Maeneo Yaliyotengwa Kwa Ajili Ya Uwekezaji Katika Manispaa Ya Moshi

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Ada za kuomba kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Moshi.

(i) Maombi mapya ya kibali cha ujenzi cha;-

✓ Makazi ni Tshs.400 kwa mita mraba moja.

✓ Makazi na biashara ni Tshs.500 kwa m².

✓ Viwanda ni Tshs.400 kwa mita mraba moja.

✓ Taasisi ni Tshs.300 kwa mita mraba moja.

✓ Vituo vya mafuta ni Tshs.600 kwa mita mraba moja.

(ii) Maombi baada ya muda wa kibali wa mwaka mmoja kuisha;-

✓ Makazi ni Tshs.400 kwa mita mraba moja.

✓ Makazi na biashara ni Tshs.500 kwa m².

✓ Viwanda ni Tshs.400 kwa mita mraba moja.

✓ Taasisi ni Tshs.300 kwa mita mraba moja.

✓ Vituo vya mafuta ni Tshs.600 kwa mita mraba moja.

(iii) Kibali cha ukarabati wa;-

✓ Nyumba pembezoni mwa mji na sio katika eneo la CRDB ni Tshs.50,000.

✓ Nyumba ya ghorofa pembezoni mwa mji na katika eneo la CRDB ni Tshs.100,000.

(iv) Kibali cha ujenzi wa nguzo ya kushikilia au kutumika kubandika matangazo ya biashara ni Tshs.100,000.

(v) Kibali cha ujenzi wa mnara wa simu ni Tshs.500,000.

(vi) Kibali cha kuvunja JINGO katikati ya mji ni Tshs.500,000.

(vii) Ada za kibali cha kuweka nguzo za matangazo.

✓ Nguzo ndogo zenye kipenyo cha chini ya futi moja ni Tshs.100,000.

✓ Nguzo yenye kipenyo cha zaidi ya futi moja ni Tshs.200,000.

Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika manispaa ya Moshi.

(a) Kujenga jumba la makumbusho, kituo cha burudani na tamaduni katika eneo la Uhuru Park.

(b) Kujenga kituo cha michezo na uwanja wa michezo wa Jamuhuri. Limetengwa eneo la hekta 15.7.

(c) Kujenga soko la kisasa la biashara maeneo ya Mbuyuni (hekta 0.63 zimetengwa).

(d) Kujenga kituo cha biashara katika kata ya Mawenzi na eneo la Shanty Town.

(e) Kujenga kituo cha uchapaji eneo la Kaloleni. Eneo la ukubwa wa hekta 3.5 limetengwa.

(f) Kujenga kiwanda cha kusindika nyama eneo la Moshi kati. Eneo la ukubwa wa hekta 2.99 limetengwa kwa ajili ya kiwanda cha nyama.

(g) Kujenga kituo cha kutolea ujuzi wa kusindika mazao ya bustani (horticultural crops).

(h) Kujenga kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi katika eneo la Soko estate.

(9) Ada ya kubadili matumizi ya ardhi katika manispaa ya Moshi.

(a) Makazi kuwa biashara ni Tshs.200,000.

(b) Makazi kuwa viwanda ni Tshs.250,000.

(c) Biashara kuwa viwanda ni Tshs.250,000.

(d) Kugawanya kiwanja/shamba ni Tshs.50,000.

(e) Kubadili miliki kwa maeneo yasiyo ya Hati ni Tshs.50,000.

(f) Matumizi mengine ambayo hayajatajwa ni Tshs.50,000.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

WhatsApp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom