeji, pamoja na kula vyakula vitamu vya aina mbalimbali ambavyo ni maarufu sana huko mkoani Xinjiang.
 
Nimependa kusikia kuhusu mji huo wa Wuerhe, ama mji wa Mashetani kutoka huko Uchina. Ni makala nzuri na uandishi wa ubunifu na kuvutia haswaa.
 
View attachment 2704324

...Miaka Milioni 100 iliyopita ?? Nani alikuwepo ?? Hadithi Njoo....!
 
Back
Top Bottom